wachezaji wa yanga wakiwa katika hoteli ya kitalii ya Hiliday Inn katikati ya jiji wakisubiri usafiri kuwapeleka mazoezini kujiandaa na pambano lao na watani wa jadi Simba SC mnamo April 11, 2010 ambapo wameahidi ushindi mnono kwa washabiki wao
basi la yanga lawasili Holiday Inn
wachezaji wakiingia kwenye basi Kocha wa Yanga Kostadin Papic 'Clinton' akiongoza msafara
basi la wachezaji likiondoka Holiday Inn

Wakati huo huo....
KLABU ya soka ya Simba imesema hivi sasa inaufikiria zaidi mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya Lengthens ya Zimbabwe, kuliko mechi ya Ligi Kuu dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga, ambao utafanyika Aprili 11, Dar es Salaam. Kupata habari hii kamili.

BOFYA HAPA
Libeneke la Yanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kumbe Yanga na Simba bado ni issue?

    ReplyDelete
  2. Soka la Bongo bwana!! Yanga na Simba tu basi ndiyo mwisho, miaka nenda miaka rudi hakuna cha zaidi. Fanyeni juhudi mfanikiwe kwenye anga za mechi za kimataifa. Yanga na Simba hakuna tija ya maana, hiyo itaishia Kariakoo tu pale.

    Check hii ya Yanga baadala ya kuweka timu kwenye kambi nzuri wakati ilipokuwa inajaandaa na Lupopo ya Congo wanaweka wakati wa Simba.

    ReplyDelete
  3. akili za yanga bwana wao wanaona muhimu kwa funga simba tu wakienda na majimaji wanafungwa

    ReplyDelete
  4. Timu zisizo na dira michezo ya kimataifa wanaipa umuhimu kidogo na wakishindwa visingizio kibao.

    Soka la bongo bwana, sasa na waamuzi hilo nao pambano wao watakuwa wamewaweka wapi??

    ReplyDelete
  5. SIMBA MSHAANZA KUONA WIVU, JEURI YA PESA HIYO.....

    ReplyDelete
  6. Wote hawa wachezaji si wanaishi hapo Dar? Wangekua wako nje ya mji na wakakaa hotelini ningeelewa lakini kuwaweka hapo wakati wote wana nyumba zao hapo hapo karibu naona kama kichwa maji vile. Hizo hela wangetumia kunufaisha maisha ya hao wachezaji. Either kuwasaidia kujenga au kujiendeleza kimasomo au something.

    ReplyDelete
  7. Yanga endelezeni soka la magazetini na globuni wakati Simba wanaendeleza soka la kitabuni.

    ReplyDelete
  8. SOKA LA USIMBA NA UYANGA NA LIGI ISIYOKUWA NA MIKIMIKI YA USHINDANI WA KUZIWEZESHA TIMU ZA TANZANIA KUMIHIMILI SOKA LA KIMAIFA NDIYO CHANZO CHA KIFO CHA SOKA LA TANZANIA.

    ReplyDelete
  9. kuliko kukaa holiday in, mgeweza kuiweka klabu yenu katika hali nzuri na yakisasa, wachezaji wakawa wanakaa klab kama inabidi, kuliko kukaa Hotel, ni kujitia gharama zisizo na faida, na kwa kweli ni ushamba ulio pita kiasi.

    ReplyDelete
  10. LIFE IS TOO SHORT... ENJOY!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...