geti la kuingilia hifadhi ya taifa ya Mikumi ambako ankal na maankal wake walipita leo kuelekea Mbeya kwenye msiba wa nyanya yao
wese linaongezwa katikati ya hifadhi ya Mikumi

maankal wa ankal, moses (shoto) na tony wakijiandaa kuongeza wese garini
nje kidogo ya Igurusi ankal na ankal wake tony wakijipatia gahawa na sangweji leo...




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. at last michuzi asema asili yake ni mbeya.

    ReplyDelete
  2. Simba huyo Simba huyo Nyuma yenuuuuuuuuu. Ah Kumbe Yanga ndomana hamuogopi.

    ReplyDelete
  3. Michuzi unakua kama hujatoka ulaya last week bwana.... Kwani hamna vituo vya petroli? Au ndio mafuta ya wizi nini? Kichekoooooooooooooo....

    ReplyDelete
  4. Hivi mpaka zama hizi bado watanzania tunatembea na madumu ya mafuta nyuma ya gari kweli ?
    Halafu ikitokea "freaky accident" na mtu aungue bila kutambulika tutasingizia nini ? Wazalendo wenzangu, hebu tujifunze kusonga mbela badala ya kubali palepale au kurudi nyuma, please.

    ReplyDelete
  5. Ni kweli twajua Ankal asili yake Mbeya lakini huyu Nyanya Mzungu!!Tueleze kaka Michuzi, Vipi huyu bibi mzungu inakuwaje??wewe una Vi-DNA vya kidhungu kumbe??!!

    ReplyDelete
  6. Pole sana

    ReplyDelete
  7. Mbona 'vidumu' tena... au hamuamini mafuta ya 'mikoani'?
    Au?

    ReplyDelete
  8. Ankal, ingawaje sikumfahamu Nyanya yenu...poleni sana kwa msiba na kamzikeni salama. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema na kumpa mapumziko ya milele, Amen.

    Mlowezi wa Ukerewe
    (asili ya Lake Nyasa - mla Mbasa na kikasa)

    ReplyDelete
  9. Ankal angalia nyuma yako simbaaa huyooo kimbia kwenye gari, fanya harakaaaaaa! Poleni kwa msiba ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Alikokwenda ni kuzuri sana ndo maana wanaoenda hawarudi!
    Safari njema! inamaana njiani hakuna gas stations za kuongeza mafuta? itabidi next time kuweka full tank sio wese la kibaba!
    Mdau wa damu USA

    ReplyDelete
  10. Ankal inakuwaje unabeba mafuta kwenye gallon wakati njia nzima kuna vituo vya mafuta? ni hatari kutembea na mafuta kwenye gallon ankal!au gari yako haina speedalmetre?

    ReplyDelete
  11. ankal mithupu hilo tumbo kama linekuwa na uwezo wa kutoa malalamiko yake ingekuwa balaa, kwenye misosi ya draft twende chai ya "left hand" twende, kaaazi kweli kweli!!!!!

    ReplyDelete
  12. MshirikinaApril 09, 2010

    Yaani bado mna mambo ya kizamani tu ya kuweka mafuta kwenye vidumu kama malendrova ya Ifakara-Mahenge! Khaah!

    Yaani juzi tu umetoka kulipwa HONORARIAM ya kuprizenti pepa kule kwenye Dayaspora umeshindwa kuweka ful tenk!?! Mweeh!
    Haiwezekani ful tenk kwa gari kama hiyo liishie Mikumi.

    Halafu msiwe mnazoea kusafiri familia kwenye gari moja namna hiyo. Sio vizuri

    ReplyDelete
  13. Ankal hata wewe umeweka chata ya OBAMA aaah Ankal namma gani hapo ? Ungeweka ya JK tafadhali au kama unaona noma basi hata ya Baba wa Taifa.

    ReplyDelete
  14. Ankal,siku nyingine kama utaishiwa wese kwenye hifadhi hiyo,andika kabisa wosia na uteue kabisa mtu atakaye endeleza libeneke la blog yetu ya jamii.Ni vizuri sana kama utatubu kwa Mungu na kujitakasa kabisa,maana kufumba na kufumbua anaweza tokea nyau pori(simba) akafanya selufu sevisi ,sidhani kama utapata hata nafasi ya kutubu.Nakumbuka nilipotembelea mbuga hiyo simba tuliwakuta barabarani kando kidogo wamepumzika,cha ajabu kuna jamaa mmoja ni kama kichaa huwa anatembea kwa miguu peke yake mbugani hapo lakini sijasikia kudhuriwa na simba hao,je simba hawali vichaa?

    ReplyDelete
  15. .....na wewe umekuwa mzee wa mafuta ya vibaba ? utaua fuel pump !

    ReplyDelete
  16. Jamani ankal hajasema asili yake ni mbeya.. kwani mbona huko mbeya wako wachaga, waluo, anyamwezi nk wameishi miaka kibao.. inawezekana ndugu na jamaa wameishi huko.. ankal hebu iweke wazi hii...

    ReplyDelete
  17. Ankal Mithupu, ukiwa Mbeya,sikiliza Mbeya Highlands FM Radio na kwa ujumbe huu pls fika pale MH FM Buma Bldg utoe tangazo lako lolote, its on the house!!
    Mdau Lawrence

    ReplyDelete
  18. ankal nini kimekufanya utembee na hayo madumu ya mafuta kwenye gari,huoni kama ni hatari?

    ReplyDelete
  19. duh ankal,gari yenu vipi?hamjui inatumia wese kiasi gani?kulikoni kutembea na galoni 2 za lita 20? nafikiri hata sheria hairuhusu kiasi kikubwa cha mafuta kama hicho,au mlinunua hapo kijijini? vinginevo hapo gari inakuwa kama bomb la petrol linalotembea,ni hatari sana ankal ajali ikitokea.naomba uweke hii comment itaelimisha wengi.

    ReplyDelete
  20. Ankal huko ni kujiadhiri!kubeba mafuta kwenye madumu kumepitwa na wakati

    ReplyDelete
  21. michuzi usifanye tena ujinga huo nihatari sana mnaweza kulipukiwa na hayo mafuta kwa jua kali ama mmesimama mtu anavuta sigara ikashika ni hatari sana kaka

    ReplyDelete
  22. Duu ankal!ile tisheti umeiuza kwa garama basi fix hiyo speedometer ili ujuage mafuta yanaishia sio kistukizia.ohooo,utaliwa na simba.tutampata wapi tena ankal kama wewe!lol!
    mdau Houston.

    ReplyDelete
  23. kweli wewe kiboko!!

    mbavu zangu

    ReplyDelete
  24. Vipi suala la kuweka mafuta ukiwa kwenye hifadhi ya taifa kimazingira?
    Sio uharibifu wa mazingira jamani. Mi naamini tone moja tuu la petroli ni hatari kwa viumbe. Mpo?

    ReplyDelete
  25. Ankal makusudi hayo sasa!!! mwangalie alivyojitwika kichwani hilo dumu.

    ReplyDelete
  26. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  27. Mi nimecheka sana hiyo kauli ya "ankal wa ankal"

    Kuhusu madumu nyie acheni tu hamjui ankal kapata wapi hayo mafuta na kwa bei gani.

    Zis iz Bongo. What you see in NOT necessarily what you get. Kila mtu na ujanja wake.

    ReplyDelete
  28. Asalaam alaykhum ankal!

    Poleni sana kwa msiba mola amlaze mahala pema peponi bibi yenu mpendwa amina.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  29. HIYO YOTE NI KUKWEPA KULANGULIWA MAFUTA BARABARANI AU? AU HAYO NDIO YALE MAFUTA YA KUKINGA KWENYE MAROLI BARABARANI KWA MIFUKO YA RAMBO PALE BUGURUNI? KAMA NDIO HAYO KAKA MNACHOCHEA WIZI... ANYWAYS INAELEKEA KUNA KA-SAVING FLANI MNAFANYA KWA MTINDO HUO.

    mZOZAJI

    ReplyDelete
  30. Wese kunyonyea porini yaleyale

    ReplyDelete
  31. ankal hiyo ze shati iliyochongoka enzi hizo tuliita kajogoo

    ReplyDelete
  32. Ankal umenikumbusha mbali sana kaka, na hiii picha ya mikumi kaka safari kunyumba kaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...