JK akikata akizindua kitabu kinachohusu historia ya maisha ya utumishi serikalini ya Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kutoka kushoto waoshuhudia uzinduzi huo ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama(wapili kushoto), Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi(wanne kushoto) na watano kushoto ni Mwandishi wa kitabu hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Royalty Bwana Joseph kahama JK akiweka mezani tayari kwa mauzo kitabu kinachohusu maisha ya Mwanasiasa Mkongwe Sir.George Kahama muda mfupi baada ya kukizindua katika viwanja vya ikulu jijini Dar usiku wa kuamkia leo jioni. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir George Kahama(wapili kushoto) na wanne kushoto ni Joseph Kahama ambaye ni mwandishi wa kitabu hicho.Joseph ni Mtoto wa Mzee Kahama Joseph Kahama ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu historia ya Maisha ya Utumishi Serikalini ya Mwanasiasa Mkongwe Sir.George Kahama akimkabidhi Mama Maria Nyerere nakala ya kitabu hicho katika viwanja vya ikulu jijini Dar baada ya JK kuzindua kitabu hicho.
JK akiwa katika picha ya pamoja na Joseph Kahama(Wanne kushoto) ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu maisha ya mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika jijini Dar. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamim Mkapa, Sir Geroge Kahama(wapili kushoto) na kulia ni Rais Mstaafyu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. tanzania elites enjoying the show.

    ReplyDelete
  2. Michuzi tafadhali tufahamishane jinsi ya kupata kitabu hiki. Kwa sisi wadau tuliopo Ughaibuni. Shukrani

    ReplyDelete
  3. Kaka michuzi hiyo tittle ya Sir kwa Mzee Georgr Kahama ni ya utani sio kitu official na ilikua utani wa Mwalimu Nyerere kwa rafiki yake huyu,ukiitumia bila ishara ya inverted comas wananci wanaweza fikiria ni ya kweli,mtanzania pekee aliyetunukiwa hadhi hii ni Sir Andy Chande tu

    ReplyDelete
  4. Hongera Kahama kwa kutupa historia yako na ya nchi yetu ktk kitabu. Tunasubiri vya wengine

    ReplyDelete
  5. Hiyo historia iandike kila kitu kuhusu huyu "mheshimiwa".

    ReplyDelete
  6. Pamoja na matatizo mengi tuliyonayo it is encouraging to note that a new culture is emerging in our country. A progressive culture which appreciates education and documentation of our important milestones.

    diaspora meetings in the UK is one such good manifestations of a new praiseworthy trend.

    Once a culture for respect and honour for all our people becomes a cornerstone of our civilization, we will be well on our way to Glory as a People!!

    Pentecotal Preacher!

    ReplyDelete
  7. Tunaona mizungu ya mambo leo:

    1: Mwanao anawezaje kuwa biographer wako? Unapoandika historia ya maisha yako ni kama kuandika shajara. Kwenye shajara mwandishi huandika matukio ya kweli ya maisha yake. Kuna matukio ambayo huwezi kumwambia mwanao. Kwa mfano, Sijui utawezaje kumwambia mwanao kwamba "Mama yako alikuwa housegirl wangu halafu nikamuoa!" Au "Mimi nilikuwa informer au spy wa mataifa ya magharibi wakati wa siasa za vita baridi".. etc etc.

    2: Mzee Edwin Mtei naye ameandika autobiography yake akaizundulia Idara ya Maelezo. Vipi hii ya Mzee Kahama ikaenda kuzinduliwa Ikulu mbele ya Marais watatu?

    Anyway pengine miye ndiyo wa ajabu kuona haya kuwa maajabu.

    ReplyDelete
  8. HONGERENI FAMILIA YA KAHAMA, NYIE KILA WAKATI MPO JUU TU. ILA JOSEPH MFUNDISHE MKEO KUVAA BORA AJATOKEA HAPO NINA IMANI ALIVAA KITUKO. MBONA WE SMART KILA SIKU HALAFU MKEO ANAVAA KAMA HOUSE GIRL. NA ASHUKURU MUNGU NI MWEUPE VINGINEVYO SIJUI INGEKUWA VIPI NA KULE KUJIKODESHA SANA SIO SIFA, KUNA WEMBAMBA WA KIASI LAKINI WAKWAKE MBAYA, TENA SIKU UKIKUTA KAVAA SKETI YA KUMSHIKA BORA HATA YALE MAVITENGE YAKO. MWAMBIE UJUMBE UMETOKA KWA CLASS MATE WAKE WA ZANAKI. NANCY SIKU HIZI UMEACHA KURINGA NA DHARAU? BADIRIKA MATE

    ReplyDelete
  9. Good Joseph!
    It is encouraging to see some Tanzanians taking their time to write about the people who made it all happen...and Sir George Kahama is one of them.
    Who is next?

    ReplyDelete
  10. Eti wa nne kushoto! kwa nini tupotezeane taim kwa kuhesabu watu wote katika hiyo foto? si useme tu wa pili kulia? ndo mana bongo haitasimama kamwe. Unywanywa tu kila kona!

    ReplyDelete
  11. Kazi nzuri ya kuweka historia katika vitabu. Kama nilivyompa pongezi Mhe 6 hapo juu, nimefarijika na kufurahia sana suti ya JK - ni nzuri sana na ninajiuliza kwa nini huwa anang'ang'ania misuti ya tai! Jamani suti ya kiBongo ni nzuri na inatutambulisha kama waTZ ndani ya utandawazi. Haipunguzi kitu. Ubaya ni pale tunapovaa ngozi ya 'wenzetu' lakini tukafanya madudu yetu yale yale. Make it your trademark JK in your 2nd term!!!

    mtaalamu wa social skin

    ReplyDelete
  12. Michuzi tafadhali rekebisha title ya Sir George Kahama the only person alie tunukiwa hio heshima na Malkia Tanzania ni Sir Andy Chande. Sawasawa na kumvisha kilemba cha ukoka Charles Njonjo wa Kenya kumwita Sir Charles. Cheo hicho bwana Michuzi hakitoki kama maembe sokoni!!

    ReplyDelete
  13. KWANZA KABISA WATU WANAOSEMA KAHAMA HAKUPEWA HESHIMA YA SIR NA QUEEN, EBU JUNGUZENI ILIANZAJE HII SIR. UKWELI NI KWAMBA ALIPEWA NA QUEEN, NA KITU ALICHOPATIA HUO U-SIR NI KWAMBA ALIKUWA MTUMISHI SERIKALINI TOKA ENZI ZA WAKOLONI NA ALIKUWA KWENYE BUNGE LA WAKOLONI LA WAKATI HUO NA NI MTANZANIA ALIANZISHA MAMBO YA CO-OPERATIVE TANZANIA NA YAKAFANA SANA TANZANIA NZIMA BUKOBA IKIONGOZA NA KITENDO HICHO NDO ALICHOPEWA HUO U-SIR NA QUEEN, SO NI RASMI NA OFFICIAL FUATILIENI HILI NA MTALIONA, SIO OOOH NYERERE ALIKUWA ANAMTANIA!

    ReplyDelete
  14. Co-sign Mbagumbangu

    Cheo cha Sir mpaka malkia akupe sasa wenzetu lini walipata au sababu jina ni kubwa??? mmmh Sir Michuzi mbona hivi tena?

    ReplyDelete
  15. sir ze fulanazz ipitishweeeeeeeee

    ReplyDelete
  16. @ Tarehe Sat Mar 27, 03:13:00 PM, yani u so ignorant n comment is pathitic..kuna watu they have close relationship with there kids n who knows u better than ur family...yani wewe kwanza ur mfano tu shows how much shallow minded ur...


    ..well looking forward to readind the book

    ReplyDelete
  17. @ Tarehe Sun Mar 28, 12:11:00 AM, before u comment do ur research siyo mpaka malkia akupe http://en.wikipedia.org/wiki/Sir

    that link should help u

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...