Kuna mtu anaweza kunifahamisha
umbumbu wangu wa TEKNOHAMA?.

Hivi blogu ya Ikulu ya Tanzania inaendeshajwe?
Haina habari za kila siku?
Hivi yote yanayotokea Tanzania, ziara za waziri mkuu hivi karibuni, mama Salma Kikwete, Rais Kikwete safari zake zote za mwezi mzima uliopita, risala zake, hotuba zake, angalau hayo tu yanashindikana kuwekwa kila siku?

http://mawasilianoikulu.blogspot.com/
Hivi idara ya mawasiliano ya Ikulu hawalioni hili?

Leo Jumapili 18.04.2010. Habari za mwisho kwenye blogu hiyo ni za Machi 18. Mwezi mzima umepita. Matukio mengi yamepita katika kipindi hicho, lakini hakuna hata picha wala nini. Tunaona picha kwenye blogu ya Michuzi, Mjengwa, Hakingowi, Mrocky, Wavuti na nyinginezo za watu binafsi.

Ikulu ka!

Basi wacha blogu, tovuti ya taifa la Tanzania, ndo´kichekesho! Manaake habari haziko katika mpangalio. Ziko shaghalabaghala! Angalieni wenyewe hapo chini
http://www.tanzania.go.tz/

Mbona tovuti za wizara mbali mbali habari zake ziko katika mpangilio? Hii ndio sura ya Tanzania nje ya nchi, lakini mwee?sisemi mengi.

Hata tovuti ya Waziri Mkuu
inapendeza iko katika mpangalio mzuri.

Wenu Tausi Usi Ame Makame,
Oslo
tausi@online.no

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tausi,

    wee acha tu..

    Naona jamaa wa mawasiliano wanatumia muda wao kwenye Faceboo, Twitter na kadhalika. Hawana muda na blogu!!!

    ReplyDelete
  2. jamani pitieni web ya kagame na linganisha na yetu.we are not seriouse

    ReplyDelete
  3. Ashakum si matusi, ustaarabu wa nyumba huanzia chooni!

    ReplyDelete
  4. Watanzania kwa kupenda makuu:

    Utakuta eti kuna kitu kinitwa "THE DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA" badala ya kusema tu kuwa ni msemaji wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...