HABARI NA PICHA
NA EVELYNE MPASHA WA MNMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk. John Magotti, hii leo ametunuku vyeti pamoja na zawadi kwa wafanyakazi bora wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa mwaka 2010.
Katika hafla fupi iliyofanyika Chuoni hapo hii leo, Mkuu wa Chuo amemkabidhi bi Diana Zambataksi Cheti pamoja na hundi ya shilingi laki sita(600,000/=) kwa kuibuka mfanyakazi bora wa chuo.
Dk. Magotti pia alimkabidhi Cheti na hundi ya shilingi laki nne (400,000/=) bi Bertha Losioki kwa kuibuka mfanyakazi bora wa pili wa chuo. Aidha, wafanyakazi bora 6 kutoka idara za taaluma na utawala walitunukiwa vyeti vya utambuzi.
Katika hotuba yake fupi aliyoitoa wakati wa hafla hiyo, Dk. Magotti amewapongeza wafanyakazi bora na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu zilizopo na maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Menejiment ya Chuo ikiwa ni pamoja na Bodi ya Chuo.

Kina mama hoyeeeeee! hongereni sana kwa jitihada zenu, kweli kina mama mnaweza hata bila kuwezeshwa, hongereni na nawatakia kazi nzuri zaidi na zaidi.
ReplyDeleteMbona kwenye hiyo picha ya katikati kuna picha ya Uncle Ben au wenzetu wa chuo cha mwalimu Nyerere wao hawamtambui msanii wetu wa sasa??
ReplyDeletendo chuo gani na kimejengwa lini na kiko wapi???kinatoa shahada gani
ReplyDeleteyani na utanzania huu ndo nasikia hiki chuo leo