SAFARI SIYO KIFO
BENDI ya Muziki ya dansi ya Akudo Impact Wanapekecha Pekesha Ijumaa ya Julai 9 itafanya utambulisho rasmi wa Albamu mpya na utambulisho wa wanenguaji wake wapya utakafanyika kwenye Ukumbi wa Polisi Jamii Uliopo Dodoma .
Mratibu wa onesho hilo hilo Zahor Said, amesema kuwa onesho hilo pia litakuwa na utambulisho wa albamu inayotwa 'History No Change', pamoja na wanenguaji wapya ambao wametoka nchini Congo .
Said alisema kuwa onesho hilo maalum litaaanza saa 2 usiku nia ni kuwapa burudani wapenzi wa mkoa wa dodoma na vitongoji vyake.
“Tumejipanga kutoa burudani siku hiyo maalum ya utambulisho Akudo itafanya vitu vya uhakika itatoa vionjo vya wanenguaji wapya ambao Akudo imewachukuwa kutoka Congo ,”alisema Said.
Said alisema katika utambulisho huo kutakuwa na burudani nyingine mbili ambazo zitasindikiza usiku huo ambapo mazungumzo na bendi hizo yanaendelea.
Baadhi ya nyimbo za albamu hiyo ni Ndoa, Umefulia na Ubinafsi na inayobeba albamu hiyo History No Change.



HII BULOGU NI YA WATU WENYE NAZO TU HASA WALE WALIOSOME MUZUMBE CHUO KIKUU CHA UNIVESITY CHA KULE MOLOGOLO. SASA WADAU WAKUU WA HII JAMVINI NI
ReplyDeleteJOHN MASHAKA
RIDHIWANI KIKWETE
JACK PEMBA
PAULO KAMAU (ANAKUJA NA BRIFIKESI)
SISI WAKULIMA HATA KAMA TUMESOMA MUZUMBE LAKINI HATUKUBALIKI KWA MAANA HATUNA DAU. NI WENYE DAU TU, AMBAYO SIYO VIZURI.ANAKL HATA SISI HATUNA DAU ILA ITAKUWA VIZURI UKIWEKA NYIMBO ZETU, TUMEIMBWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA MUZUUMBE
Kweli sasa wadau tumetambua kuwa Globu ya Jamii pia ni PRESS CONFERENCE YA JAMII a.k.a Speakers'corner(go to public speaking history www.speakerscorner.net ya London's Hyde Park), wadau hiki ni kiwanja chetu.
ReplyDeleteMdau
Honolulu, Visiwani Pasifiki.