Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Meli ya Mv Serengeti iliyokuwa ikifanya safari zake katika Bahari ya Hindi inawaka moto hivi sasa karibu na bandari ya Zanzibar ilipokuwa ikifanyiwa matengenezo madogo kabla ya kuondoka kuelekea Pemba.
Aidha Kikosi cha zima moto Zanzibar kimewasili eneo la tukio kikifanya juhudi za kuuzima moto huo kwa kutumia meli ingine.
Kwa habari zaidi na picha tuvute subra kidoogo.!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. tunashukuru Mungu watu ni wazima lakini kwa upande mwingine haya ma-vyombo ya usafiri ambayo ni machakavu bora yaungue yaishe walete mapya

    ReplyDelete
  2. Tafadhali tunaomba details zaidi kuhusu hii taarifa, je kuna recovery yoyote, kikosi chetu kimejitahidi kiasi gani? mali za wananchi zimesalimika? nani mmiliki wa meli kwa sasa na jee ina bima
    ni kwa vipi huduma za Unguja na Pemba zitaweza kutolewa bila ya usumbufu maana Serengeti ilikuwa ndio mkombozi wetu
    Mdau, ughaibuni

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza, nakubaliana na wewe kuwa hivyo vyombo ni vichakavu. Ila ukisema bora viungue kuna mambo mawili ya harakaharaka nayaona hapo:
    1. Katika hali iliopo sasa hivi watakaoteseka ni wananchi katika suala zima la usafiri maana mpaka waje wa-replace itachukua muda kwa nijuavyo serikali zetu huko bongoz.
    2. Hata wakinunua meli nyingine, mwendo ni ule ule, kwanza chajuu then hakuna kuzingatia ubora wa chombo, matokeo yake unapata chakavu tena, tena huenda zaidi ya hata iliyoungua.

    :Huo ndo utambarare wa bongo;

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...