Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Meli ya Mv Serengeti iliyokuwa ikifanya safari zake katika Bahari ya Hindi inawaka moto hivi sasa karibu na bandari ya Zanzibar ilipokuwa ikifanyiwa matengenezo madogo kabla ya kuondoka kuelekea Pemba.
Aidha Kikosi cha zima moto Zanzibar kimewasili eneo la tukio kikifanya juhudi za kuuzima moto huo kwa kutumia meli ingine.
Kwa habari zaidi na picha tuvute subra kidoogo.!


tunashukuru Mungu watu ni wazima lakini kwa upande mwingine haya ma-vyombo ya usafiri ambayo ni machakavu bora yaungue yaishe walete mapya
ReplyDeleteTafadhali tunaomba details zaidi kuhusu hii taarifa, je kuna recovery yoyote, kikosi chetu kimejitahidi kiasi gani? mali za wananchi zimesalimika? nani mmiliki wa meli kwa sasa na jee ina bima
ReplyDeleteni kwa vipi huduma za Unguja na Pemba zitaweza kutolewa bila ya usumbufu maana Serengeti ilikuwa ndio mkombozi wetu
Mdau, ughaibuni
Mdau wa kwanza, nakubaliana na wewe kuwa hivyo vyombo ni vichakavu. Ila ukisema bora viungue kuna mambo mawili ya harakaharaka nayaona hapo:
ReplyDelete1. Katika hali iliopo sasa hivi watakaoteseka ni wananchi katika suala zima la usafiri maana mpaka waje wa-replace itachukua muda kwa nijuavyo serikali zetu huko bongoz.
2. Hata wakinunua meli nyingine, mwendo ni ule ule, kwanza chajuu then hakuna kuzingatia ubora wa chombo, matokeo yake unapata chakavu tena, tena huenda zaidi ya hata iliyoungua.
:Huo ndo utambarare wa bongo;