Aliekuwa Mkurugenzi wa utumishi na utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi,Kisutu leo tayari kwa kusikiliza kesi yake.

Liyumba akiingia Mahakamani leoAliekuwa Mkurugenzi wa utumishi na utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba (kulia) akijadiliana jambo na wakili wake Bw. Majura Magafu kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu leo.Liyumba akiingia katika Chumba cha Mahakama

Liyumba akitolewa Kizimbani leo
Liyumba akipanda ngazi kuelekea katika chumba cha Mahakama leo Liyumba akisindikiwa na maaskari wa Jeshi Polisi na Magereza wakati akitoka kusikiliza kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo. Liumba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alikuwa akikabiliwa na mashitaka mawili, moja likiwa ni kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 221 leo ameondolewa shitaka la kutumia vibaya madaraka na hivyo kubaki na kosa moja.Liyumba aliyekuwa akikabiliwa na kesi hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, alifutiwa shitaka hilo baada ya mawakili wa upande wa utetezi kutoa vielelezo vilivyothibitisha kuwa mteja wao hakuwa na kesi ya kujibu.Mshitakiwa huyo amerudishwa rumande mpaka Aprili 22 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. That's what we call "the positive approach".The guy has nothing to worry about as he has pay his political contributions/donations to the administration.

    ReplyDelete
  2. askari wanane wanamlinda mtu mmoja, tena hao ndio tunaowaona kwenye picha wengi waliokuwa hawapo hapo sijui ni wangapi. hivi kweli kulikwa na haja ya kuwepo wote hao pale?

    au ndio ule mtindo ule ule wa zamani? pakichezwa yanga na simba askari wote huvaa sare zao na kuelekea uwanjani japokuwa hawako shift ili wapate kuona game bure?

    ReplyDelete
  3. Bw. Liyumba pole kwa huu mtihani lakini ninaamini utashinda.

    Uamuzi wako wa kutetewa na Bw. Majura unaonesha uko makini sana.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. toka mwanzo nilijua hii kesi ilikua haina nguvu. kwanini wamemueka huyo bwana muda mrefu rumande. huu ni uonevu mtupu.

    ReplyDelete
  5. Money talks..bull shit walk!

    ReplyDelete
  6. The Tz gorvernment has no grounds to put a case on Liyumba wanatapatapa tu.Liyumba yuko jela jela politically na kwa nguvu za state tu,everybody knows that.

    ReplyDelete
  7. uu ni upotevu wa pesa za umma ili watu wakidhi matakwa yao binafsi. Kama mmekanyagana miguu huko mitaani kwanini kulipiza kisasi kwa kdi ya wananchi?

    ReplyDelete
  8. HIYO NDIO BONGO YA WENYEWE BWANA

    WAMEMSHIKA KWA SPEED 200 YANI KWA NGUVU ZA GESI YA PEPSI NA MDOGO MDOGO WATAMUACHIA

    USIFANYE MCHEZO NA MAMBO YA NOTI WANA JAMII MONEY TALK

    HAPO NENDA WEWE ULIEIBA KANDAMBILI UTACHEZEA KIFUNGO

    AU KAJARIBU KUIBA TAA YA GARI YA KIGOGO FULANI UTAFUNGWA MPAKA UKITOKA UJUWE UMEZEEKA

    BONGO SHERIA INAFATA WATU SIO WATU WANAFATA SHERIA

    WATU WANAIBA MABILIONI WAKATI WANANCHI WANAKUFA KWA NJAA MAGONJWA WENGINE HAWANA UWEZO WA KULIPIA ADA ILI KUPATA ELIMU

    KILA GOTI LITAPIGWA SIKU HIYO IKIFIKA. PARAPANDA ITAKAPOLIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...