Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro lager, George Kavishe akiongea na waandishi wa habari leo juu ya wasanii waliofanikiwa kuingia katika kinyang'anyicho cha kutafuta wasanii na vikundi bora vya muziki kwa mwaka 2009.Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro lager ,George Kavishe (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika leo ndani ya Makao makuu ya TBL. Kushoto ni Mkurugenzi wa masoko wa TBL, Bw. David Minja.Mratibu wa tuzo za Kili Music Awards ambaye pia ni mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Angelo Luhula akitangaza majina ya watakaoshiriki katika kusaka wasanii na vikundi bora vya muziki 2009 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya Bia ya TBL. Shoto ni Neema Mwingu kutoka shirika la ukaguzi wa mahesabu Deloitte Touche na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya One Plus Fina Mango (kulia) akiwa na mafisa wa kampuni ya Deloitte Touche walikifuatilia kwa makini utajwaji wa majina ya washiriki wa tuzo za Kili Music Awards 2010
baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika mkutano huo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa
Mkurugenzi wa One Plus Fina Mango akibadilishana mawazo na Neema Mwingu kutoka Deloitte Touche mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari.
===================================

Wafuatao ndio watakaowania (nominees)
wa Kili Music Awards 2009

MWIMBAJI BORA WA KIKE

1.LADY JAYDEE
2.MWASITI
3.MAUNDA ZORO
4.VUMILIA
5.KHADIJA YUSUPH

MWIMBAJI BORA WA KIUME

1.MARLOW
2.BANANA ZORO
3.MZEE YUSUF
4.ALI KIBA
5.CHRISTIAN BELLA

ALBAMU BORA YA TAARAB

1.JAHAZI MODERN TAARAB – DAKTARI WA MAPENZI
2.5 STARS MODERN TAARAB – RIZIKI MWANZO WA CHUKI
3.COAST MODERN TAARAB – KUKUPENDA ISIWE TABU
4.NEW ZANZIBAR STAR – POWA MPENZI
5.EAST AFRICAN MELODY - KILA MTU KIVYAKE

WIMBO BORA WA TAARAB

1.JAHAZI MODERN TAARAB – DAKTARI WA MAPENZI
2.5 STAR MODERN TAARAB – WAPAMBE MSITUJADILI
3.KHADIJA YUSUPH – RIZIKI MWANZO WA CHUKI
4.JAHAZI MODERN TAARAB – ROHO MBAYA HAIJENGI
5.COAST MODERN TAARAB – KUKUPENDA ISIWE TABU

WIMBO BORA WA MWAKA

1.MARLOW – PII PII (MISSING MY BABY)
2.DIAMOND – KAMWAMBIE
3.BANANA ZORO – ZOBA
4.MRISHO MPOTO – NIKIPATA NAULI
5.HUSSEIN MACHOZI – KWA AJILI YAKO

WIMBO BORA WA KISWAHILI (BENDI)

1.MACHOZI BAND – NILIZAMA
2.AFRICAN STARS BAND – MWANA DAR ES SALAAM
3.TOP BAND – ASHA
4.FM ACADEMIA – VUTA NIKUVUTE
5.EXTRA BONGO – MJINI MIPANGO

ALBAMU BORA YA BENDI

1.AFRICAN STARS BAND – MWANA DAR ES SALAAM
2.KALUNDE BAND – HILDA
3.MSONDO NGOMA MUSIC BAND – HUNA SHUKURANI

WIMBO BORA WA R&B

1.BELLE 9 – MASOGANGE
2.DIAMOND – KAMWAMBIE
3.AT-STARA THOMAS – NIPIGIE
4.MAUNDA ZORO – MAPENZI YA WAWILI
5.STEVE – SOGEA KARIBU

WIMBO BORA WA ASILI YA KITANZANIA

1.MRISHO MPOTO – NIKIPATA NAULI
2.MACHOZI BAND – MTARIMBO
3.OFFSIDE TRICK – SAMAKI
4.WAHAPAHAPA BAND – CHEI CHEI
5.OMARI OMARI – KUPATA MAJAALIWA

WIMBO BORA WA HIP HOP

1.JOH MAKINI – STIMU ZIMELIPIWA
2.QUCK RACKA – BULLET
3.CHID BENZI – POM POM PISHA
4.MANGWEA – CNN
5.FID Q – IM A PROFESSIONAL

WIMBO BORA WA REGGAE

1.HEMEDI – ALCOHOL
2.DABO FT.MWASITI – DON’T LET I GO
3.MAN SNEPA – BARUA
4.MATONYA FT,CHRISTIAN BELLA – UMOJA NI NGUVU
5.A.Y – LEO (REGGAE REMIX)

RAPA BORA WA MWAKA (BENDI)

1.CHOKORAA
2.FERGUSON
3.KITOKOLOLO
4.TOTOO ZE BINGWA
5.DIOF

MSANII BORA WA HIP HOP

1.JOH MAKINI
2.FID Q
3.CHID BENZI
4.MANGWEA
5.PROFESSOR J

WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI

1.BLUE 3 FT.RADIO AND WEASAL (Goodlife) – WHERE YOU ARE
2.KIDUMU FT.JULIANA – HATURUDI NYUMA
3.CINDY – NA WEWE
4.RADIO AND WEASAL (Goodlife) – BREAD AND BUTTER
5.KIDUMU – UMENIKOSA

MTUNZI BORA WA NYIMBO

1.MZEE YUSUF
2.MRISHO MPOTO
3.LADY JAYDEE
4.BANANA ZORO
5.MZEE ABUU
6.FID Q

MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO:PRODUCER WA MWAKA

1.LAMAR
2.MARCO CHALI
3.HERMY B
4.ALLAN MAPIGO
5.MAN WATER

VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA

1.LADY JAYDEE – NATAMANI KUWA MALAIKA
2.DIAMOND – KAMWAMBIE
3.A.Y – LEO
4.BANANA ZORO – ZOBA
5.C PWAA – PROBLEM

WIMBO BORA WA AFRO POP

1.BANANA ZORO – ZOBA
2.ALI KIBA – MSINISEME
3.MARLOW – PII PII (MISING MY BABY)
4.MATALUMA – MAMA MUBAYA
5.CHEGE – KARIBU KIUMENI

MSANII BORA ANAYECHIPUKIA

1.BELLE 9
2.DIAMOND
3.BARNABA
4.QUICK RACKA
5.AMINI

WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA

1.AT FT. STARA THOMAS – NIPIGIE
2.MANGWEA FT. FID Q - CNN
3.BARNABA FT. PIPI – NJIA PANDA
4.MWANA FA FT. PROF. JAY NA SUGU – NAZEEKA SASA
5.HUSSEIN MACHOZI FT. JOH MAKINI – UTAIPENDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Jamani Fina, looking good darling!

    ReplyDelete
  2. jamani sisi wapenda regee hatuhesabu kama hizo za bongo fleva ni regee wekeni wakali wa regee mbona wapo watz halisi

    ReplyDelete
  3. nitafurahi kuona wimbo wa kushirikikiana wa NIPIGIE,Stara na At ukishinda

    ReplyDelete
  4. Hussein machozi hayumo kwenye listi ya waimbaji bora wa kiume????!

    ReplyDelete
  5. joh makini here we go, thz z ur time,watu wa kili- sisi streets we r fade up,speakin of h.i.p h.o.p thiz time around z joh, thz guy hz bn workin hard to desserve thz, so dont take away from him thz time around, plz plz, iko wazi...iko wazi...arachuga stand up

    ReplyDelete
  6. Nilikuwa nategemea Hussein Machozi katika kuwepo katika categories zingine as well;Wimbo Bora,Msanii Bora.

    ReplyDelete
  7. Marlow na Mzee Yusuf watapambanishwa vipi ilhali nyimbo zao hazikutani mahala popote. Basi sema unapambanisha BONGO FLEVA na TAARAB........Pambanisha waimbaji wa taarab kivyao na Bongo fleva kivyao

    ReplyDelete
  8. WEWE KAVISHE VAA SHATI VIZURI BASI MANGI. FUNGUA VIFUNGO VIZURI BWANA, MTU MZIMA WEWE. ALA

    KAMA VIPI BASI ONDOA SHATI LOTE KABISA.

    ReplyDelete
  9. Mtoto wa CoastMarch 26, 2010

    Kili -Music Award organizers nawapa shavu kazi njema.

    Maoni yangu:

    1. Hakuna usawa katika kuchagua baadhi ya makundi(categories).

    Mifano:

    i.Ukisema Msanii bora anayechipukia vipi mmeacha msanii bora aliyebobea na kudumu katika fani muda mrefu ambaye pengine ndiye hata amemnyanyua huyo anayechipukia! Naye anahitaji sana kutiwa moyo aendeleze libeneke.

    ii. Katika aina ya miziki tumeona R&B,Reggae,Hip Hop, Taarab, wimbo bora wa Kiswahili- bendi - hapo mmechanganya somo kwa sababu kigezo si lugha wala organisation (bendi / mtu mmoja mmoja). Pengine mngetafuta lugha nyingine kama muziki wenye mahadhi ya rumba au Soukous n.k

    iii.Katika taaluma au tuseme nafasi katika muziki tumeona, Muimbaji bora, Rapa bora, Producer bora, je wapi Mpiga ala bora na wapi mchezaji (Dancer) Bora. Jamani niseme tu wazi kuwa hao watu wawili ni muhimu sana kuliko tunavyodhani. Kuna nyimbo ngapi zimegonga nyoyo za watu kwa sababu TU ya beats zake toka kwa wapigaji wa ala au je mnajua kuwa watu wengi katika bendi tunavutiwa sana na madansa na style zao kuliko hata rapa (after all Rapa ni muimbaji na tayari kuna tuzo ya muimbaji bora!)


    iv. Mwisho ni namna mnavyotangaza hizo Nominations. hapa umakini unatakiwa sana.

    Huwezi kusema tuzo ya Video bora ya Muziki; ukaitambulisha kama;
    Lady JayDee- Natamani kuwa Malaika bali utasema; Natamani kuwa Malaika- Lady JayDee au Machozi Band kama ndiye mmiliki wa hiyo album.

    Tuzo za wimbo bora huenda kwa mwenye haki milki. Ingawa kuna watu binafsi wachache mmoja mmoja, mara nyingi huwa ni Kampuni au Band.

    Na hata Producer bora ni Kampuni na sio mtu binafsi (yule mtumishi anaye fanya mixing).

    HILI NI SUALA LA MUHIMU SANA NA HIVYO NALISISITIZA KWA HERUFI KUBWA. MAANA HAPA NDIPO MNAWEZA KUSHIRIKI KUMINYA HAKI ZA WASANII WENGINE (WASIO KATIKA PICHA) KWA KUHALALISHA MAJINA YA MASTAA TU WAKATI WIMBO NI MALI YA KIKUNDI CHOTE AKIWAMO HATA YULE MDOGO LAKINI WA MUHIMU AMBAYE KAZI YAKE HUWA KUUNGANISHA NYAYA NA KUWEKA SAWA VYOMBO N.K

    Pamoja na hayo machache , nazidi tena kuwapongeza. Na ni matumaini yangu kuwa mbele ya safari mtarekebisha kadiri inavyofaa na kustahili.

    ReplyDelete
  10. jamani hussein machozi asikose zawadi hapo amejitahidi sana mwaka jana ,na wimbo wa kwa ajili yako na utaipenda video na mandali ya nyimbo zenyewe ni nzuri sana

    ReplyDelete
  11. bongo kwa vyeo tumeanza kumeng'enya. yaani lazima neno mkurugenzi, mratibu, meneja nk nk ndio mambo yaende

    ReplyDelete
  12. Mimi kwanza naguna sana
    hivi nyie kili awards mpo sawa kweli?
    iweje maproducer ambao wametengeneza hits ngoma hawamo hivi hao maproducer bora huwa mnawachukua wanatengeneza nyimbo nyingi au wanaotengeneza hits singles pia
    1.marlaw - pi pi missing my baby katengeneza producer Tudd hayumo
    2.diamond - kamwambie katengeneza dogo Bob Junior pia hayumo
    3.mataluma - mama mubaya kafanya Enrico pia hajawekwa
    4.alikiba - msiniseme kafanya kgt pia hayumo
    Jamani hii ni aibu sana sijawahi ona kabisaa hamuoni tuzo za majuu zinavyokuwa mtu akitengeneza hit song?
    yani ni aibuuuuuuu sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...