wenye data tunaomba msaada tutani tafadhali...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. du!ninao wakumbuka ni marehem komredi Abdulrahman Babu,pia namona rais mstaafu Mzee Aboud Jumbe

    ReplyDelete
  2. Nimewatambua watatu tu hapo. Aboud Jumbe, Shanabi Mloo na Abdulrahaman Babu.

    ReplyDelete
  3. Mzanzibar_100%February 18, 2010

    Sisi sote tumegomboka, kwa ndugu...
    Kwandugu zetu walopotea, walooo..
    Walopigania nchi yetu,makusudi..
    Makusudi yakutugombowa, hatusaha..
    Hatusahau maisha yetu, kwa roho...
    Kwa roho zao zilopoteaaaaaaaaa!
    Hao ndio waalimu wetu, walio...
    waliokwisha kujitolea, nasisi...
    Nasisi hatutarudi nyuma, sote mbele...
    Sote mbele tutaendelea, kwaku lili..
    Kwakulilinda taifa letu, muhanga...
    Muhanga sote twajitoleaaaaaa!

    ReplyDelete
  4. WAPILI KUTOKA KULIA NI MAREHEMU ABRAHMAN BABU AMBAYE BAADAE ALIKUWA NCCR.

    ReplyDelete
  5. Wa pili kulia mwenye masharubu ni Marehemu Abdurrahman Babu na wanne kutoka kulia ni Mzee Aboud Jumbe Mwinyi

    ReplyDelete
  6. MOHAMED BABU, MAKAME, JUMBE, KOMBO
    NI TOKA KULIA KWENDA KUSHOTO WALIO KATIKATI WANAONEKA MWILI MZIMA

    ReplyDelete
  7. Wadau nimesoma tu wala sijawahi kuwaona kwa macho zaidi ya picha kwenye maofisi, dah, kwa mbali namuona Mzee Aboud Jube ooooh sorry sioni uzuri maana hili picha halina rangi na mmm sikuzoea hizi kwani mm ni mtoto wa tisini msaada jamani.........

    HYD

    ReplyDelete
  8. ninaowafahamu mimi wa pili kutoka kulia ni marahemu abrahman babu na wa nne mwenye miwani sheikh aboud jumbe mwinyi.

    ReplyDelete
  9. Kuanzia kulia kwenda kushoto wa kwanza ni baba yake nani hii, wa pili ni marehemu Abdulrahman Babu(Comrade) wa tatu ni Marehemu Sheikh Aboud Maalim na wa nne ni Sheikh Aboud Jumbe .
    mdau UK.

    ReplyDelete
  10. Kusema ukweli nimewafahamu watu wawili tu walovaa vimao nao ni Mzee Jumbe na Abdalhaman Babu wengine sipati picha.

    ReplyDelete
  11. Mkuu, Umenikumbusha mbali sana, enzi za uzalendo. kijana wa zamani.

    ReplyDelete
  12. alieva koti,kofia na shuka ni mzee Thabit kombo,then Aboud Jumbe

    ReplyDelete
  13. chama chetu cha mapinduzi chajenga nchiiiii
    chama chetu cha mapinduuuzi chajenga nchi
    nyerere aaah.. karume wanajenga nchi..

    ReplyDelete
  14. Anonym. wa 05:58 PM ahsante sana. nipo ughaibuni napiga BOX, huo wimbo umenikumbusha mbali sana ndg yangu. Enzi hizo nipo majeshi(JKT)mshapiga gwaride wakati mnatoka nje kabisa huo ndipo wimbo unapigwa, huku nyuma kabisa ya Kombania yupo kamanda anachagiza 'RINGA MPIGANAJI'. Dah, jamani naomba serikali ilirudishe jeshi.

    ReplyDelete
  15. Michu Thx kwa kumbukumbu kama hizi kwa kuchangia tu mwenye combat anaeimbisha ni Yusuf Himid na kutoka kulia kwenda kushoto wa pili ni marehemu Abdulrahman Babu wa tatu ni Marehemu Sheikh Aboud Maalim , wa nne ni Sheikh Aboud jumbe, wa tano ni Marehemu Mtoro Kingo Rehani na wa sita ni Marehemu Abdulhamid Twala.
    mdau Kizee cha long time .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...