Dear Tanzanians,
I, as Tanzanian, am proud to have achieved another milestone... The Tanzanian Shilling is now equal to more than 1,400 to 1 US$!!!! Congratulations to all of us Tanzanians for:
1) Using Chinese toilet paper rather than Rexa or Tanpack...
2) Buying ice cream made in Kenya or South Africa rather than Azam
3) Using Omo rather than Foma
4) Eating Heinz baked beans rather than Dabaga or Red gold
5) Using Shoprite as your favourite shopping destination since "expired" South African goods are better than FRESH Tanzanian products
6) Using Anchor butter/cheese on your bread rather than ASAS or AZAM
7) Using Colgate and CloseUp as they make your teeth brighter rather than Whitedent
8) For drinking Heineken and Red Bull rather than a good old Kili....its a matter of image in it!
9) For drinking St.Anne, Namaqua and Overmeer than Dodoma wine
10) For using Farmer's choice sausages than Beef Vienna from Arusha
11) For using Kangaroo matches than KIBO match
12) and the list goes on...
Come on guys WAKE UP!
It’s time for a change
BE TANZANIAN BUY TANZANIAN!
And a request to the expatriate community...especially South Africans... please change your mind set and help Tanzania grow by supporting local products...
Pass it on to all Tanzanians.
BE POSITIVE & THINK POSITIVE
Mungu Ibariki Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2010

    ni sawa lakini nyingi hazina ubora na hazina mvuto wajaribu kuboresha vitu kwani wao waweze wana nini hata sisi tushindwe tuna nini? toilet paper zetu ni aibu manake ni ngumu kama karatasi halafu hazina hata sehemu ya kukata hadi mpambane ukiwa hayo maeneo ya starehe vibiriti vingine ni njiti tupu havina viwashio yani ni full kero na pia nilishakuta kizibo cha soda chenye kutu kwenye soda ya fanta wakati nainywa mtu alikitafuna kikapinda akadumbukiza ndani nilipoona hicho kisoda nilichukia sana na kususa mlo yaani kero ni nyingi sana kwenye bidhaa zetu kwenye chupa za bia mende condom watu washakumbana na uchafu huo acha tuu bidhaa zetu zinatakiwa ziwe na ubora. mr supu huu ni ukweli na uwazi meseji hii ifike ili wahusika waone kero zao

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2010

    who is allowing all those foreign products you have mentioned to enter the country?? Then if you know him or her he or she is the cause of the problem.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2010

    Dah ni juzi tu nilikua nawaza haya mambo, yanauma sana kwa mzalendo yeyote jinsi watu tulivyokua malimbukeni wavitu vya nje na kusahau na kudharau vya kwetu..
    Tumegeuzwa dampo kwa kila kitu mpaka vitunguu saumu na hata tangawizi toka upare hatutaki tena, twataka vya china.

    ukinywa bia zetu machoni mwa watu unaonekana wa kawaida sana, ila ikiwa umeshika chupa ya bia ya kutoka nje wewe ni bonge la mjanja..na utapata sifa kedekede..

    jamani tunakwenda wapi...? shukurani mdau kwa kuleta mada hii...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2010

    We imagine out of Tanzania borders is more beautiful than inside here!!
    Great Shame!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2010

    Najua upo udhaifu wa ubora nyakati nyingine, lakini hatuwezi epuka ukweli kwamba kamwe hatuwezi inua viwanda vyetu kama hatutobadili tabia na kuanza kutumia bidhaa za kitanzania, naunga mkono hoja na tubadilike!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2010

    Hongera sana mdau kwa kutukumbusha kwamba kutukuza vya watu ni ushamba!!! watu tubadilike na kuwa wazalendo na akili zetu pia, utaona mtu hata akisimulia tu anataka aonekane anatumia vya nje zaidi ya vya kwao

    Na huu ujumbe pia ungefika vizuri zaidi kama tungetumia lugha yetu ya taifa basi. Mabadiliko yaanzie nyumbani!!!!!!!

    Duh tunasafari ndefu au hatujaanza kabisa sijui tunahitaji tume iundwe au SIRIKALI maana wadau hawakawii, serikali ikataze vitu vyote kutoka nje!!!!! teh teh!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2010

    FOR USING ENGLISH LANGUAGE RATHER THAN SWAHILI!!!!!

    MDAU NAKUBALIANA NA WEWE KWA KIASI FULANI. LAKINI, HAPA INGEBIDI UANDIKE KWA KISWAHILI. ASILIMIA KUBWA YA WATEJA WA BIDHAA ULIZOOROZESHA HAPO NI WASWAHILI HIVYO WANGEKUELEWA VIZURI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2010

    Soko uria manake ni kuweza kushindana kwa ubora. Sasa kama wewe unataka kununua bidhaa ambazo hazina ubora kwa kuwa ni za Kitanzania basi hatufiki mdau. Kimsingi kama mdau mmoja alivyosema ni kuwa na bidhaa bora ambazo siyo tu zinaweza kuuzwa ndani ya nchi bali zinaweza kuuzwa na nje ya nchi pia. Bidhaa nyingine aibu tupu inabidi ziuzwe tu nchini au nje ya nchi kimagendo. Soko uria jamani watu wafungue macho bidhaa za Tanzania zenye ubora sawa, lakini bila ubora nakataa nitatumia za nje. Tatizo wababaishaji wengi... Uzalendo na malengo vinginevyo tungekuwa tunafuata ujamaa mpaka leo? Si ndio wadau...

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2010

    Jamaa uliyemwandikia Michuzi
    Nakuomba ubonyeze kile kidude kinacholeta REWIND turudi mwanzo wa stori yetu, Stop ukifika,One English pound is equal to twenty Tanzanian shillings
    I appreciate and I am concerned with events, but you are not telling us the answers
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2010

    Nawewe uliyeleta hii mada ni mtumwa wa kutumia vitu vya nje.. Angalia sasa umetumia lugha ya nje badala ya lugha yetu adhimu KISWAHILI. By the way naunga mkono hoja. Inauma sana kuona mtu ananunua machungwa ya South Africa wakati yetu yanaozea sokoni. Nawasilisha. Nagira - A Town.

    ReplyDelete
  11. gpublicstrategies.blogspot.comMay 26, 2010

    its okey but to some extent you are not fully informed the wine you called overmeer in actually produced in Tanzania using grapes from Dodoma by Tanzania Distilleries Ltd.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2010

    13. Kutumia Kiingereza na kubeza lugha yetu wenyewe

    BE TANZANIAN, USE TANZANIAN!

    Naanzia na mtoa mada.

    Tatizo ukienda madukani wanakuambia "imeisha, hadi tuagize tena" kana kwamba hawakuwa wakiona inapungua.

    ReplyDelete
  13. Yaaani kati ya mada ambazo huwa zinaletwa kwa michuzi ili ziwe discussed, ya leo IMEENDA SHULE. MDAU ULIYELETA HII MADA UANDIKE NA JINA LAKO NIKUPE OFA YA KIBUKU.

    Mtu ukiongea kingereza unaonekana bonge la mtu na mtu anapotaka kuongea kiswahili lazima aombe msamaha kwanza "sio kwamba sijui kingereza ila ..." ila nini? kwani kujua ngeli ndo nini?

    Ni kweli kwamba kuzuia vitu sasa itakuwa ngumu kutokana na mikataba ya kimataifa tuliyoingia na kwasasa kwakweli hakuna jinsi lakini tunajinsi ya kuvidharau vya nje na kula vya ndani.

    Mimi mdau hapa niko ulaya yaani hata vyakula wanavyoleta wachina na wazungu ni vya maabara si original. Kweli jamani tunashindwa kwenda kununua vitu sokoni kariakoo tunaenda shoprite kununua nyanya.!!! AIBU JUU YETU

    Pia, mnajua kwamba mazao haya mbegu zinatoka katika maabara na wanatumia makorokoro kibao yakuleta kansa. Hivi mnadhani kwanini siku hizi kuna kansa nyingi? Mazao yetu yanaozea mashambani alafu tunasema eti kuna njaa? AIBU JUU YETU.

    AIBU, AIBU, AIBU AIBU.

    Basi tuelimishane sijui tuwe na wizara ya bidhaa za ndani yaanni sijui.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 26, 2010

    Ninakubaliana na anon Wed May 26, 03:49:00 PM. Tuko kwenye ulimwengu wa "International Business and Marketing". Ndio maana nchi zenye uzalendo mkali kama Marekani bado wananunua magari kutoka Japan na Europe. Kwa nini?. Mteja sasa hivi ana uamuzi (choice) na bidhaa za nyumbani lazima zinyanyue kiwango ili ziweze kushindana na za njee. Toilet paper kama Rexa inayeyuka mkononi..haina ubora. Sisemi kila kitu ni kuhusu ubora. Mfano, sidhaani Kili inaweza kushindana na Heineken kwa matangazo (Champion's League nk) kwa hiyo ni bora Heineken wawekewe kodi (tariffs) za juu zaidi kuliko Kili ili kulinda soko la nyumbani. Ni swala kubwa,
    (Mr. X)

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 26, 2010

    Kuna sabuni ya dettol nilinunua shoprite inasema 5% ya pesa zitokanazo na ununuzi wa hiyo sabuni itasaidia kulea watoto wenye HIV South Africa. Nikafurahi kusaidia watoto wa Africa lakini nikajiuliza kwa nini hizo pesa zisisaidie na watoto wetu wa Tanzania wapo wengi mayatima walioathirika?

    Kingine ni kuwa sio kweli kuwa bidhaa zetu zote ni hafifu. Mfano, vitunguu vya hapa home ni tamu na vinanukia kuliko vya shoprite toka South Africa sema wanunuzi hawajui kama hivyo vitunguu sio vya nyumbani. Muwe makini mkienda idara ya mboga na matunda kuuliza haswa machungwa, vitunguu, mbatata za urojo, vitunguu thwaumu, maharage....nk... nyingi za kutoka bondeni ni ladha mbaya na za hapa home ni tamu kuliko.... Be Tanzanian Buy Tanzanian.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 26, 2010

    Tuwe watanzania wazalendo bana! Mwanaume wa kitanzania oa mtanzania, na mdada wa kitz olewa na mtz! Tehtehtehteh!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 26, 2010

    Mdau umewahi kutumia Rexa au unasema tu? Kutumia Rexa ni kama kutumia vidole tu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 26, 2010

    Kipindi kifupi kilichopita kwenye hii blog niliona picha ya (mkuu wa mkoa wa dar/meya; sinauhakika ni kiongozi gani exactly wa mkoa wa dar) akimkabidhi rahisi Kikwete zawadi ya jezi ya mchezaji wa mpira wa nchi za nje. Pichani rahisi alionekama mwenye furaha kwa kukabidhiwa jezi hio. Ikiwa viongozi wenyewe wa serekali yetu hawajui umuhimu wa kudhamini vya kwetu wenyewe unadhani itakuwaje. Mimi binafsi niliona ki kitendo cha kishezi mnooo. Kama zawadi ilikuwa lazima iwe jezi kwanini isiwe jezi ya mchezaji bora wa simba/yanga n.k.
    Nilisha ona pia hizi bendi zetu kama twanga pepeta kwa mfano... kundi zima wamefaa fulana zina bendera ya Jamaica.... what the hell is that. I watched that video nikiwa Canada... imagine kama mtu mwingine ambaye si mtanzania akiangalia upuuzi ule, am sure atadhani bendi ya twanga pepeta ni Jamaican Band.
    Angalia watu wakikaaga nje mwaka mmoja tu anarudi bongo hajui tena kiswahili... anazungumza kiswahili cha tabuuuu. Mungu wangu; ni ulimbukeni wa kiasi gani huu jamani
    Well, I am sad; I think tuanza na kuwa-proud kwamba sisi ni watazania. Tuipende nchi yetu, tudumishe utamaduni wetu... tutumie bidhaa zetu..

    Asante

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 26, 2010

    mnawasema hao wachina na wasouth africa amkeni wamewaona mmelala ndio maana washukuruni sana kwanza kwa kuja kuwekeza kweye nchi kama hii angalau mmejua hata supermarket zinafananaje,ndio maana siku hizi mkija ulaya mnajifanya mnajua kila kitu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 26, 2010

    Wabongo bado mbumbumbu kuwa mavyakula nje kuwa si healthy. yana mikemikali ya kumwaga. Usishangae kuona mi-kansa na mi-unene umeanza kujikita Bongo. Vyakula vya nyumbania asilia ni Organic na very healthy. Hapa marekani watu hawawezi kumudu chakula organic- na kula organic ni ujiko mkubwa hapa.
    Pili- serikali imetokomeza kabisa ujenzi wa uzalendo. ndo maana hata vijana nyumbani hivi sasa wanavyaa suruari mitepecho (chini ya matako) kuiga mila ilotoka kwa wafungwa weusi wa Hapa majuu, waloifanya kuwabinulia matako walinzi wa magereza.
    Wakorea, wachina, wamarekani, wajerumani n,k. woote wana uzalendo mkubwa wa vitu vyao. Well, aliye na macho haambiwi tazama.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 26, 2010

    Why would i care about local products, and you, the advocate don't even care to use our own swahili language?

    Why would I care to consume Tanzanian Products while the very producers don't care about the consumers?

    Why would i care to be a Tanzanian while the government and fellow citizens don't even care about their own people and colleagues?

    Upumbafu wetu umetufikisha hapa!! Mungu Ibariki nchi yetu ya daraja la tatu na produce zetu zilizopo daraja hilo hilo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 26, 2010

    Mnasema kiandikwe kiswahili wakati watu wengine wanaandika kikwao 'soko uria' maana yake nini? Kasheshe kweli kweli.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 26, 2010

    MHESHIMIWA WA ARTICAL HII UMEWAKUNA WENGI..LAKINI HILI SWALA LINADHARAULIWA. NA HII YOTE KUTOKUWA NA DIGNITY HAMNA LINGINE...HUWA NAJIULIZA KWANINI MTU ALE MAVYAKULA YA MAKOPO TANZANIA AACHE FRESH..JIBU MOJA NI KUWA AMEKOSA UPEO WAKUJUWA.NA SASA TUSISHANGAE KUWA NA WATOTO MACHIZI ...KWASABABU BIDHAA NYINGI ZINA CONTAIN MADAWA TUKUBALI AU TUKATAE. NI MAMBO MENGI YAPO YA SARAFU ZETU KUSHUKA SIO HILO PEKEE.

    ReplyDelete
  24. Mtoto wa CoastMay 26, 2010

    Wakati wa kubadilika ni sasa, ..inaendelea.

    14. Kuweza kuvaa jezi za Inter, Liverpool, Arsenal, ManU na kuweza kuwataja kwa majina yote mawili wachezaji wa hizo timu kwa ufasaha na maisha yao na kukariri ligi zao zote na point walizonazo lakini hajui hata mchezaji mmoja wa African Lyon, Manyema, Azam FC, wala ratiba ya ligi zetu au za Kombe la Kagame n.k

    15. Kumsifia Bibi wa Kwanza wa US kwa mavazi yake na anavyotembelea Taasisi mbalimbali lakini ukamponda wa kwenu na kuuliza hivi yeye ni nani katika Serikali?

    16. Kusifia na kusikiliza kila wakati nyimbo kama Young Money World- Wayne na uko tayari kulipa hata 30,000 kiingilio kumwona akija hapa kuliko Mwana wa Dar - ASSET au hata Nikipata Nauli - Mpoto na hauko tayari hata kulipa 5,000 tu kwa ajili ya onesho lao la kujituma na linalogusa nyoyo na maisha yetu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 26, 2010

    Je umewahi kusikia kisa cha
    The kettle calling the pot black?
    Kuna ndugu yangu asema kuwa jamaa wakaa nje kwa muda mfupi na wakirudi huwa wana matatizo na lugha ya bongo.Namkumbusha kuwa yeye pia kakaa Canada kwa muda gani, sijui, lakini yeye pia anaanza kusahau kiswahili. Nimehisabu manenno katika barua yake,takriban, kuna maneno ishirini ya kingereza kwenye jamvi la maneno mia moja na sabini ya kiswahili

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 26, 2010

    13) kutumia lugha ya kiengereza badala ya lugha yako kiswahili.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 27, 2010

    Nyumba na Bidhaa nyingine za kila zinapangishwa na kuuzwa kwa Dola badala ya Shillingi basi si tubadilishe tuu helayetu iwe Dola ? Nenda Kenya tuu uone kama wanafanya UPUUZI HUU.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 27, 2010

    ukiwa na jambo la kuwaeleza watanzania inabidi uandike kwa lugha ya taifa yaani kiswahili,unalalamika watu wanakumbatia vitu vya ugenini na kuacha vya nyumbani,wewe ni wa kwanza kukumbatia vya wenzio kiingeraza sio lugha yako kwanini uwaeleze watanzania kwa kiingereza,punda wewe

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 27, 2010

    ikiwa mnataka ukweli ni lazima tujuwe kwa nini tumefika hapa na nani katufikisha hapa, bila ya ukweli tutazidi kupotea,si kiuchumi hata kimawazo,ikiwa uchumi ulikuwa mzuri wakati fulani,je?ilikuwaje? na hata bidhaa zilikuwa na ubora, je ilikuwaje?,historia ya tanzania ni ya uongo,viongozi ni waongo na wananchi wengi ni waongo pia,kwanza tuanzie hapo.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 27, 2010

    ikiwa mnataka ukweli ni lazima tujuwe kwa nini tumefika hapa na nani katufikisha hapa, bila ya ukweli tutazidi kupotea,si kiuchumi hata kimawazo,ikiwa uchumi ulikuwa mzuri wakati fulani,je?ilikuwaje? na hata bidhaa zilikuwa na ubora, je ilikuwaje?,historia ya tanzania ni ya uongo,viongozi ni waongo na wananchi wengi ni waongo pia,kwanza tuanzie hapo.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 27, 2010

    kwa mnaosema hadi quality ibadilike hampo sahihi, tunaanza na low kwenda high, tuvitumie huku tunatoa maoni yetu na kufatilia kuwa marekebisho yanafanywa, huwezi kuanzia angani tu leo uwe na bidhaa 100% bora, tuwe na kipindi kifupi cha mpito, najua tunaweza, pia serikali iache ukiritimba wa kuondoa kodi kwa wageni, ukienda shoprite beer 1300 na chupa yake, kwa akili ya kawada tu mtu unajikuta unaenda kule, serikali nayo inachangia kudumaza vitu yetu vya uzawa! nakutanaga na wakubwa wa govt na matoroli nao wamenunua nyanya shoprite etc

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 27, 2010

    iweje sasa??

    kiswahili chenyewe kinatoweka sasa?

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 27, 2010

    Hi michuzi,
    Jana nimetoa comment yangu kuusiana na buy Tanzania product na WTO,AGOA,SADC lakini nashangaa umebana. Ni ndefu na ni ya fact lakin umebana sijui kwanini?

    Tafhali isome na uiruhusu haina nia mbaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...