Na Mohammed Mhina
na
Athumani Mtasha
wa Jeshi la Polisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 42 wa Jeshi la Polisi kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 42 wa Jeshi la Polisi kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, imesema kuwa waliopandishwa vyeo kuanzia Machi 16, mwaka huu ni pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa tisa, Makamanda watano wa vikosi na Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Jeshi hilo waliopo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam na Zanzibar.
Kamanda Mssika amesema kati ya hao wapo Maafisa wanne wakuu ambao wamepandishwa vyeo kutoka vyeo vyao vya zamani vya Makamishna Wsaidizi Wandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Manaibu Makamishna wa Polisi (DCP).
Waliopandishwa kuwa Manaibu Kakamishna wa Polisi (DCP’s) ni Mkuu wa Huduma za Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi SACP Isaya Mngulu, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Afya nchini SACP Neven Mashayo, SACP Rashid Omari Ali, wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACPO Suleiman Kova.
Kamanda Mssika amewataja Makamanda 38 wakiwemo Makamanda wa Polisi wa Mikoa tisa ya Tanzania Bara na Visiwani kutoka Vyeo vya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP ambao sasa kila mmoja anakuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ambao ni Makamanda Thobias Andengenye wa Morogoro, Henry Salewi wa Kagera, Bi Celina Kaluba wa Singida na Kamanda Lucas Ng’hoboko wa Kilimanjaro.
Wengine ni Kamanda Absalom Mwanyoma wa Pwani, Simon Sirro wa Mwanza, Isuto Mantage wa Rukwa, Michael Kamhanda wa Ruvuma na Yahaya Rashidi wa mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kamanda Mssika amewataja Makamanda wa Vikosi waliopandishwa vyeo kuwa ni Mohammed Mpinga, wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Tresphory Anaclet wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini (FFU), Sospeter Kondela, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Ujenzi, Geofrey Nzoa Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na kupambana na Madawa ya Kulevya na Mkuu wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam Bi. Alice Mapunda.
Wengine ni Mkuu wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini Kamanda Hussein Nassoro Laizer, Mkuu wa Bohari Kuu la Polisi nchini Kamanda Adriano Magayane, Mkuu wa Kikosi cha Usafirishaji cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Kamanda Ali Mlege na Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Jonas Mgendi.
Wengine ni Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania kwenye Ofisi za Interpol Kanda ya nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika Kamanda Goodluck Mongi, Mkuu wa Kitengo cha Picha na Maabala ya Uchunguzi wa Vielelezo vya Makosa ya Jinai nchini (FB) Kamanda Hezron Gyimbi.
Wengine ni Kamanda Jamal Rwambow, Kamanda Lucas Haule na Kamanda Donald Ludamila wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Makao Makuu, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Lucas Kusima, Kamanda Saidi Juma Hamis kutoka Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu.
Kamanda Mssika amesema kuwa wengine walipandishwa ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mifumo ya Mitangao ya Kompyuta ya Jeshi la Polisi nchini kamanda Anyisile Kyoso, Kamanda Renatus Chalamila, Mwanasheria wa Jeshi la Polisi nchini Kamanda Donald Kaswende na Kamanda mwanamke Adolfina Chialo.
Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Abdulrahman Kaniki, Msaidizi wa Mkuu wa Operesheni Maalum nchini Kamanda Hezron Kigondo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zananzibar Kamanda Mussa Alli Mussa na Kamanda Hamdani Makame wa Ofisi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Mkuu wa Mipango Kamanda Ernest Mangu, Kamanda Makame Ali Makame, Kamanda Mwalim Ame na Kamanda Mpinga Gyumi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Mimi naomba kuuliza jamani. Hivi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi hana Mamlaka ya kupandisha vyeo askari polisi au wanajeshi mpaka wa wapandishwe na Amiri jeshi mkuu ambaye ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano??
ReplyDeleteAsenti.
Nampongeza kamanda wa mkoa wa kaskazini Pemba, nilikubari hilro kamanda linapiga kazi kiutendaji zaid.
ReplyDeleteGod bless him
we mchangiaji wa kwanza acha uchonganishi kwa marais wetu. ila mi nawahurumia upinzani yaani hayo ni maandalizi ya kupigwa vizuri kwa sababu jamaa wanaongezewa mzuka kwamba ni watendaji bora ili mwezi wa kumi watie bidii sawa sawa ya kuwatandika wapinzani
ReplyDeletekova letu jamani. kamanda la ukweli
ReplyDeleteKazi nzuri wanazozitenda ziko wapi? Mbona wa2 bado 2nakamatwa kwa uzuraji? Piteni kinoclain mida ya saa mbili ucku au tatu, nne utaona wa2 wanafungwa mashati. Huu ni uwonenu, askari wa post bado wanakamata wa2 kwa uzuraji na wakukifiksha ki2oni kama una buku tano wakikufikisha magomeni na kesi wanakupa. Jakaya uwe unafanya mikutano na wananchi wako kama anavyofanya Obama. Tafadhari uwe unaongea na raia wako na uwalize nini wanatendewa mitaani maana wewe ujui. Yanayotendeka mitaani ni mengi. Jakaya mwaka juzi alitembelea gereza la keko alilia kwa machozi. Uliza kama alifanya mabadiriko yeyote? akufanya lolote, keko bado iko vile vile.
ReplyDeleteMdau, Londo, Lindi
I DONT UNDERSTAND THEREFORE MY APPOINTMENT OF THIS POLICE MAN AND WOMEN OF POLICE DEFENCE FORCE BECAUSE OF MANY BANDITS AROUND OUR COMMUNITY AND STREETS OF EVERY CORNER OF DAR AND THEIR NEIGHBORINGS. THE BANDITS SITUATION IS NOW VERY CUMBERSOME INDEED AND CERTAINLY IT AFFECTS OUR POOR CHILDREN AND OLDER WOMEN WHO ARE NOT ABLE TO HELP THEMSELF. MR. PRESIDENT KIKWETE HOLY FATHER PLEASE HELP YOUR PEOPLE COMBATE THESE BANDITS FROM KILLING OUT OUR CHILDREN AND OLDER PEOPLE OF TANZANIA, IM VERY SICK TIRED OF THIS ISSUE WHICH CAN NOT BE ABLE TO DISSAPEAR AFTER DECADE OF VIOLENCE AND HUMANITY, MICHUZI PLEASE HELP US TO PUBLISH THIS THINGS IN THE BLOGS OF SOCIETY. THANK EVERYBODY FOR UNDERSTAND EACH AND EVERY THINGS.
ReplyDeleteHon Peter Nalitolela is officially back, great!
ReplyDeleteSASA KILA MTU AKIWA NA CHEO NI NANI ATAMKOMAND MWENZAKE?
ReplyDeleteWE MCHANGIAJI WA KWANZA: SOMA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977:
ReplyDeleteIBARA YA 33(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.
IBARA YA 34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano
katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote
yahusuyo Tanzania Bara.
IBARA YA 147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au
kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au
kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu
wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina
mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi
wa Tanzania.
IBARA YA 148(1)(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayo
yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani-
(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi ya ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(b) madaraka ya kuwateua watu watakaojiunga na majeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshini
wanajeshi;
(c) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongozavikosi mbali mbali vya majeshi ya ulinzi;.....
NYONGEZA YA KWANZA KATIKA KATIBA:
Mambo ya Muungano:
Kifungu 3. Ulinzi na Usalama.
Kifungu cha 4. Polisi.
HIVYO, RAIS WA SMZ HANA MADARAKA JUU YA JESHI NA ULINZI WA TAIFA. YEYE SI AMIRI JESHI.
LABDA: kwa maoni binfsi sijui Mhe. Rais anatumia vigezo gani vya utendaji kuwapandisha vyeo Maafisa wa ngazi za juu wa Polisi wakati wapambanaji (wenye vyeo vya chini) bado wanaumia na hakuna matokeo yeyote mazuri kwenye vita dhidi ya uhalifu hapa nchini.