Assalamu alaikum Mkuu wa Wilaya ya nanihii na wadau wote.
Naomba kama kuna mtu ambaye anafahamu Vyuo ambavyo vinatoa nondo za Udaktari-MD nchini India au China anipatie majina au websites zake.
Santeni sana.
email yangu ni mkijawangu@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Wewe acha uvivu, kesho kutwa tena utaomba tukusaidie jinsi ya kukata ticket ya ndege. usipende kutafuniwa.. amka kijana tena ndio kama unataka kusoma MD unatakiwa uwe smart hapo juu!!. nachotaka kukushauri ni kuwa ingia kwa google search then andika kitu unataka hakika utapata!!..nimefungua kwa google nimekuta list ya vyuo vingi sana..sasa ni wewe tu uchague unakitaka kipi kutokana na chuo chenyewe kilivyo.. so jaribu kutafuta kwanza mwenyewe kabla ya kuomba msaada..Naweza nikaumabia chuo fulani kumbe boom kabisa ila wewe ukiingia kwa google utaviona na utachagua kulingana na uwezo wako
    Mdau

    ReplyDelete
  2. wasiliana na hii website kwa taarifa zaidi za vyuo vya udakitari nchini China pamoja na scholarship duniani kote,mimi nimejiunga nayo na wanatoa update kila mara.

    www.mallaba.ning.com

    mdau

    ReplyDelete
  3. Indian Institute of Management (IMM) kiko mji wa Ahmedabad. Mwambie aasearch kwenye internate for more details aandike

    Indian Institute of management (IIM) Ahmedabad India atakipata

    ReplyDelete
  4. Naomba msaada jamani. Natangaliza shukrani zangu kwa wadau popote pale mlipo. Namtafuta bwana mmoja anaitwa TASI namfahamu kwa jina moja tuu. Tulikutana naye Dar es salaam maeneo ya Wizara ya ardhi. Tulifika hadi kwake maeneo ya Mbezi - samaki wabichi au tangi bovu. Nilimpeleka hadi nilipokuwa nakaa pia. Aliondoka mapema kurudi Sudan alipokuwa anafanyia kazi IT-UN na mimi nikarudi Norway. Lakini nasikitika nilipoteza contact zake na nina nahitaji sana kuwasiliana naye amjuaye huyu jamaa anisaidie jamani. Mke wake alikuwa anafanya ofisi fulani maeneo ya ubalozi wa USA wa zamani. Huyu bwana ameishi USA muda mrefu kabla ya kwenda Sudan. Tuwasiliane kwa email. aal090tz@gmail.com. Asante sana kaka Michuzi

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau utaweza kusoma Udaktari kweli wakati unashindwa kufanya research mwenyewe kwenye mtandao. Hujawahi kusikia Google? Ebu wacha uvivu..nenda google ukatafute hivyo vyuo mwenyewe...wabongo kwa kupenda urahisi? Hili si swala la kuwauliza wana jamii...labda ungetaka mtu akusaidie shule gani ni nafuu zaidi, ama shule gani ina wabongo ambao wanaweza kukusaidia ningekuelewa..lakini eti wewe unataka kujua shule gani wanatoa nondo ya udaktari India ama China..ziko mia kidogo...fanya utafiti mwenyewe.

    ReplyDelete
  6. Mkuu bora uende Uturuki Kwani ni cheapest compare na hao vili wana miundo mbinu bora

    ReplyDelete
  7. MI NAKUPA MSAADA TU WEWE GOOGLE TU, MAANA WAKINA OYOOYOO (CHAI) WAKIINASA TU UNALO

    ReplyDelete
  8. mkuu mbona vyuo ni vingi bongo, wenzio tunajuta huku urusi tulipo
    Soma bongo......
    Binafsi sikushauri usome udaktari India ama china, labda kama unaenda kwa masters
    Ahsante.
    Mdau wa urusi nikiwa vakesheni Nairobi

    ReplyDelete
  9. ukigoogle kwenye hihi hii blog kuna mtu ameweka vyuo vya China ni majuzi tu

    ReplyDelete
  10. wewe mtu ambaye humshauri mwenzio kusoma china unamamo yako,..wengi wenu mnaishia kuwa walevi tu na mnaona shule ngumu..kusoma china kunafaida kibao tu practiclas ni nyingi compared na bongo ambako theory mpaka mwisho..
    wewe search google.
    hakuna lugha ngumu as long as u work hard on it

    ReplyDelete
  11. Bwana mdogo nakushauri kama ni shahada ya kwanza usomee hapahapa nyumbani halafu uende nje kwa shahada ya pili. Miaka ya kumaliza kozi ni ile ile. Ukirudi unakuwa kibopa wa maana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...