
1955-2008
Leo Machi 24, 2010 ni miaka miwili kamili toka ulipotuaga, mpendwa wetu Suma. Tunakukumbuka na kukumiss sana.
Wewe ulikuwa mhimili wa maisha yetu na nguzo imara ya familia yetu, jamaa zetu na marafiki zetu.
Wewe ulikuwa mwangaza katika mihangaiko yetu. Ulikuwa nyota ya asubuhi katika maisha yetu. Wewe ulikuwa mshauri mwenye hekima kwa wote waliokusikia. Wewe mlezi maridhawa kwa wanao na sisi sote.
Wewe ulikuwa faraja na kitulizo kwa waliokuwa wakihangaika.
Wewe ulikuwa tabibu hodari kwa wenye maradhi, ukawatunza kwa upendo wagonjwa wa aina mbalimbali, ukawatia moyo waliozidiwa.
Ewe mkunga uliyehudhuria matukio mengi ya wageni kuingia duniani hapa, umo katika kumbukumbu zetu.
Unakumbukwa na familia huko Mbeya na Kiwira, kadhalika Mkongo-Namtumbo, bila kusahau Dar es Salaam na pande zote za Tanzania. Wapendwa wa Michigan na Marekani kwa jumla, na hata wale wa Yuropa wote wanakukumbuka sana.
Yote ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu.
Na ahimidiwe leo na milele kwa maana yeye alitupa wewe kama zawadi kwetu. Tumeifurahia dunia kwa sababu ya zawadi hiyo.
Tembelea ukurasa wa kumbukumbu
http://suma-ngonyani.virtual-memorials.com/
main.php?action=reflections&mem_id=16310
KYALA GWA MAKA!NDAGA SEMEKI!
ReplyDeletewith all due respect to the late Suma as my heart goes to the family and friends, is it me or just my english that tumekukumbuka is the same as tumekumiss?? mmmh.
ReplyDeleteREST IN PIECE MAMA!
ReplyDeleteMwenyezi akupokee kwenye makao yake ya milele, AMINA!
ReplyDelete