JK, ambaye ni Mlezi wa Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT),akipiga picha kwa kutumia kamera ya mpiga picha wa Jamboleo Richard Mwaikenda, Ikulu Dar es Salaam jana baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwaapisha Makatibu Tawala wa mikoa minne pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere. Picha kwa hisani ya Mo Blog ambayo imerudi hewani baada ya kukosekana kwa siku mbili kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Safii! mpaka kwa mara ya kwanza leo nimeona bodigadi wa Rais katabasamu...nilidhani hawaruhusiwi kutabasamu.

    Mdaku

    ReplyDelete
  2. "THAT IS GOOD,VERY GOOD OUR DEAR PRISIDENT JK".PLS KEEP IT UP!

    ReplyDelete
  3. Katika gazeti la HabariLeo (3-11-2010) walitundika picha hii hii na hisani wakazisogeza kwa Mroki Mroki. Ni nani kati ya Mroki na Mo anastahiki kutambuliwa kuwa mwenye hakimiliki ya picha hii?

    ReplyDelete
  4. Ukiwa kwny vyeo vikubwa vikubwa sometimes unamiss kama vitu hivyo vya kupiga picha, au hata kujichanga kwny bar za uswahilini sehemu km manzese au kkoo kwny kuchagua vitu kama mitumba au vitu vinavyotembezwa na machinga. Sometimes mtu ukiwa raia wa kawaida halafu mshiko upo sio siri unaweza ku-enjoy na kuwa huru zaidi kwny kujichanga hata kwny miziki. JK Zoom kidogo.

    Mdau Chimbachimba

    ReplyDelete
  5. Du! Maro kibarua chako kiko matatani.
    Kumbe mzee anavipaji vingi?

    ReplyDelete
  6. DU Obama kamuiga Raisi Wetu Raisi wangu ni Black.

    ReplyDelete
  7. Jamani naomba kuuliza, hivi kwa nini wakati mtu unataka kupiga picha kwa camera kama hiyo ya Obama au JK unafumba jicho moja? na kwa nini style hii haitumiki mtu akitumia Digital Camera? naamanisha ukitumia digital camera hakuna haja ya kufumba jicho moja na cha ajabu zaidi hata mtoto hata bila kuambiwa afumbe jicho moja anafumba ili achukue taswiraz. Najua Ankal analo jibu ya kutosha maana ni Bobez katika anga za makonoz!

    Mdau wa Kudadavua!

    ReplyDelete
  8. Pat-MagazetiMarch 13, 2010

    Hongera-Kwani Patrick Tsere sasa Balozi

    ReplyDelete
  9. Mdau wa 02:17:00
    Inategemea digital camera gani unatumia..kama unatumia hizi camera za SLR...nyingi bado unatumia jicho moja kuangaali.Ila zile za wenzangu na mie za dola 100-150 bado hazina pakuchungilia.Hizi kamera pia zinategemaea na aina na mikogo mingi iliyopo.Hizo kamera walizoshika ndio za akina Michuzi,Maro,CNN na wengineo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...