Kondomu feki kiasi cha 70,000 zimekamatwa na kuteketezwa na mamlaka ya udhibiti wa viwango TBS na bosi mmoja wa taasisi hiyo Bw. Lazaro Msasalaga amesema nyenzo hizo za ngobni zilikamatwa bandarini Dar kutokea India baada ya kuagizwa na kampuni ya jijin i Dar iitwayo Generics & Specialities Company ambayo ilipigwa faini ya shilini milioni 3.5 kwa kuingiza bidhaa isiyofaa kwa matumizi ya binadamu pamoja na gharama za uteketezwaji wake.
Kondomu hizo, zinazokwenda kwa jina la 'Kama Sutra' zimetengenezwa na kampuni ya J.K Ansell Ltd ya Aurangabad, India, ambayo unadai kwenye gamba lake kwamba zimejaribiwa kielektroniki na kuridhisja viwango vya kimataifa vya ISO na kupewa namba ya uthibitisho 4074 of 2002.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Huu ndio utani wa Wabongo. yaani kampuni ya export yenye turnover ya mamilion ya $ inaadhibiwa kwa faini ya TZS 3.5 mil!!!! Kama tunataka maendeleo ya kweli basi tuanze kuwa serious na jinsi tunavyofanya kazi zetu. vinginevyo tutayasikia tu.

    ReplyDelete
  2. hapa hukumu yake ni kifo tu, huyu mtu ni muangamizazi. Mimi huwa sinunui zana za nje hata siku, siziamini kbs.

    mtumiaji wa zana za nyumbani

    ReplyDelete
  3. uko tunapokwenda sasa ni hatari!!!

    ReplyDelete
  4. ANKAL MICHUZI NAOMBA NIKUULIZE. NIKITAKA KUSOMA HABARI ZA SIKU MBILI AU TATU ZILIZOPITA NINAFANYAJE. ZAMANI NILIKUA NIKIMISS HII BLOG KWA SIKU MBILI HIVI NAWEZA KUINGIA KWENYE KUMBUKUMBU NA KUPATA HABARI. SIKU HIZI NIMEJARIBU KAMA MARA MBILI HIVI NA WALA SIFANIKIWI. KUMBUKUMBU YA APRIL INANIPA HABARI HIZI HIZI ZILIZO KWENYE FRONT PAGE...

    MAJUKUMU MENGI SIKU HIZI SASA KUFUNGUA BLOG KILA SIKU SIWEZI ILA NINAPENDA KUCATCH UP NA MAMBO YALIYOPITA ILA SIFANIKIWI KABISA...

    NAOMBA UNIELEWESHE
    THANKS IN ADVANCE

    ReplyDelete
  5. Hiyo heading mithupu haijakaa vizuri, hicho chakula siyo cha usiku tu! kinaliwa wakati wowote, infakti hata ukiwa kazini ukisikia maumivu ya mgongo, unapata msosi huo na kurudi kazini kama kawaida.

    mdau, mtumiaji mzuri wa msosi.

    ReplyDelete
  6. wadosi kweli noma!
    Wanataka kueneza kwa nguvu DINI ya
    KAMASTURA!!
    Kamasutra ni dini au madheebu ya wafuasi fulani nchini India,
    Dini ya Kamastura,ibada zao ni zinaa au Ngono,yaani waumini wanakutana na kufanya ngono kwa kuchangiana,bora ndomu hizi zilivyopigwa moto,

    ReplyDelete
  7. Jamani inatisha hii!mtu unajua 99.999999 uko salama kwa kutumia condom kumbe doooooh!.

    ReplyDelete
  8. Duhh! hii sasa ni soo. Nadhani nilikatumia jana usiku, nikidhani nipo salama, kumbe noma. SIRIKALI, jamani tusaidiane, kwani sijuwi tutafika wapi? Msiendelee kujaza matumbo jamani, angalieni na usalama wetu.
    Nadhani ili kuonyesha mfano, hao jamaa wangefutiwa na leseni ya kuagiza hizi zana.

    Serikali ingeweka ILANI kwenye zote za wageni.

    ReplyDelete
  9. Hizo ni zile zilizokamatwa, je ni ngapi zimepenya? Tanzania bila ukimwi ina"mashaka"!>Shukrani za pekee ziwaendee mliofanikisha hili maana mmeokoa watanzania takribani 70 alfu jumlisha 70 alfu wengine suppose ni waume wa watu hao, maana ukweli ndio huo watu wengi wanaoishi maisha ya mke na mume au mchumba na uchumba hii kitu haitumiki ili kudumisha uhusiano.

    ReplyDelete
  10. sasa kama hivi tutaponea wapi jamani?

    ReplyDelete
  11. florian rweyemamuApril 17, 2010

    1) Doing business well is very, very hard
    2) Few people do business well
    3)The conceptual frameworks and tools underlying the conduct of today's business are hopelessly outdated

    source: The World is Flat by Thomas L.Friedman

    ReplyDelete
  12. MIMI NAAMINI ZIMESHAPITA CONDOM NYINGI NA HIZO ZILIZOKAMATWA NI AROBAINI YAKE ILIFIKA.

    ReplyDelete
  13. Kila mtu akapime. Unatakiwa ujue status yako kila baada ya mwaka na kama unakula chaakula cha jiona kama snacks vile basi unatakiwa ukapime kila miezi mitau au sita hivi...Uwe umeoa/umeolewa au la as long you are doing it that is it....."TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA" Just don't trust nobody

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...