Habari bwana Michuzi,
Pole sana na majukumju ya kila siku.naomba msaada tutani kaka katika hili,nina bwana mdogo wangu ambaye amemaliza kidato cha sita mwaka huu , tunapenda sana apate elimu yake ya juu katika nchi za Sweden ,Norway au Finland.
Mwenye taarifa zitakazotuwezesha kutimiza dhamira yetu hiyo basi tunaomba atusaidie ,tumejiandaa kwa mazingira yote ikiwemo scholarships na hata kujilipia.
Tutashukuru iwapo tutapata taarifa za colleges na Universities .
Natanguliza shukrani
Mdau katika Elimu
Kuna watu walitoa michango yao hapa:
ReplyDeletehttp://vijanafm.blogspot.com/2010/03/elimu-nje-ya-nchi-tuambie-hali-halisi.html
Kama una maswali usisite kuandika kwenye link hapo juu na wahusika watakusaidia.
Mi nasoma hapa sweden, kwa kweli sweden ni nchi nzuri na elimu yao ni nzuri japo ni ngumu ukilinganisha na ya bongo.Sweden elimu ilikuwa bure kwa miaka yote ya nyuma hata mimi nilibahatika kupata elimu hiyo ya bure,ila kuanzia mwaka kesho meaning wale wote watakaoingia kusoma mwakani watatakiwa kulipa school fees.Jingine ni kwamba kama ndugu yako anata kufanya first degree then atatakiwa kujifunza lugha yao kwani bachelor zote zinatolewa katika luga yao,isipokuwa masters ndio zinakuwa kwa english. website yao ni www.studera.nu. nakutakia kila la heri.
ReplyDeletenirahisitu kama una access ya Internate ukigoogle Universities katika nchi hiyo unayoitaka utapata ila nafikiri kwa Bechelor angetakiwa awe amesha apply.
ReplyDeletekwa sweden kunajinsi wanachagu google STUDERA then humo utapata maelekezo ila kwa sweden kuanzia mwakani wataanza kulipisha fee mana ilikua free mpaka mwaka huu kwa nchi nyingine za scandnavia i think bado itakua free
http://www.studyinsweden.se/
ReplyDeleteMIE NAKUSHAURI UENDE PALE UBALOZI WA NORWAY HUWA WANAKUWA NA SCHOLARSHIP ZA KUJA KUSOMA HUKU...AU AJARIBU KUAPPLY VYUO HUKU NORWAY..MDAU NORWAY
ReplyDeleteKwa nini usi-google tu na kuwaandikia emails kwa ajili ya clarifications? It's easier that way unless umpate mtu ambaye yupo chuoni. Ila kwa mtazamo wangu ni rahisi zaidi ku-google na ku-keep in touch nao (wanarespond fasta sana na thoroughly). Anyway, best of luck!
ReplyDeleteIshengoma.
ingia wavuti.com huwa wanapost hivyo vitu
ReplyDeletekaribu sana ndugu yetu.Ni vyema kuinvest pesa kwenye kumsomesha mdogo wenu, ni jambo la busara sana.Sasa walioko hizo nchi nyingine watakusaidia wanavyofahamu.Mimi niko Finland, kwa mwaka huu mmeshachelewa.Applications huwa zinaanza mwezi January mpaka February katikati.Majibu yakuitwa kwenye mtihani yanatoka March na mitihani mingi ni April na May.Shule zinaanza August,ofcourse kuna shule chache zinaanza January masomo,lakini ni chache na huwa ni risk kuja kipindi hiko maana ukikosa inakuwa kasheshe.Bora ukija kipindi ambako kuna shule nyingi unakimbizana nazo kukosa zote kwa kweli huwa sio rahisi sana labda kama uliondoka kwenu bila kumuaga bibi akakupa mkono wa kheri.
ReplyDeleteWengi huwa wanaomba degree na hata diploma, akikosa kabisa Degree basi anajishikiza diploma hata nusu mwaka au mwaka,huku akiendelea kuhangaikia kuapply degree, then unakuta anapata anaanza masomo rasmi sasa.Kwa maelezo zaidi soma www.cimo.fi (click sehemu wamendika Discover Finland) humo utapata maelezo mengi sana na hata kuangalia courses zilizopo.Sijui uwezo wenu lakini sisi akina "ahangaikaye" tunapendelea zaidi kuishi mji mkuu wa Helsinki au Tampere, ndio sehemu ambazo foreigners ni wengi na vibarua angalao vinapatikana so mtu anaweza akajimudu baada ya muda asihitaji tena msaada wenu.
Kama ukipenda maelezo zaidi, toa email au namba yako tuwasiliane.Nashuka Dar July ntakutafuta tuongee zaidi,maana kwa ufupi jamaa HAWATOI visa za kuja huku kufanya mitihani na shule zisizo na mitihani ni chache mnooo.So,sikuhizi kuingia kwenye hili "paradise" ni hadi uwe na mtu unamfahamu,otherwise labda uangalie UK na marekani ambako kwenyewe kwa maswala ya kwenda kusoma ni pesa yako tu.Naita paradise mana mi nilikotokea kwetu hali ni mbovu sana,ila kwa waliotoka kwenye hali yenye afadhali, alafu mtu labda mmezaliwa watatu au wanne tu kwenu na wote mmechangamka basi hapa sio pa kukaa unajisahau,ni unasoma then unatimua, au unakuwa unakaa unafanya mitkasi yako bongo huku unakuja kuzichanga tu na kupumzika malaria.Ila wakina sisi ndio tushafika hatuondoki hapa hata winter iwe mwaka mzima,sie poa tu.
Karibu sana.
NDUGU NJIA RAHISI NA YA UHAKIKA NI KUTUMIA YAHOO ITAKUPA SHULE ZOTE YA NCHI UNAZOTA HALAFU ITAKUJULISHA MUDA NA GHARAMA NA NJIA NYINGINE UKISHA PATA ANUANI KATIKA YAHOO YA SHULE UTAKAYO UNAWAANIKIA E-MAIL NA KUWAULIZA MASWALI YOTE UTAKAYO NA E-MAIL UNAPATA KATIKA SHEMU YA CONTACT.
ReplyDeleteAU NJIA NYINGINE TEMBELEA EMBASSY HAPO BONGO ZA NCHI UTAKAZO MAANA KILA EMBASSY MARA NYINGI WANAKUWA NA SEHEMU ZA ELIMU PIA. NAKAUOMBEA MFANIKIO WAKO NDUGU MOHAMMED TOKA DUBAI
NAKUTAKIA KILA LA KHERI
Sijui sababu zinazo mfanya atake kwenda kwenyehizo nchi ulizo zitaja, ila kama ni ushauri wangu ningemshauri pia afikirie kusoma Australia. sababu:-
ReplyDelete1)Vyuo vyao viko juu sana ki rank katika world accredited universities, mfano. ANU(Australian National University), Melbourne, University of sydney, university of new south wales, monash, maquarie uni, etc.
2)Gharama za maisha huku Australia ni rahisi sana ukilinganisha na nchi za ulaya,(so ata serve money into that)
3)Australia wanaongea kiingereza,kwahiyo itakuwa ni added advantage kuimarisha english yake,(as East african commercial language, in case akitaka kufanya kazi east africa baadae).
Hata hivyo vyuo vinatofautiana kutokana na faculty na faculty, so angesema anataka kusoma masomogani ili tumpe ushauri zaidi.
all the best,
Mdau Australia.
pop in in their respective balozi to get all the info you want
ReplyDeleteZuru tovuti mbalimbali za elimu ya juu(higher education / Universities)katika nchi husika kupitia google.
ReplyDeleteKwa kuanzia cut, paste & click mpini huu:
http://graduateschool.topuniversities.com/articles/scandinavia/study-european-north-destination-nordic-countries
Ngojeni kwanza jamani,kwanza tujue kapata ngapi then tuendelee?
ReplyDeleteushauri wangu ng'ng'ania huko huko sweden na finland,asikushauri mtu kijan huyo kumleta uk atakufa,mimi ni mwaka wa tano hapa nasoma ila ni ushuzi mtupu,shule bei mbaya sana na maisha yako juu mno,hata mimi niko njiani kuikacha hii nchi,uk sikushauri hata kidogo ila kama unataka watu wajue tu kwamba kijana yupo uk basi mlete ila matokeo yake atakuhadithia akikaa miezi 6 tu.asante ni hayo tu.
ReplyDeleteAs wadau wengine wa huku scandnavia walivyosema,application deadline ya Norway kwa kuanza shule August ni 1 dec for international students.hivyo kuanza this year umechelewa,halafu for first degree unahitaji kujua norsk as course zao zote zafundishwa kwa norsk.Except chuo kimoja ambacho ni private na very expensive wana programme wanayotumia English.Ni norwegian school of management,nao deadline ya application ni 15 april.just try to apply wana rolling adm system.But be prepared kudeposit kwenye account watakayokufungulia kiasi cha nok 140,000.you have to be fast visa takes up to 3months,be aware you must have passed English and mathematics minimum c and have your otefl results ready.Lykke til or Gooduck
ReplyDeleteUSHAURI WANGU KTK HILI
ReplyDeleteSasahivi nipo naandika kitabu kiitwacho SCHOLARSHIPS FOR INTERNATIONAL STUDENTS IN NORTH AMERICA AND WESTERN EUROPE: Secrete From Makulilo
Kitabu hiki kitatoa ufafanuzi wa mambo mengi mno, mojawapo ni kama suala hili lililopo mezani. Sasa ngoja nijibu hili na kuwa specific.
1. Katika kutaka kwenda kusoma shule ya Undergraduate ni lazima ujue ni nchi gani unataka kwenda kusoma. Hapa kitu cha kwanza cha kuangalia ktk nchi ni LUGHA MAMA itumikayo ktk nchi husika. Nchi zile ambazo English sio lugha yao mama na taifa kuanzia elimu ya vidudu hadi chuo kikuu upande wa bachelor's degree hufundishwa kwa lugha yao. Mfano Sweden wanatumia ki-swedish, Finland wao ni kifin, Ujerumani wao Kijeruman nk. Hivyo ukitaka kwenda huko itakubidi uingie gharama zingine za fedha na muda kusoma kwanza lugha na ufaulu mitihani ndio uweze kuanza shule ya degree ya kwanza sasa. Ila kwa nchi hizi masters na PhD zinafundishwa kwa English. Ni vyema kwenda kwenye nchi hizi baada ya kuwa na bachelor's degree
Ila ukienda ktk nchi ambazo lugha mama na taifa ni English huko wao mfumo wao na lugha ya kufundishia ni English kuanzia vidudu hadi chuo kikuu (bachelor's to PhD). Mfano wa nchi hizi ni USA, Canada (part of Canada), UK, Australia, New Zealand nk. Hivyo ushauri wangu ungeangalia shule ktk nchi hizi.
2. Kuhusu Undergraduate Scholarships.
Scholarships kwa ujumla huwa ni "vita" kwa maana ni watu wengi mno toka nchi mbalimbali wanaomba nao. Hivyo inabidi ujipange kuandaa application iliyoshiba kwa maana maswali yajibiwe kiufundi sana na kwa umakini ili kuleta ushawishi.
Scholarships kwa undergraduate huwa ni chache sana. Kwa mtazamo wangu, nadhani undergraduate sio "target" yao kama ilivyo kwa masters na phd. Na pia ukiangalia bachelor's degree mfano hapa USA ni 4 yrs wakati masters ni 1 or 2 yrs, sasa ni ubora wawalipie wanafunzi wawili wa masters kuliko mmoja wa undergraduate. Pia kwa vyuo vingi wanaamini watafaidika zaidi na mtu wa masters na phd kuliko wa undergraduate kwa maana kuwa teaching assistant, research assistant, paper presentation nk.
3. Vigezo na taratibu za kuomba vyuo
Kama unataka mtoto wako aje kusoma USA kuna vigezo vikubwa viwili kwanza. Vigezo hivyo ni ADMISSION TESTS. Kwa kuwa Tanzania lugha mama sio English, hivyo unalazimika kufanya mtihani unakupima uwezo wako wa english, yaani English Profiency Test. Hii iko mitihani ya aina mbili, moja ni wa Waingereza, International English Language Testing System (IELTS) unafanyikia British Council kwa ada ya shiliki laki 240. Au mtihani mwingine wa wamarekani Test of English as Foreign Language (TOEFL) huu unafanyikia University Computing Center at University of Dar (Mlimani Campusi) kwa ada ya dola 140. Hapo unatakiwa kufanya mtihani mmoja kati ya hiyo miwili. Nashauri mtu afanye huo wa IELTS kuliko TOEFL. Nina sababu nyingi, sipendi kuweka maelezo marefu hapa kwani itakuwa kuwachosha watu.
Mtihani mwingine ni SAT unaweza kufungua link hii kusoma SAT ni nini na inakuwaje http://en.wikipedia.org/wiki/SAT
Pia mtihani huu unafanyikia University Computing Center - UDSM kwa ada ya dola 140. Ni LAZIMA mtihani huu mtu afanye kwani hata wamarekani wenyewe ili waende chuo kufanya bachelor's degree ni lazima wafanye. Usipofanya, na shule hupati uwe unajilipia au ni scholarship.
Naamini maelezo hayo yatakuwa na msaada kwa kiasi fulani, japo nimeandika kwa haraka haraka, ubize wa michakato.
Nakutakia mafanikio mema ya mwanao kupata shule nzuri na ya uhakika
MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
www.scholarshipnetwork.ning.com
San Diego, CA
SCHOLARSHIP FOR UNDERGRADUATE DEGREE AT BEREA COLLEGE IN KENTUCKY, USA
ReplyDeleteFungua website hii http://www.berea.edu/prospectivestudents/ ni chuo kipo Marekani jimbo la Kentucky kinaitwa BEREA College.
Ikifunguka site hiyo nenda kwenye International Students ambayo link yake ni hii
http://www.berea.edu/prospectivestudents/international/default.asp
halafu anza kusoma hizo details za Applying for Admission, Download an Application the Cost and Financial Aid hizi zote ni kwa International Students.
Ukifungua hapa utasoma Scholarship ni 100% for 1st year then miaka ya mbeleni ndio unalipa just kiasi cha dola 1000 kwa mwaka ambacho ni kiasi kidogo sana kwakua utakua unafanya kazi ndani ya campus kwa masaa 20 kwa wiki lakini chuo kikifungwa utaweza kufanya kazi masaa mengi Off Campus. Fungua http://www.berea.edu/prospectivestudents/international/costsfinancialaid.asp
Angalia kozi hapo kwa kwenda kwenye Academic Majors and Minors http://www.berea.edu/prospectivestudents/academicsmajors/majorsminorsprograms.asp
Kama unaswali lolote niulize. Naamini hii ni golden chance kwako ndugu Mtanzania mwenzangu
NOTE: Kumbuka ni lazima ufanye mtihani wa TOEFL (iBT - Internet Based Test) at UCC - Mlimani chuo Kikuu au ufanye IELTS - pale Birtish Council. Na pia ni lazima ufanye SAT Exam pale UCC. Soma kwa makini details ni jinsi gani ya ku-apply then unapokua na swali waandikie na kuuliza chuoni ambapo e-mail yao ni askadmissions@berea.edu
Siku njema
MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
www.scholarshipnetwork.ning.com
San Diego, CA