Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia bunge la jumuiya hiyo jijini Nairobi leo asubuhi.
Mwenyekiti wa jumuiya Ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia bunge la jumuiya hiyo jijini Nairobi leo asubuhi.Kushoto aliyeketi ni Spika wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Abdirahin Abdi.
Rais Jakaya Kikwete(Katikati) Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdirahin Abdi(kushoto) na Spika wa Bunge la Kenya Kenneth Marende(kulia) wakiwa katika viwanja vya Bunge la Kenya Muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili na kupigiwa wimbo wa taifa ambapo baadaye Rais Kikwete alilihutubia bunge la jumuiya hiyo.
Rais Mwai Kibaki wa Kenya akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Kikwete katika ikulu ya Nairobi ambapo viongozi hao wawili walifanya mazungumzo mafupi kabla ya Rais Kikwete kulihutubia bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...