Lengo la taratibu hizi, ni kuwataarifu Watanzania waishio Uingereza na Jamhuri ya Ireland kuhusu mwelekeo mpya ya Jumuiya ya Watanzania na kilichofanyika hadi sasa, pia kuwataarifu kuwa tarehe 26 & 27 Machi 2010 kutakuwa na mkutano wa Diaspora ya Uingereza na Jamhuri ya Ireland, ambapo katika siku ya pili, sehemu ya mkutano huo utatumika kama Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza na Jamhuri ya Ireland. Katika sehemu hiyo ya mkutano, pamoja na mambo mengine, utachagua Viongozi Wakuu (wa kitaifa) wa Jumuiya ya Watanzania kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.
UTANGULIZI
Jumuiya iliyopo ya Watanzania (TA-UK) ilianzisha mchakato wa kutaka Jumuiya mbali mbali za Watanzania zilizopo nchini Uingereza na Jamhuri ya Ireland, zifanye kazi kwa pamoja. Kufikia hatua kama hiyo, viongozi wa Jumuiya mbali mbali waliopo hapa Uingereza waliitwa na uongozi wa TA kwa lengo la kujadiliana ni namna gani Watanzania washirikiane kikamilifu katika hii Jumuiya yao.

Hatua hiyo ililenga zaidi katika kuwa na Jumuiya yenye uwakilishi mpana zaidi wa Watanzania waishio pote Uingereza na Ireland, kwani siku zote “umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”. Baada ya vikao na mikutano mbali mbali ilikubalika kuwa iundwe Kamati ya kuratibu muundo mpya wa hii Jumuiya ya Watanzania.
Kamati hiyo iliundwa na ilitokana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hizo mbali mbali zilizopo Uingereza. Baada ya kazi nzuri ya Kamati hiyo kukamilika na kuikabidhi kwa Uongozi wa TA, mambo yafuatayo yameonekana kuwa ni muhimu kuyatekeleza ili kuwa na Umoja wa kweli wa Watanzania waishio Uingereza na Jamhuri ya Ireland.
MUUNDO MPYA WA JUMUIYA YA WATANZANIA
Kamati ilipendekeza,vipengele mbali mbali vya Katiba iliyopo ya Jumuiya ya Watanzania, vifanyiwe marekebisho kwa lengo la kuwezesha Watanzania kwa hiari yao, kuunda Umoja wao wenye nguvu. Kufanikisha hilo ilikubalika kuwa Muundo wa Jumuiya ya Watanzania uliopo uboreshwe kama ifuatavyo:-
Kwa hatua za kuanzia, imependekezwa kuanza na Jumuiya za Watanzania zilizopo katika Mikoa/Majimbo/Miji (Chapters) 14 yafuatayo:- Scotland, Wales, Republic of Ireland, London, Great Manchester, Coventry, Birmingham, Reading, Slough, Southampton, Northampton, Cardiff, Leicester, Milton Keynes.
Kila Mkoa utakuwa na uongozi wa mkoa, utakaochaguliwa kwa kushirikisha uongozi wa, pamoja na, Jumuiya ndogo ndogo kama zilivyokwisha jitokeza au kama zitakavyoanzishwa kutokana na mafanikio ya kuwahamasisha Watanzania katika kushirikiana ki-Jumuiya. Kila Mkoa wa Jumuiya utakuwa huru kuendesha kipekee shughuli za ki-Jumuiya Mkoani mwao, alimradi tu shughuli hizo hazikiuki Katiba ya Jumuiya.
Katika siku za usoni, uongozi wa Jumuiya utaweza kubadilisha, kwa makubaliano, mgawanyiko wa Mkoa/Jimbo/Miji, iwapo patakuwa na ulazima kwa ajili ya upanuzi wa Jumuiya ndogo ndogo.
UCHAGUZI
Jumuiya zote za Kitanzania zilizomo katika Mkoa/Jimbo/Miji zitatakiwa kukutana na kufanya uchaguzi za kuchaguwa wagombe watatu (03) wenye uwezo na ari ya kuwatumikia Watanzania, ambao watawakilisha Mkoa huo katika kugombea nafasi za Kamati ya Kitaifa ya Utawala ya Jumuiya ya Watanzania (TA-UK).
Majina ya Wawakilishi wa Mkoa yatapaswa kuwasilishwa katika Kamati ya Uchaguzi si chini ya siku tano (5) kabla ya Uchaguzi Mkuu. Wagombea hawatopokelewa baada ya hapo. Kila Mkoa utakuwa na kura tano (05) yaani wagombe 3 pamoja na wawakilishi 2 wa kuchagua viongozi wa Kamati ya ya Kitaifa ya Utawala ya TA-UK Inasisitizwa kuwa watakaochaguliwa kupiga kura kwa niaba ya Mikoa/Majimbo/Miji ni lazima wawepo siku ya Uchaguzi. Uchaguzi wa wawakilishi kutoka katika kila Mkoa/Majimbo/Miji utatakiwa ufanyike mapema kuzingatia kipindi husika cha kuwakilisha majina kwenye Kamati ya Uchaguzi – kama ilivyotamkwa hapo juu.
Tafadhali izingatiwe kuwa si kila Mtanzania atakayehudhuria ataweza kushiriki katika kupiga kura katika Uchaguzi huo Mkuu, bali watakaopiga kura ni wale tu waliopewa dhamana ya kuchagua na Mkoa (mji) wao.
Inatazamiwa kuwa kila Mtanzania atajiunga na “tawi” la Jumuiya lililopo karibu naye, katika mkoa wake /jimbo lake/miji wake, ili aweze kutumia nafasi yake kikamilifu katika Kuchagua viongozi na/au kugombea nafasi ya uongozi wa Jumuiya katika hilo eneo lake nakuweza kushiriki kikamilifu katika kuchangia maendeleo ya jumuiya yake hapo alipo.
Kwa hatua za awali, iwapo kutakuwa na Jimbo/Mkoa/Mji ambao utakuwa bado haujahamasisha Watanzania kikamilifu, na kwa hiyo kijikuta kuwa kuna Watanzania wachache waliojiunga, wataombwa wajiunge na Jimbo/Mkoa/Mji wa karibu wenye Jumuiya ili waweze kuwa ni sehemu ya Kushiriki katika harakati za kuchagua Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania (TA-UK) na pia kuchangia maendeleo.
Uchaguzi kama ulivyotajwa hapo juu, utachagua Wajumbe kumi na wawili (12) miongoni mwa wawakilishi waliochaguliwa na Jimbo/Mkoa/Mji. Hawa 12 ndio watakaokuwa wana-Kamati wa Kitaifa.
Hii Kamati ya Kitaifa ya Utawala itakaa katika kikao chao cha kwanza mara baada ya uchaguzi na kuchaguana ili kujaza nafasi za Uongozi wa Kitaifa wa TA-UK yaani Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Mwenezi, Mweka Hazina na wajumbe saba waliobaki watakamilisha idadi ya Kamati Inasisitizwa kuwa kuwe na angalau Wajumbe 2 wanawake.
Mkutano Mkuu wa Machi 2010 utaombwa upitishe Katiba mpya na halafu kufanya uchaguzi wa watu 12 kati ya wawakilishi, watakaounda Kamati ya Kitaifa ya Utawala.
NAMNA YA KUPIGA KURA
Uchaguzi wa Viongozi utazingatia taratibu na sifa za uongozi kama zilivyofafanuliwa katika utaratibu wa uchaguzi wa Katiba ya Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza na Jamhuri ya Ireland.

Majina ya wagombea wote wenye sifa zilizotakiwa yatapigiwa kura za siri na Watanzania wanaohusika na kupiga kura, mshindi atapatikana kwa wingi wa kura (Simple Majority). Ikiwa katika uchaguzi kura za wagombea zitalingana, Kamati ya Uchaguzi itakuwa na kura moja ya Turufu ambayo itaamua mshindi au Kamati ya Uchaguzi inaweza kuamua uchaguzi urudiwe kwa waliolingana kura.
Kila mpiga kura atachagua wajumbe 12 kati ya wagombea waliojitokeza kupigiwa kura. Baada ya washindi kupatikana, watatangazwa kuwa wana-Kamati ya Kitaifa ya Utawala wapya wa Jumuiya ya Watanzania na kutambulishwa rasmi kwa Mkutano Mkuu. Kisha wana-Kamati watajitenga kwa kikao chao cha kwanza cha kuchagua Uongozi wa Kitaifa wa TA-UK.Wakikamilisha, viongozi hawa wapya nao watatambulishwa kwa Mkutano Mkuu.
MATAYARISHO KABLA YA UCHAGUZI
Ili kuwapa fursa wote watakaopiga kura, ili waweze kupiga kura ya ufahamu, inabidi wale wote watakaowania nafasi za uongozi, wawakalishe taarifa fupi ya kujieleza sifa na kuwashawishi wajumbe wawapigie kura. Taarifa hiyo itatakiwa iwakilishwe, kwenye Kamati ya Uchaguzi, wakati mmoja na uwakilishaji wa majina ya wawakilishi watano (5)wa Jimbo Mkoa/Mji , si chini ya siku 5 kabla ya Mkutano Mkuu.
Nafasi zitakazopigiwa kura ni:
Watu 12 wa Kamati ya Kitaifa ya Utawala
Kila atakayechaguliwa/teuliwa na mkoa/mji wake kugombea nafasi kitaifa ni lazima kuhakikisha kuwa wanatuma barua pepe ya taarifa zao (profile/resume), ikiambatana na picha zao kwa kamati ya uchaguzi,
Ni muhimu kuzingatia muda ulipangwa hapo juu, ili ziweze kusambazwa kwa watu kuwapa na muda wa kutosha kufanya maamuzi ya nani watakayemchagua.
Taratibu nyingine za uchaguzi zitaendelea kutolewa, ikiwa ni pamoja na upigaji wa kura wenyewe katika siku hiyo.
Kwa Habari zaidi wasiliana na Kamati ya Uchaguzi :
Uniting-Communities@yahoogroups.com

Tel: 07908010344.

Wadau wenzangu wa UKerewe, kama kuna mtanzania anaishi hapa Cambridge naomba tutafutane kwa namba +447529525176...kwani tangu nije nina mwezi wa tatu sijaona Mmatumbi mwenzangu hapa.
ReplyDeleteAsanteni
Cambridge Diaspora.
VIPI KUHUSU SISI WASOMALI LAKINI TUNA ASILI YA TANZANZANI KUTOKA GEREZANI,KARIAKOO NA KINONDONI TUNA RUHUSIWA KUJIUNGA NA KUGOMBEA UONGOZI MAANA UKO KWETU MOGADISHU HAKUNA NCHI TENA.
ReplyDelete