MKUU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE DR. JOHN MAGOTTI (wa sita kushoto) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAFANYAKAZI BORA WA IDARA MBALIMBALI KUTOKA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA MWAKA 2010. WA KWANZA KUSHOTO NI MWENYEKITI WA RAAWU TAWI LA CHUO BW. JOSEPH BABILE NA WA PILI KULIA NI NAIBU MKUU WA CHUO BW. JACKSON MUSHI.

DR. JOHN MAGOTTI AKIMKABITHI BI DIANA ZAMBATAKSI HUNDI YA SHILINGI LAKI SITA (600,000/=), IKIWA NI ZAWADI YAKE BAADA YA KUIBUKA MFANYAKAZI BORA WA CHUO KWA MWAKA 2010.

DR. JOHN MAGOTTI (KATIKATI) AKIWA NA MFANYAKAZI BORA WA CHUO BI. DIANA ZAMBATAKSI (KULIA) NA MFANYAKAZI BORA MWENZA WAKE BI BERTHA LOSIOKI (KUSHOTO).


HABARI NA PICHA
NA EVELYNE MPASHA WA MNMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk. John Magotti, hii leo ametunuku vyeti pamoja na zawadi kwa wafanyakazi bora wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa mwaka 2010.

Katika hafla fupi iliyofanyika Chuoni hapo hii leo, Mkuu wa Chuo amemkabidhi bi Diana Zambataksi Cheti pamoja na hundi ya shilingi laki sita(600,000/=) kwa kuibuka mfanyakazi bora wa chuo.

Dk. Magotti pia alimkabidhi Cheti na hundi ya shilingi laki nne (400,000/=) bi Bertha Losioki kwa kuibuka mfanyakazi bora wa pili wa chuo. Aidha, wafanyakazi bora 6 kutoka idara za taaluma na utawala walitunukiwa vyeti vya utambuzi.

Katika hotuba yake fupi aliyoitoa wakati wa hafla hiyo, Dk. Magotti amewapongeza wafanyakazi bora na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu zilizopo na maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Menejiment ya Chuo ikiwa ni pamoja na Bodi ya Chuo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    Kina mama hoyeeeeee! hongereni sana kwa jitihada zenu, kweli kina mama mnaweza hata bila kuwezeshwa, hongereni na nawatakia kazi nzuri zaidi na zaidi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2010

    Mbona kwenye hiyo picha ya katikati kuna picha ya Uncle Ben au wenzetu wa chuo cha mwalimu Nyerere wao hawamtambui msanii wetu wa sasa??

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2010

    ndo chuo gani na kimejengwa lini na kiko wapi???kinatoa shahada gani

    yani na utanzania huu ndo nasikia hiki chuo leo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...