na Mwandishi Wetu,
Dodoma
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Mbrazil, Rodrigo Stockler, amesema kwamba mashindano ya kombe la taifa, Kili Taifa Cup, yamewasaidia vijana wake kuongeza uzoefu wa kupambana na hivyo watakuwa katika hali nzuri zaidi katika mchezo wao wa kimataifa unaofuata.
Ngorongoro Heroes ambayo imesonga raundi ya pili kwa kucheza na Ivory Coast baadaye mwezi Julai, imealikwa kushiriki mashindano ya Kili Taifa Cup ili kuwapa mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya Afrika kwa vijana.
Akizungumza na Globu ya Jamii, Stockler, alisema kwamba wachezaji wake wameonyesha uwezo mkubwa wa kukabiliana na wachezaji wenye umri mkubwa na hivyo wameonyesha kwamba wako tayari na mashindano ya kimataifa.
"Mashindano yametusaidia sana, wachezaji wangu hawajaonyesha kwamba wao ni wadogo kwa kujitahidi kwenda sambamba na wachezaji wa mikoa mingine ambao ni wakubwa kiumri na uzoefu wa kucheza michuano mbalimbali," alisema kocha huyo.
Alisema kwamba mechi tatu ambazo timu yake imecheza zimewaongezea mbinu mbalimbali nyota wake ambazo zitawasaidia katika mchezo wao unaofuata dhidi ya vijana wenzao wa Ivory Coast watakaokutana nao baadaye mwezi Julai.
Aliongeza kuwa tatizo la uwanja limekuwa likiwasumbua nyota wake tofauti na viwanja vya Dar es Salaam ambavyo wamezoea kutumia katika mazoezi na mashindano mbalimbali ambayo wameshiriki.
Alisema pia waamuzi bado wamekuwa ni tatizo katika kuendeleza soka ambapo wameshindwa kuwalinda wachezaji wake kwa kuruhusu wafanyiwe madhambi yasiyo ya lazima.
Katika msimamo wa kituo cha Dodoma, Ngorongoro Herous iko katika nafasi ya tatu kutokana na kujikusanyia pointi mbili baada ya kutoka sare mara mbili wakati Kigoma yenyewe ndio inashika mkia ikiwa haina hata pointi moja.
Wenyeji Dodoma ndio wanaongoza kituo wakiwa na pointi nne sawa na Singida lakini Dodoma wakiwa na magoli matatu ya kufunga wakati Singida ikiwa na goli moja la kufunga.
Kwa kweli TFF wamefanya ubunifu mzuri sana katika hili ukizingatia matatizo ya kifedha tuliyo nayo. Ingawa sio sawa na kucheza mechi ya kimataifa lakini angalau timu imecheza mechi zenye ushindani dhidi ya 'vijeba'.
ReplyDeleteBig up TFF.
heruus + herous = Blog ya Jamii Oyeee!!!
ReplyDeletewebmaster acha ufisadi w fikra, baada ya kurekebisha maandishi uliokuwa umeyakosea, kama hukutaka kushukuru kureke japo basi usingepost komenti iliokuonyesha umekosea kwa kuandika neno moja mara mbili, ukiwa umelikosea mara zote mbili yaani 'heruus' na 'herous'
ReplyDelete