KATIKA HALI ISIYO YAKAWAIDA LEO HUKO MJINI KIBAHA ENEO LA KWA MFIPA, MNAMO SAA 4 NA DAKIKA NYINGI ASUBUHI LILITOKEA AJALI YA NGUZO MOJA TA TANESCO IKIWA NA NYAYA NNE, AMABZO ZIMEKATISHA BARABARA ILITAKA KUANGUKA KUTOKANA NA MVUA, NA HIVYO KUSABABISHA NYAYA ZAKE KUINAMA NA KUKARIBIA CHINI LAKINI BILA YA KUKATIKA, NA HAPO MAGARI YALISHINDWA KUPITA KWA URAHISI NA KUSABABISHA FOLENI KALI,

KILA PALIPO NA TATIZO SULUHISHO PIA LIPO. WALIJITOKEZA VIJANA WA ENEO HILO KWA LENGO LA KUTOA MSAADA, WAKIWA NA VIPANDE VYA MITI MIKAVU TAYARI KUINUA NYAYA NA KUWEZESHA MAGARI KUPITA.
LAKINI WALIPOONA WANFANYA KAZI YA KANISA SIKU YA IJUMAA KUU WALIAHIRISHA ZOEZI LA KUPITISHA MAGARI BURE. WAKAANZA KUDAI MALIPO KWA KILA GARI KUBWA LILILOPITA HAPO.
BAHATI NZURI KWA MAGARI MADOGO HAIKUWA NA UGUMU KWANI YALIWEZA KUPITA BILA KUGUSA NYAYA HIZO HIVYO YENYEWE HAYAKULIPISHWA CHOCHOTE.

GHAFLA ZOGO LIKAANZA HAPO HAPO BARABARANI. KWANI KILA MTU AKATAKA KUWA MWEKA HAZINA. HADI TUNARUKA HEWANI MAFUNDI WA KAMPUNI HUSIKA WALIKUWA HAWAJAFIKA ENEO LA TUKIO NA VIJANA WAKAWA WANAENDELEA 'KUSAIDIA' MADEREVA.
HUYU NI RIPOTA WA GLOBU YA JAMII
EMMANUELLY MGONGO, KIBAHA
kufa kufaana...
waya za umeme zazuia njia
vijana 'wakisaidia' kunyayua waya
basi likipitishwa chini ya waya
msururu wa magari wamea
vijana wakiendelea kutoa 'msaada'
kwanza mapatano, 'msaada' baadae.....









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Duh! ilikuwa kazi risk sana kufanya, lakini sasa wafanyeje.

    ReplyDelete
  2. hapa ni kufa kufaana au siyo michu?

    ReplyDelete
  3. hii ndio tanzania hamna taratibu, hapa hawa watu hawakupaswa kuruhusiwa hata kidogo kufanya hiyo kazi ya kunyanyua waya, ni maalaka zuinazohusika tu ndo zilipaswa kufanya hiyo kazi. swala zima la usalama na uokoaji ni zero kabisa

    ReplyDelete
  4. That is risk....Duhhhhh masikini nchi yangu....Ni shilling ngapi walikua wanapata hapo jamani kurisk their lives hivyo......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...