Vijana wawili wa Kitanzania David Mziray na Magongo,wasomao Mahajana First Grade College leo wamefanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana baada ya kupigwa na askari wa barabarani wakisaidiwa na wananchi,tukio zima lilianza leo asubuhi baada ya vijana hao kupata ajali ya pikipiki,wakiwa wao ndio wamegogwa na raia wa kihindi.
Askari wa barabarani ambaye hakuwa mbali na eneo la ajali alianza kuwatukana na kuwapiga vijana hao hivyo kusababisha na raia wengine wa kihindi kuanza kuwashambulia vijana hao na kudai lazima waondoke nchini kwao.
Baada ya kupigwa vijana hao walifikishwa kituo cha Polisi cha V.V Puram ambapo walianza kushambuliwa kwa maneno makali na ya kuwadhalilisha,wakapigwa picha kama wahalifu na pia kuandikiwa mashtaka yasiohusiana na ajali yaani wameandikiwa shitaka la kudhalilisha askari polisi(assaulting police officer) makosa ambayo hayana dhamana(non bailable offense) kwa sheria za India.
Hata hivyo kwa kushirikiana na vijana wenzao wakiongozwa na Rais Mstaafu wa FISAM Ndg.Abdu M. Mjaka na Mwenyekiti Mstaafu wa Tasam Idd Haruna Mituro,pamoja na Bahati Magoti walihakikisha haki inatendeka na bwana Abdu M. Mjaka alilifikisha swala lile moja kwa moja kwa Msaidizi Kamishna wa Polisi Mysore na hatimaye swala likafanyiwa kazi mara moja na Vijana hao kuachiwa huru na kufutiwa mashtaka yote pia kuombwa msamaha na mkuu wa kituo cha V.V Puram.
Muda umefika kwa Watanzania waliopo masomoni nchini India kupata ushirikiano wa kikamilifu kutoka ubalozi wetu uliopo Delhi,kusaidia kuwanusuru Watanzania kutoka kwenye vitendo vya kibaguzi na kudhalilishwa na wahindi.
Kuishi ktk nchi ya kigeni kuna shida zake pia, iwe india,Uingereza, South Africa na sehemu zingine.
ReplyDeleteMimi ni mkazi wa Uingereza, ukiwa na gari zuri hata makosa hujatenda, utasimamishwa na Polisi, maswali kibao kutaka kujua uhalali wa kulimiliki, wakisikia lafudhi ya kigeni saa hiyo hiyo wanawasiliana na idara ya uhamiaji wa Uingereza kujua uhalali wa ukaaji wako!
Ukiingia supermarket, walinzi macho juujuu kukufuatilia wanadhani utaiba vipande vya kuku aliyeganda barafu umtie ndani ya koti. Pia kudhihakiwa na raia wa kiingereza sio jambo la ajabu hasa hasa ukipita ktk maeneo ya 'manzese' ya London.
Kila unapotembea hatua 50 tayari ushapigwa picha na kamera kibao za serikali ktk majumba, barabara, vituo vya usafiri n.k
Ukienda kutibiwa mbali na kituo cha afya cha jirani na makazi yako unaulizwa pasipoti.
Hivyo ndugu zetu wa huko India mjifunze kuwa kuishi ktk nchi ngeni ni kazi, pia msitegemee sana kubishana na wenyeji wenu kuwa mtapata haki sawa, inabidi kutumia busara na uvumilivu na mbinu za medani, ili kujiepusha na yanayoweza kuepukika.
Mdau
Jijini London UK.
katika nchi zoote unaenda kusoma india.
ReplyDeleteBoycott INDIA, NENDENI KUSOMA NCHI ZINGINE, WAHINDI WALIPIGWA NA KUUWAWA AUSTRALIA MBONA WAO WALIGOMEA KWENDA KUSOMA HUKO, NASI PIA TUGOMEE KUSOMA INDIA, AU SWALA HILI LIFIKISHWE KWENYE SERIKALI YAO, PELEKENI BARUA KWA PRIME MINISTER WAO
ReplyDeletethat`s one side of the story, tusifanyane wajinga huwezi ukapata ajali halafu ukavamiwa na kuanza kupigwa tu, kwa kifupi masuala ya ubaguzi yako popote kule hata huko bongo tunabagua waarabu, wahindi na sasa tumewavamia wachina jifunze kuishi na watu wengine, dunia ya leo ya utandawazi msitemee kuishi peke yenu, huku marekani mambo hayo bado yapo pamoja nakuwa na raisi mweusi, ila watu wanajua kuvumiliana, ndio maana wamefanikiwa
ReplyDeletepoleni sana mnakwenda kwa wahindi au kwa waarabu huko hata wao wanakimbia wamejaa huko usa na ulaya
ReplyDeleteindia na china hata raia wake wanaona ni bora waje kuishi bongo msiende huko
ReplyDeleteAcheni kupeleka watoto huko.
ReplyDeleteMtalalamika hadi lini?
Tunausaidia uchumi wao kwa kuwasomesha watoto huko.
Pelekeni watoto wenu nchi nyingine
Marufuku mtoto wangu kusoma India
Bora abaki bongo
kijana katika maelezo yako hakuna pahala umesema kuwa uliripoti tatizo lako ubalozini.lakini unamalizia kwa kualumu ubalozi kuwa hauwasaidii. sijui unadhani ubalozi utajuaje kuwa hivi sasa kuna mtanzania pahala anapigwa na polisi?
ReplyDeleteacheni lawama za kitoto. ni lazima muujulishe ubalozi kwana kuwa kuna tukio limetokea kisha ndio muanze kualumu. mnadhani ubalozi unaendeshwa na malaika kila tukio linalomuhusu mtanzania watalijua bila ya nyinyi kuwajulusha.
pia muwe na tabia ya kujisajili ubalozini mnapokuwa katika nchi za kigeni. watanzania wewngi huona ubalozi kama kituo cha polisi kisha wanapopatwa na matatizo ndio huanza kulalamika. nendaubalozini ukajisajili ujulikane taarifazako na pahala ulipo hiyo itarahisisha kazi zao katika kukusaidia wakati wa shida. otherwise kila mtu anaweza kudai ni mtz na akaomba msaada wa ubalozi kumbe ni raia wa nchi jirani.
wewe anony wa Sat Mar 13, 04:57:00 AM, tafadhali usiongee kitu usichokijua..sisi tunaishi huku india..na siku zote siri ya mtungi anaeijua kata...hiyo ipo kweli ukigongwa wewe na muhindi utapigwa na mwizi na wanaweza kukuua hasa...isitoshe tunabaguliwa mpaka kwenye hio elimu..yani darasani unabaguliwa kama una maradhi ya kuambukiza loll...ukiangalia wewe unalipa pesa nyingi kuliko wao..ubaguzi umepitiliza huku...na sijui serikali yetu iko wapi.inashindwa kutusaidia...au mpaka tuchinjwe wote huku ndio watu watashtuka...hawa watu ni wana roho mbaya hatari..
ReplyDeleteWazazi mnaopenda kusomesha watoto wenu nje ya Tanzania nawashauri muwapeleke Marekani au canada.UK ni pazuri lakini tatizo pamejaa sana.Wenye nchi wameanza kuja juu,usumbufu umekuwa mwingi.Ninawashauri hivyo baada ya kukutana na wanafunzi mbalimbali wanaishi marekani ambao pia waliishi nchi nyingine kabla ya kuingia marekani au Canada.msidanganywe kama mtoto akisoma Marekani atakuwa muhuni,ni jinsi mzazi ulimlea mwanao.Kama hukumfunza adabu hata ukimpeleka Mecca au Vatican atachemsha.Si kila anyesoma Marekani anasuka nywele na kuvaa heleni(kwa wavulana).Mwanao akienda India akarudi salama mshukuru Mungu.Hapafai,wazazi naomba mnielewe.
ReplyDeletePoleni vijana wa Mysore.Tatizo la askari wa kihindi ni rushwa na wanaamini watu wageni wote wana pesa ndo maana waaliandika haraka haraka hiyo hati ya mashtaka.
ReplyDeleteJitahidini kuvumilia tu maana hamko nyumbani kweni ingawa hata tanzania siku hizi polisi wanaua raia bila hatia bora ya njie mlipigwa tu.
ila kuweni makini pia na pikipiki (BIKE)zenu maana India hiyo misogamano.
Poleni sana.
Walichokiongea anon 01:19, anon 04:57 na anon 08:02 ni mambo ya msingi sana kuhusiana na sakata hili.
ReplyDeleteKitu ambacho vijana wetu inabidi wajifunze ni uvumilivu. Maisha nje ya bongo ni tofauti sana na wasitegemee kupata mtelemko muda wote.
Matukio kama haya mtaendelea kukumbana nayo mpaka mnamaliza kozi zetu. Weka msisitizo kwenye kitu ulichoenda kufuata huko. Fanya kila utakaloweza kuepuka matatizo yanayokwepeka.
Mdau ulieandika hivyo hujui mambo yanayoendelea India.. ubalozi umeshataarifiwa mambo mengi yawapatayo watanzania Mysore na India kwa ujumla na hakuna lipatikanalo kama "nyinyi wakorofi" je tatizo lilitokea mwenzi mmoja uliopita mjini Bangalore mtanzania kuuliwa kikatili kwa kukatwa kichwa baaado halivuti taaswira ya kuwa maisha ya watanzania yapo hatarini India? juzi tu watanzania wakiwa katika mazoezi ya Bangalore University International students day katika nyumba ya mmoja wa wanafunzi hao walimwagia petrol na kuwashwa moto na ubalozi taarifa wanazo jee bado haivuti taaswira? Vijana waliopigwa jana for no reasons askari aliwatukana pia kuwaambia hamna haki katika nchi hii na alidiriki hata kumpiga helment la kicha kati ya vijana hao..
ReplyDeletehebu angalia ni ukorofi gani unaodaiwa wanafunzi tuliopo India ni wakorofi? kuja kusoma India au?
Tatizo ni kwamba sio kujitambulisha ubalozini kwani elewa ubalozi upo New Delhi wanafunzi wapo katika miji mbalimbali si rahisi ufikiriavyo kwenda ubalozini.. ila taarifa zote za watanzania na majina yao ubalozi unafikishiwa na uongozi ta jumuia za watanzania katika miji mbalimbali.. ila uwajibikaji wa ubalozi wetu katika maswala ya wanafunzi ni ziro kabisa.
Ila tunaomba watuelewe tunaendelea kufa..
Hivi mbona sasa tumechoka kunyayaswa?utumwa ulikuwa wetu,na hawa watu weupe ndio walitufanya watumwa,tukateswa sana,kwa nini tusivunje uhusiano na hawa wahindi au mturuhusu tuwamalize sisi wenyewe kwa mikono yetu,au wao ni wa thamani sana,au wanatupa nini zaidi ya kujaza Nchi yetu,na kwa nini viongozi wetu wasilifuatilie hilo?na huyo balozi wetu anafanya nini huko afuatilii watoto wake kwani hata kama umri wake ni mdogo ni baba yao tu,sasa tunamuomba ahakikishe anafuatilia haya mambo tumechoka kudhalilishwa,tumefanywa kama wanyama.mimi kama mimi nitawaombea.lakini pia mtupe hatma ya hawa vijana wetu wanaouwawa wanaonyanyaswa huko india,la sivyo tutaanzana nao na sisi
ReplyDeleteNa sisi tukianza kuwachapa hawa wahindi hapa itakuaje?
ReplyDeleteNchi ya watu shida sana. Unamwona yule mtu alituomyesha Michuzi jana akikandamizwa na gari sijui ni muhindi aliona kuendelea na hoja itakua sooo labda vibali vyake vya kuishi nchini vimeisha akajiondokea polepole
ReplyDeleteHebu acheni kwenda kusoma India. Tatizo la watanzania ukisikia kusoma nje ya nchi mnafikiri kila mahali ni pa kwenda. Halafu vijana wa kitanzania mnatakiwa muwe wavumilivu na watulivu mnapokuwa nchi za watu. Sio mkifika huko muishi kama mpo kwenu, watawamaliza wote, shauri yenu. Mtaishia kulalamika na hakuna anayewasikiliza.
ReplyDeletemnachomewa nyumba mkiwa ndani, kupigwa na hata kuuawa. pia mnasema hata hiyo elimu mliyoifuata mnabaguliwa madarasani. sasa nini kinachowaweka huko? au ni ile hali ya kujisika raha uko nje ya nchi? kuna ugumu gani kurudi kwenu au mmeua?
ReplyDeletemimi sijui sisi watanzania na waafrika kwa ujumla tuna tatizo gani? upungufu wa akili? wema uliopita kiasi? hawa wahindi tunadiriki hata kuwapa ubunge na nyadhifa kubwa hapa kwetu, hao waarabu ndio usiseme maduka yao kila kona, watu hao hao ndio wanaotubagua na kutunyanyasa nchini kwao tunakaa kimya tu? hivi mnafikiri idd amin dada wa uganda alikuwa kichaa kuwafukuza wahindi uganda? na hao waarabu wanajifanya kurainisha mioyo ya waafrika kwa kutumia dini kumbe ni waovu kwao, wanaonea raia wetu kwao..kuna siku kitawaka tu hapo tz kwa hao wahindi na waarabu..you can fool people some time but cant fool people all the time..mungu ibariki tanzania na afrika..mimi sina udini wala ukabila ila ni mzalendo..
ReplyDeletetutawafukuza hao wahindi na waarabu kama alivyofanya idd amin dada kule uganda..ni washenzi tu tunawapa hapa nyadhifa serikarini kama ubunge, maduka yao kila kona harafu wanatufanya mazoba...kitawaka tu siku moja hapo tz wala si muda mrefu..huu ni ujinga na huruma iliopita kiasi ya sisi waafrika...
ReplyDeletejamani unyanyasi uko kila sehemu..kwa mfano huku russia watu wanapigwa hadi wanauwawa,taarifa za vifo zinazotolewa hazina maana..who cares?tena hamna hata ubalozi unaojitolea kuuliza,balozi ziko nchi za watu kutetea haki za wananchi wao,lakini wafanyakazi wamekua waoga na kulinda nafasi zao za kazi bila kujali maslahoi ya wananchi wao.waafrica tutabaki watumwa ndani na nje ya nchi zetu.coz hatuwezi kujitetea.
ReplyDeletewahindi na waarabu hawafai, na sisi tutaanza kuwafukuza bongo si muda mrefu. tutafanya kama idd amini alivyofanya uganda, tena bado kidogo cha moto watakiona. suala la kuwa wanajiita wasukuma wa igunga hatutaki.
ReplyDeleteINAWEZEKANA MTU AKABISHA KWA KUWA AJAFIKA AU KUKAA INDIA,TATIZO LILILOPO INDIA NI NJAA WANANCHI WA INDIA WANAMAISHA MAGUMU SIJAWAHI KUONA DUNIANI WANAPOMUONA MGENI NA HASA MWAFRIKA WANAKUWA NA HASIRA NAE WANAJUA KAJA KUBANANA NAO KIMAISHA,PENGIE ASKARI WALA HAKUJUA KAMA KUNA WAFRIKA WAKO HAPO KIMASOMO,MZUNGU KWAO NI NUSU MUNGU KWA VILE WANAAMINI WANAPESA,NENDA MUMBAI LEOPORD CAFEE KAKAE NA MZUNGU MEZA MOJA WAITER ATAKUJA KUKUOMBA UHAME MEZA JAPO UNA PESA YAKO.WEWE ULIONA WAPI MZAZI KUZAA MTOTO KILEMA ANAFURAHIA KWA SHANGWE ATAPUNGUZA UMASKINI KWA KUMGEUZA MRADI WA KUMLAZA JUWANI BARABARANI AOMBE WAPITA NJIA.NJAA,SHIDA NA UFAHAMU MDOGO NDIO KUMEPELEKA KUTOKEA TUKIO ZIMA POLENI VIJANA,SISI TUNA IJUA INDIA TUNAWAASA MUWE MAKINI NA MZINGATIE MLICHO FUATA(ELIMU) KWANI NCHI MLIOKUWA HAINA MPANGO.
ReplyDeleteoya mwana poleni sana wa hindi mimi nawajua fika nilikuwa uko!!yalinishinda nika kimbia!!! sasa tatizo lenu kwa nini mnangangania uko india kwani mnasoma bure? chukua transfer urudi bongo ukamalizie shule yako hila msilogwe kuamia nchi nyingine ya ASIA kote ni moto huo huo hata malaysia.yani ni bora ukasome vyuo vya africa au ulaya jamani SOUTH AFRICA MBONA KUNA VYUO POA SANA!!!AU NA UKO UBAGUZI !!ACHENI KUNGANHANIA NCHI ZA WATU JAMAA AWAWATAKI RUDINI KWENU!! KWANI LAZIMA USOME HINDIA??
ReplyDeleteIndia, Na wahindi, ndio maana wapakistani wanawaingilia mpaka mjini mwao na kuwapa kipigo.
ReplyDeleteUnafikiria watu wenye kuabudu ng'ombe watakuwa na akiri? Na mimi sioni hiyo elimu yao wanayowanyanyasa vijana wetu!
Jamani pelekeni vijana wetu katika vio vyetu vya ndani. Watapata elimu nzuri tu, na pesa kubaki hapo hapo tz au katika nchi nyingine za kiafrika.
Baniani wameshaanza kuona utamu wa kuuwa waafrika hawataacha mpaka serikali yao iingilie kikweli kusimamisha ujinga huu na kuwaelimisha au sisi kutokwenda huko. Kwani wanaona sisi tumefulia sana hawajali hata kama mnatumia fedha zenu kuwatajirisha, inaumaa sana.
Serikali, maliza chuo cha dodoma ili vijana wengi wabaki hapo.
wewe kaka waındı sıo watu weupe sawa hao nı jamıı ya watu weusı 2,dunıanı kuna aına 3 za watu,wupe,njano na weusi
ReplyDeleteNILIWAHI KUULIZA KWA NINI WATU WAACHE KENDA USA KWENYE ELIMU BORA WANAENDA INDIA NIKASHAMBULIWA KWELI.
ReplyDeleteHAO WAHINDI WAKIMBILIA USA HAWATAKI KWAO NYIE NDO MWAPAONA BORA.
nadhani pia hata vijana wanaweza kuwa wana makosa ya kibongo kujidai wababe nchi ya watu, kwani wabongo si mnawajuwa eti 'usitubabaishe we ponjoli/gabacholi"
HAHAHA nacheka kwa uchungu kabisa, kweli jamani nchi zote wageni wanapata taabu ila sisi wa India ni too much tena nasema too much coz i have experience na nchi nyengine, wadau siri ya mtu aijuae kata. Wanafunzi wa India tuna taabu, nilipo ingia tu nimetukanwa ila nilikua najua nikavumilia, leo nasoma habari hii nakumbuka nimetukanwa Charminar Hyderabad India. India hatokuja mdogo wangu wala mwanangu na nimeshauri wengi wasije hku. huku si kwa kukaa wageni haswa sisi weusi.
ReplyDeleteWadau zingatieni haya sisi ndio tunaoishi hapa.
Nyinyi nyote hamna point, hao wanaoenda kusoma huko India, UK, na kokote kule nje ya TZ mkae mkijua Maji ukishayavulia Shart...... Uyaoge... Sawa.. hapo tupo pamoja, USHAURI WA BURE LETENI HAO WAALIMU WA KIHINDI, NA WENGINEO, WAJE WAWAFUNDISHIE HAPA HAPA TZ, maana mnaona huku hamna elimu sasa mnakwenda nje mnaanza kupata matatizo hiyo ndo solution pekee, hamtaki MJIJU!!! kudadadeki..
ReplyDeleteKuna ushauri mzuri sana ktk post nyingi hapo juu. Siri ya kuishi nchi za watu ni kuwa mpole. Usitambe kama unavyokuwa kwenye nchi yako. Kwanza wewe ni student nchi ya watu pikipiki ya nini? Panda public transport - inatosha. usingekuwa na pikipiki yasingetokea hayo. Kuna nchi ukisababisha ajali gharama yake ni kubwa. Hakuna kumalizana barabarani au kukimbia ajali kama Bongo, ati. Punguza vitu vinavyoweza kukutia matatani. Usiende kwenye madisco. Usicheze na wasichana wao. Waogope. Rudi nyumbani mapema. Tumia muda wako nyumbani, library, darasani... Kama kweli mtu atakufuata nyumbani kwako au darasani au library akakutukana, basi hapo sasa hapafai. Mimi niko ughaibuni pia na ndio mkakati wangu wa maisha huku. Wanigeria hapa wananiita anti-social lkn najua ninachofanya. Nina moja kichwani.
ReplyDeleteMdau wa ughaibuni pia.
Thomas...Tomas.....Tom. Cool down, acha jazba. Hakuna haja yoyote ya kuuwa mtu wowote hapa Bongo. Sisi sio washenzi, kama wanafuata sheria zetu waache waishi salama kama raia wengine wa nchi.
ReplyDeleteHakuna kumbagua mtu kama muhindi au mwarabu wakati akiwa raia mwema, na vilevile acha kuzungumza zungumza kuhusu udini udini utaonekana unachuki zako za kibinafsi za udini.
Mwalimu Nyerere alikemea suala la la kubagua kwa aina yoyote kwani "dhambi yake inakuwa aishi, mtaendelea kubaguana mpaka mtu wa mwisho."
Hili la wahindi huko India ni umasikini wa wahindi ndio chimbuko la chuki hizo, nawaomba vijana wawe makini, wafuate kilichowapeleka waache kutanua wakati wenyeji wako hoi, chuki zao zitazidi. Wahindi wengi huko wengekuwa na hali nzuri wasingekuwa na muda na wanafunzi maskini wa kiafrika. Jiulize kwanini hayo hayo hayatokei kwa wanafunzi walioko, amerika, ulaya, japan, australia, canada, uturuki na kwingineko ambako wananchi wengi wa kawaida wako vizuri kuliko wanafunzi wageni kiuchumi.
Vijana poleni lakini pigeni shule, acheni show off, tumieni muda mwingi katika mazingira ya shule/elimu, acheni kutaka kuchanganyika na hao wananchi.
Good luck.
JAMANI TUSIPITE PEMBENI KUHUSUA SWALA HILI LA WAHINDI, KIUJUMLA HATA HAPA KWETU TANZANIA WANTUBAGUA SANA. NA NDO MAANA HATA WANAOFANYA KAZI KWENYE MAKAMPUNI YAO WANAPATA SHIDA SANA. MISHAHARA KIDOGO SANA, KAZI ZA KIBANO, KUTISHIWA KUFUKUZWA KAZI, NA MENGINE MENGI SANA. WATANZANIA TUSIPOKUA MAKINI TUTAKUA MASKINI MILELE. TUAMKE TUIPIGANIE NCHI YETU TUUKOMBOE UZALENDO WETU. NCHI YETU INA MALI NYINGI SANA. VIONGOZI WETU WAMETEKWA AKILI NA WAGENI. HILI JAMBO NI CHANZO CHA UKOLONI TANZANIA.
ReplyDelete