SIKU ZA MKUTANO WA PILI WA DIASPORA ULIOPANGWA KUFANYINKA JIJINI LONDON, UINGEREZA, ZINAKARIBIA NA UBALOZI UNASHUKURU KWA MUITIKIO WA WADAU AMBAO WENGI WAMEJIANDIKISHA NA KUAHIDI KUHUDHURIA. KWA WALE AMBAO BADO KUJIANDIKISHA WASICHELEWE SANA MAANA SIKU NDIYO ZINAYOYOMA. NENDA
KWA MAELEZO NA MAELEKEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi,
    Hizi diaspora event nio nzuri kabisa na ndizo zinazotakiwa kuwa kazi za kila siku za maofisa na Ofisi zetu huko nje ya nchi. tatizo langu bado ni moja na nadhani nitapatiwa majibu au maoni ya wananchi. Je balozi zetu zina mwongozo wowote wa namna ya kuratibu mambo haya. Au ni kila ubalozi unaratibu kivyake vyake bila mfumo maalum.nchi nyingi zina taratibu au mifumo maalum ya kutaribu mambo haya. Hata nyumbani tayari taasisi binafsi zimeshaweka mazingira fulani ya kuwahusisha hawa diaspora katika shughuli za nyumbani ..tatizo ni kuwa serikali haijawa na mfumo maalum wa kuratibu shughuli hizi katika sehemu mbali mbali duniani kote.Itakuwa ni jambo la busara wananchi kulelezwa jambo hili limefika wapi na si mambo kufanyika vipande vipande. hapa London wanaoneka wameshafika hatua moja mbele katika jambo hili...vipi huko mashariki ya mbali, urusi, korea, uchina, afrika ya kusioni, marekani, hata hapa kwa majirani zetu kenya na uganda...anything formal underway...
    Asante

    ReplyDelete
  2. NIMEFIKA NYUMBANI KWA MARA YA PILI MWAKA JANA, BAADA YA MIAKA KUMI NJE YA NCHI.
    NIMEMSHUKURU SANA MUNGU KWAMBA PAMOJA NA MATATIZO KIBAO YANAYOIKABILI TANZANIA YETU, KUNA NURU INAYONG'ARA NA KULETA MATUMAINI.
    FIKRA YA KUTUKUTANISHA DIASPORA NAIPA HONGERA ZOTE, NILIHUDHURIA KONGAMANO LA KWANZA HAPO 2008, NA HAPANA SHAKA LILITUPA MOYO SANA SISI TULIO NJE YA NYUMBANI.
    ASILIMIA KUBWA SANA YA TULIO MBALI MACHO YETU YANATAZAMA NYUMBANI, NA NDILO LENGO HASA LA KUWEPO HUKU.
    MZEE WANGU ALIONDOKA MCHUKWI RUFIJI AKATOROKEA KUNDUCHI KUVUNJA MAWE, NA HATIMAYE KUWEKA KITUO CHA MAISHA YAKE DAR ES SALAAM. MABADILIKO YA WAKATI, LAKINI AZMA NI ZILE ZILE, KUWA KIZAZI KIJACHO KIWE BORA YA KILICHOPITA. KWA SABABU HIYO NDOO NA SISI TUMELOWEA HUKU UK. JAMAA ZANGU WENGINE NILIOKUWA NAO DARASANI KULE TANDIKA, ZANZIBAR NA PIA BUJUMBURA, WENGINE NI MAWAZIRI, WENGINE MAGAVANA NA WENGINE NI WABUNGE.
    PROFESHENI TOFAUTI LAKINI LENGO MOJA, NALO NI KUJIKWAMUA.
    SOTE TUNA MCHANGO MUHIMU KATIKA KUSUKUMA MBELE GURUDUMU LA MAENDELEO YA NCHI YETU.
    NAJUA KUNA WENGI WANATURUSHIA VIDONGO DIASPORA, NA HAWATAKI KUONA TUKITHAMINIWA-WANADHANI SISI NI WASALITI-LAKINI HAYO NI MATOKEO LABDA YA KUTOKUELEWA VIZURI BAADHI YA KWELI ZA KIMAISHA. LABDA PIA NI SABABU YA CHOYO NA WIVU.
    NATAMANI WATU HAO NAO WANGEKUWA HUKU TULIPO SISI, WAKAPATWA NA HISIA TULIZONAZO. LABDA WANGEJITAMBUA.
    KWA MFANO SUALA LA URAIA WA MATAIFA MAWILI JAMAA WENGINE HAWATAKI KABISA KULISIKIA, UTADHANI NI UHALIFU. NI SABABU YA CHOYO TU NA KUTOKUWA NA ITBARI. FAIDA ZAKE KWA NCHI CHANGA KAMA TZ NI NYINGI ZAIDI YA HASARA ZAKE. LAKINI SI WENGI WENYE KULIONA HILO.
    AHSANTE SERIKALI YETU KWA KUTUPA FURSA INGINE YA KIKAO CHA DIASPORA-TUTAJITOKEZA KWA WINGI INSHAALLAH
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  3. Hima Watanzania jiandikisheni na mhudhurie hilo Kongamano hapo London.

    Acheni kulaza damu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...