Ajali ya gari iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Mabungo nje kidogo ya mji wa Moshi ikihusisha lori la mafuta lenye namba za usajili T 391AFA na Toyota Hilux lenye namba T133 AQX. Hakuna taarifa iliyotolewa juu ya vifo au majeruhi walitokana na ajali hiyo.

Wakazi wa eneo hilo inaonekana somo lililotokea kata ya Isongole mkoani Mbeya halikuwaingia ,wakaendelea na utaratibu wa kuchota mafuta bila kujhali kuwa wanahatarisha maisha yao. Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
nani aanze....wananchi wanajiuliza
wa kwanza mwenye dumu la njano aliposhuka tu, hao....
mwenye ndoo, haya...mwenye dumu, hayaaaa mradi kila mtu alishuka kuchota wese la bure
hapo kibiriti chwaaa! kwishnehi...
hilux hoi bin taaban
bahati hakuna aliyepoteza maisha









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. mmmm!mwe!mwe! kweli Bongo Tambarale,na mungu yupo pamoja nasi

    ReplyDelete
  2. hivi haya mahilux ya kisasa yametengenezwa kwa maboksi au makaratasi duu

    ReplyDelete
  3. AKILI KWELI NI MALI, HAPO AKIPITA MVUTA FEGI TU NI MAAFA YASIYOSEMEKA. HATA KAMA NI UMASKINI, NDOO MOJA YA WESE ITAKUSAIDIA NINI MAISHANI?

    ReplyDelete
  4. Hiyo sehemu ina kakona hivi na ka slope harafu mbele kuna daraja, hatari sana hapo kama unajidai wewe ni Michael Schumacher lazima ulambe tope. Poleni wahanga na hongereni kwa Israel kutowapitia maana ajali ni mbaya sana. Mkatoe shukrani ya pekee huko mnakoabudu.

    Drive safe to rescue life.

    ReplyDelete
  5. Mr michuzi yule mama sijui ni mzambia huwa anakaa na watoto wake wanne pale ufukwe wa ocean road jirani na agha khani leo bado nusu nipate ajali nilipokuwa nashangaa baada ya kumwona ana mimba nyingine kubwa
    wanaume tuache tabia chafu nidhambi kama wanaompachika ni vichaaa basi wasamalia wema wamtoe kizazi ili asiwatese watoto wasio na hatia kwa jua na mvua nawakilisha

    ReplyDelete
  6. HIVYO TV KAMA TBC NA TVT ZINAFANYA NINI NCHINI TANZANIA? KATIKAK UELIMISHA JAMII KWENYE TV KUHUSU MAMBO KAMA HAYA? WANANCHI NA WAJUMBE WAO WANAWAFUNDISHA NINI WANA VIJIJI? KWANINI SIE BADO TUNARUDI NYUMA TU? TUNACHOKIJALI KWENYE MA TV YETU NI MISS TANZANIA SHOW NA FASHION SHOW BASI, ELIMU ZENGINE ZAK UJIKINGA NA MABALAA HATUONESHI. MASUDI.

    ReplyDelete
  7. Poor Tanzanians. Hawa jamaa sio kwamba hawathamini maisha yao bali hali ya kimaisha ni mbaya sana, mtu bora afe kuliko kukosa dili la buku, kwani hujaona watu wanang'oana meno kisa wamedhurumiana sh 100. Inasikitisha sana, ila hiyo ndiyo inaonyesha hali halisi ya maisha ya Watanzania walio wengi. Bado maadui watatu aliowasema Baba wa Taifa wanatuandama kwa kasi kubwa na kwa kila hali inaonyesha tumeshindwa kuwakabili. Kwakweli Watanzania bado sana. Nadhani ktk kila Watanzania 100 watakaoona gari la mafuta limeanguka 85 watalikimbilia ili wachote mafuta yanayotiririka. Kwani hamjawaona watu Dar es Salaam wanaofungua matanki ya magari yanayobeba mafuta yanapokuwa kwenye foleni na inakuwa ni mchana na hakuna anayejali, na wakati mwingine matrafiki wanakuwa hapo hapo.

    Bado kazi kubwa sana ipo mbele yetu katika Taifa hili ambalo kila siku tunaliita changa wakati tuna miaka 49 sasa tangu uhuru.

    ReplyDelete
  8. TATIZO UMASKINI WATU WANAKOSA HATA AKILI KIDOGO ZA KUFIKIRIA HATARI

    ReplyDelete
  9. bongo magaidi hawahitaji mabomu, hii ni njia mbadala, tena unaangusha malori matano kwa wakati mmoja

    ReplyDelete
  10. mwenye kidumu ,mwenye kijiko akamimina.mwenye ndoo akachota ...

    ReplyDelete
  11. BWA SHEMEJI KWETU THITHI NI TAMBARARE TUMEENDELEA BWANA, EMBU HAPO BWA SHEMEJI KUNA TOFAUTI GANI NA MPITIMBI AU KIBAIGWA, NIKIMAANISHA UONEKANO WA WATU, TANZANIA NI MOJA SOTE TUKO SAWA KILA SEHEMU KUNA WA MATAWI YA JUU NA YA CHINI HATA LONDON WAPO WATU KAMA HAO

    ReplyDelete
  12. NJAAAAAAAA kweli mbaya !! Sasa awa wapuuuuzi wakiwaka moto je ?

    ReplyDelete
  13. daaah,kweli Mungu Mkubwa.sasa hao jamaa walivyotapakaa mafuta,hapo kama gari lingelipuka si wote wangeangamia?Mungu tu kaamua kuwanusuru lkn hali wala haikuwa shwari kivile.
    Umaskini wetu huu ................

    ReplyDelete
  14. bongo njaa kweli kweli,watu wamekuwa hawajali roho zao tena.

    ReplyDelete
  15. maisha magumu!!! wanasema unapotafuta maisha usiogope kufa, kufa ni ajali kazini!!!
    Kaka hapa nasikiliza kwanja rudeboy la rihana dah hili kwanja si mchezo!!!
    bwana dickson busagaga mambo vipi mkuu. vipi huko moshi mambo yakoje hapo?? mambo ya enh enh enh yakoje hapo wakichaga hao?? lete vitu bwana tutoke watu

    mdau wapajazzzz+titizzzz

    ReplyDelete
  16. yote hayo ni umasikni..mtu anawaz nyumbani mpaka giza linaingia hakijaeleweka anaona bora ajitoe muhanga akijua likitokea lolote atakimbia..jaman umasikin huu sijui watanzania tutaendelea lin

    ReplyDelete
  17. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.SIDUMU ITIKADI SAHIHI ZA CCM.CCM OYEEE!!

    ReplyDelete
  18. hivi watanzania wataelimika lini wanajigawia tu wese hivi ni kweli maisha magumu au kutokujijali maisha ni zaidi ya mnavyofikiri na ukikosa leo kesho utapata

    ReplyDelete
  19. Hata hifo derefa wa hako kahailux amechitahiti.

    ReplyDelete
  20. apa sina mbavu adi nimepaliwa na chai,,,hahahahahhaaa ndo mana naipenda hii blogu ata nikiamka vibaya nikisoma tu umu basi cheko

    ebu msomeni annon Feb 18,06:51:00pm

    kwi kwi

    ReplyDelete
  21. Wazungu wanasema "Unless you risk you can't harvest". Hawa jamaa wana-apply hiyo hapa.

    ReplyDelete
  22. ndugu zangu wabeba mafuta:ninaelewa sana hii hali ya maisha ndo ivo ilmradi kipatikane cha kula na kuendesha maisha kwa sasa!!poleni sana na iyo hatari

    watu hawaelewi hali ngumu ya watu bongo,nyie mshukuruni mungu wenu mna hali zuri unajua wala nini baadae,,,MSITUKANE WATU

    ReplyDelete
  23. Hizi hilux za sasa ni mabox.....acha hiyo. Angalia wachota mafuta hao. Lakini tutafika, baada ya kizazi hiki kuisha. Binadamu wa sasa na maisha ni vitu tofauti.

    Dunia itaumbwa upya na nchi itabadirika.

    ReplyDelete
  24. Mungu wasamehe hawa ndugu zangu wachaga kwa kuwa hawajui watendalo. Najua kwenu nyie hela haifananishwi na kitu chochote ndio maana hiyo ajali haikufananisha na ile iliyotokea Mbeya au Chalinze. Kilichokuwa kikiwazwa hapo ni hela tu.

    Ila mlianza kwa tahadhari kubwa!!! naona kama mlianza kusali kwanza wote kabla hamjaingia kuchota.

    ReplyDelete
  25. Serikali inapiga kelele tu ajali ajali ajali..Nae Rais anaagiza tu ajali zipunguzwe. Lakini hakuna hatua mahsusi zinazochukuliwa kushughulikia hilo.

    Tatizo kubwa ninaloliona Tanzania ni kutokuwepo kwa utaratibu wa kuhakikisha kosa linamilikiwa. "Own a Mistake". Mara hili litakapokuwepo basi inakuwa rahisi kuweka gharama ya umiliki huo.

    Hii ndio wenzetu wamefanya na ndio maana hapa UK ukimuazima mtu ghari atakuuliza unayo insurance? Na kichwani atajiuliza je huyu jamaa rekodi yake ya udereva ikoje? Na zaidi ya hapo ataweka rekodi ya muda alipokupa gari na muda umerudisha. Hivyo Ukifanya mafyongo yako huko yeye anatoa tu data zako kwa watu wa bima na Polisi. Kwa misingi hiyo utakuwa Zoba kumpa mtu usiyemjua na wala hujui address yake tena ni vizuri ukachukua kabisa namba ya leseni yake ya Gari. Sasa lile kosa ni lako na Bima wataliweka kwenye hesabu zako na utalilipia kwenye bima.
    Sasa hapo akili itakujia na Polisi pia wanakunyonga Leseni yako sasa adabu inaingia. Na kama kazi yako inabidi gari basi wewe adabu kweli kweli!!

    Hivyo hii si sayansi ya maroketi Serikali inabidi ikae na watu wa bima ili utaratibu huu uweze kufanyiwa kazi na kutekelezwa maana kadiri watakavyokubana mfukoni akili kichwani itafanya kazi maana upande wa Polisi kwetu bado maana kaufisadi.

    Sasa tusilie tu ajali tuchukue hatua ambazo wala hazihitaji kutumia nguvu ni akili tu kidogo.

    Sasa sisi Tanzania bado tunawekea bima gari badala ya dereva au Mmiliki. Sababu gari haligongi bali Dereva. Mfano ukipaki gari hapo nyumbani litamgonga nani?!! Na hata gari likiibiwa halipati hasara bali mmiliki ndio anaepata hasara. Ndio maana katika sheria ya bima husema kwa kimombo..."Insured Interest".
    Kwa kufanya hivi hata wamiliki wa magari watakuwa waangalifu katika kuajiri madereva maana akiajiri dereva ambaye rekodi yake mbovu bima yake itakuwa juu na kwa misingi hiyo madereva nao watakuwa waangalifu zaidi maana bima kwao itakuwa juu na kazi kupata itakuwa ngumu. Na pia hatathubutu kumpa dayworker!!!
    Vichwa ngumu watakuwepo kama ilivyo huku lakini watakuwa wachache na 40 yao huwa haiko mbali.

    Mimi hata sielewi kwa nini tunashindwa kufanya mambo ambayo ni madogo sana badala yake tunaanza kufikiria Maflyover wakati kadaraja tu tunaomba misaada...ajabu kabisa.
    Mzawa

    ReplyDelete
  26. mnawashangaa hao! wanamavazi bomba kabisa, nyie kweli mmekulia mbogo saba. Kuna vijiji huko sehemu hata kaputura hawana. Hawa wako fit kabisa basi tu njaa zao tu. Tz acha bwana

    ReplyDelete
  27. Better die trying than dying poor that i think is the mentor right there.but what a stupid decision is that watu kweli hawawezi kuona mifano mengine ya watu wengi walioteketea kwa kufanya issues za namna hio its a shame aibu kinoma kudadadadadeki

    ReplyDelete
  28. NIMEANGALIA MAONI KARIBU YOOTE YANAPONDA KITENDO CHA WATU KUCHOTA MAFUTA, LAKINI HII BLOG INGEKUWA INAFIKIWA NA MAJIDA WA MITAANI UNGEPATA PICHA HARISI KAMA KILE KITENDO NI CHA KISHENZI AU LAH. MIMI NIMEONANA NA KACHALA WANGU MAENEO YA KIBORORONI ANALIA NILIPOMUULIZA ANALIA NINI AKADAI YEYE AMEZALIWA NA MKOSI KWASABABU NEEMA IMETOKEA AKIWA YUPO MBALI ENEO LA TUKIO NA NI JANA YAKE TUU ALIKUWA MAENEYO YA AJARI NA WASHIKAJI ZAKE WANAMPIGIA WAKIWA WAMECHOTA MAFUTA NA KUYASUKUMA FAASTA SASA WANAZIGIDA BIA NA KITIMOTO KUTOKANA NA NEEMA ILE, MIMI MWENYEWE KULIKOSA LILE ZALI IMENIUMA NINA UHAKIKA NISINGEKOSA JAPO LITA25 KWA BEI YA FASTA NISINGEKOSA EF20. ALAFU MTU MWINGINE UMEKAA OFISINI UNAPIGWA NA KIPUPWE HUKU UKICHEKI NETI NA KUPONDA WATU WAKIFANYA KAZI ZAO AU KWASABABU WEWE KAZI ZAKO ZIPO KWENYE JOBUDISKRIPSHENI? SISI WENGINE TUKIAMKA ASUBUHI NA JOBUDISKRIPSHEN YETU INAANZA WAKATI WOWOTE KUTEGEMEA NA MATUKIO NA INABADILIKA KILA SAA, HIVYO SISI WENGINE HIYO NI KAZI KAMA KAZI ZINGINE NA TUNAIHESHIMU. MICHUZI ANGALIA NAMNA UNAVYOWEZA KUTUSAIDIA MAJIDA WA MTAANI NAMNA TUNAVYOWEZA KUTOA MAONI KWENYE MADA ZINAZOTUGUSA SISI MAJIDA.

    usipoweka hii komenti nitamaindi mbaya maana nimeingia intaneti cafe kwa buku langu la fegi ili kutafuta marafiki huko mamtoni ili kama vp ipo siko mzee huuuyo ma-Jobegi au ma Newyork tukapigane vikumbo na akina Jay zee

    ReplyDelete
  29. Jamani,ukiwa na njaa ,hauwezi kufikiri .....msifanye mchezo...kama mfukoni huna hata buku then unategemea nini ktk ishu kama hii?

    ReplyDelete
  30. hapo issue sio tu kiberiti au fegi..hapo nyanya za battery zikisuguana tu..stori inakuwa mpya..

    kweli its not easy ila tutafika tu

    ReplyDelete
  31. Wabongo wanafikiria moto kulipuka kapo ni mpaka kiberiti kiwashwe..mto hapa unaweza kulipuka from no where..

    ReplyDelete
  32. Umaskini au uchu jamani!!! Hivi hao wazoa mafuta hawaogopi kifo? Kibiriti, sigara, cheche inawasha hayo mafuta na tungesikia vilio kibao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...