Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Watano kulia) Rais Wa Zanzibar Amani Abeid Karume (Wasita kulia),pamoja viongozi wengine wa kitaifa wakiomba dua katika kaburi la muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abeid Amani Karume huko katika ofisi kuu ya CCm Kisiwandui Zanzibar leo asubuhi.wengine katika picha kutoka kushoto Naibu Waziri kiongozi wa SMZ Ali Juma Shamuhuna,Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar Salehe Ramadhani Feruzi,Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha, na makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Watano kulia) Rais Wa Zanzibar Amani Abeid Karume (Wasita kulia),pamoja viongozi wengine wa kitaifa wakiomba dua katika kaburi la muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abeid Amani Karume huko katika ofisi kuu ya CCm Kisiwandui Zanzibar leo asubuhi.wengine katika picha kutoka kushoto Naibu Waziri kiongozi wa SMZ Ali Juma Shamuhuna,Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar Salehe Ramadhani Feruzi,Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha, na makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein.
Maghorofa mpya yaliyopo mtaa wa Michenzani Zanzibar yaliyoanza kujengwa kwaajili ya makazi bora ya Wananchi wa Zanzibar na hayati Mzee Abeid Amani Karume na kukamilishwa na Rais wa sasa Amani Abeid Karume.Makazi hayo tayari yamenza kugawanywa kwa wananchi waliokusudiwa kwa utaratibu maalumu. Picha na Freddy Maro



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Alhamdu llillah Viongozi wetu wamependeza Inshallah Mungu awape kila la kheri awape ufanisi katika kazi zao ili tuuishi maisha bora.Amiin

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Rais wa Zanzibar kwa ktimiza azma ya ukamilisho wa majengo hayo muhimu kwa jamii. Aidha iwe fundisho kwetu hususan kwa viongozi wa nji hii kuwa enzi hizo Mh marehemu Karume aliwaza juu ya huduma hiyo na kuianza/kuitekeleza hima... Je ni kitu gani kiliuzuia mradi huu muhimu kwa wananchi mpaka leo? na pia imeshindikanaje kwa kipindi hiki cha miaka 34 kufanya hayo kote bara na visiwani?? Angeamka le mzee wetu hyu angetandika woote bakora. RIP A.A.Karume

    ReplyDelete
  3. Inashangaza kwa uongozi uliopo madarakani siku hizi hata kwa ngazi yoyote uianzia juu. Je hakuna mwenye wazo kama la mzalendo huyu - marehemu Karume - walao yakajengwa maghorofa mawili kama ya michenzani zanzibar kila mwaka kila mkoa? hivi ni kweli haiwezekani? inashangaza hata miradi mingi iliyopo licha ya ufadhili mkubwa wa wahisani ama inakwisha kwa muda mrefu sana tena kwa viwango vya chini ama ifie njiani? kulikooni??

    ReplyDelete
  4. wazanzibari wenzangu, ninakumbuka katika miaka ya mwisho ya 80 na awali 90 kulikuwa na uvumi kuwa ukipita usiku pale makao makuu ambapo penye kaburi la marehemu karume watu walikuwa wanaona jambo fulani la ajabu, jee hii ni kweli? kuna yeyote aliyewahi kuona?

    ReplyDelete
  5. hii project inafaa kuwekwa kwenye World Guinness Records kama the longest housing project ever. imeanza miaka ya 60 na imemalizika 2010. Tena ni jumla ya majengo nadhani 10 au 12 tu!!!!!!

    ReplyDelete
  6. RIP
    ONE OF THIS NATION'S FATHERS

    ReplyDelete
  7. kweli bongo mwendo pole x2 yameanza kujengwa some 40yrs ago sasa ndiyo yanakamilika?

    ReplyDelete
  8. nyumba hizi zilijengwa baada ya nyumba zilizokuwepo sehemu hizo kuvunjwa miaka hiyo ya late sixties na marehemu karume. wenye nyumba hizo waliahidiwa flat katika magorofa ya kisasa, hata hivyo wengi hawakupatiwa kwa vile mradi mzima ulizozota na ndio kwanza unamalizika mwaka huu.

    sasa sijui kama waliovunjiwa nyumba zao watapewa hizo flats au zitakwenda kwa kujuana, pia sijui kama waliovunjiwa nyumba watakuwa wako tayari kuhma tena katika nyumba walizopewa wakati ule kama ni temporary wakati flats zikijengwa.

    ReplyDelete
  9. AFADHALI HICHO KIDUCHU HUKU BARA KAZI YAO NI WIZI NA KUJENGA NYUMBA ZAO NA SISI TUNALALA KWENYE MBAVU ZA PANYA MTU AKIPITA NJE BASI NDANI WATUONA, HAMNA SIRI KUTAFUTA MTOTO HADI USIKU WA MANANI NA SOMETIMES HAIWEZEKANI HADI TUENDA PORINI. MWEEEE!

    ReplyDelete
  10. NIMEONA SHEMU KIBAO WAMEANDIKA "SIKU YA KARUME DAY" HIVI SAWA????

    ReplyDelete
  11. Hongera Wazanzibari, hata kama yakichukua miaka 100 hatimaye yakamilike na watu kupata makazi bora. Bara wananyang'anya ardhi kwa mafukara kuiuza kwa wenye nazo, wanagawana mali za umma na nyumba za viongozi halafu wanawaweka serikali inalazimika kuwagharamia viongozi wapya kuishi hotelini au kuwajengea nyumba kwa mipesa mingi ya Umma!!! Na wabara wamelalaaaaaaa!!

    ReplyDelete
  12. unaona jinsi gani bongo unavyopendeza kwa vazi hilo la wakuu wetu hapo juu hehehe bongo ni ya wenyewe bwana wengine wanajichomeka tu kwa nguvu za wadhugu

    ReplyDelete
  13. Hizi sikukuu kama hizi ilitakiwa watu waendelee na kazi kama kawaida na viongozi ndio wafanye mambo hayo,ni vzr kuwaenzi sikukuu ni nyingi mno uzalishaji na maendeleo kwa ujumla vinarudi nyuma. Takwimu zinaonyesha uchumi wa TZ kwa siku moja ni takribani Tsh.200bln, sasa zote hizo zimesimaa. Natoa hoja !!

    ReplyDelete
  14. I think now IS THE TIME TO EVERY Body Now Let That Is Not The Way Relatives TO GO! Any Idea Let TO MY WINNING RUN TO THIS PROJECT BIDER By PUTTING IN SWAHILI herein Will IAM TELLING YOU THESE BE IN A Ness A Year.

    ReplyDelete
  15. mdau wa Fri Apr 09, 06:56:00 AM, uhali gani? unatumia kitu gani mwenzetu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...