JK akimpa kiungo hodari wa Brazil Kaka zawadi ya kinyago baada ya gemu na Taifa Stars
JK akiwapungia mkono wadau wanaomshangilia kwa nguvu baada ya gemu
Mtangazaji mashuhuri wa Zenji Faroukh Karim akisalimiana na Kaka


paparazzi wetu
Paparazzi wao...
Data za gemu la jana





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2010

    Kubali usikubali Brazil ni wazuri na wanafanya vizuri kutokana na defence yao imara, Lucio, Maicon, Dan, Viungo Kaka, Robinho,na wengine mnawajua.

    Kwa hiyo basi Ugumu uliopo kuwafunga Brazil goli moja na timu kama yetu...ni sawa na urahisi wa wao kutufunga sisi Mabao 5.

    Kutokana na statistics za Gemu kama ulivyozitoa, na ukuchukulia possession does not necessariry mean ushindi...na kipa alikuwa si mbongo....basi ngoma ni Droo au vipi washikaji?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2010

    Haya vikamera vya waandishi wa Bongo ni vya kupigia ndani ya kiji-hall cha mnuso.

    Angalieni wenzenu wana-zoom hadi mita 1000.

    Ankal itabidi globu ya jamii i-'up-grade' camera zake kuonyesha kuwa sisi tunaongoza wengine wanafuata.

    Asante kwa kutuhabarisha maana huku Honolulu Hawaii ngoma inachezwa sisi tupo kazi na ni saa nne asubuhi, tulikuwa tunaibia kwa jamu up-dates za gemu toka globu ya jamii.

    Mdau
    Honolulu, Visiwani Pasifiki Ocean.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2010

    Nimezipenda sana zile picha zinazo waonyesha Paparazzi wetu na Paparazzi wao. Wakati mapaparazzi wao wako bize wanaseti vifaa vya kazi mapaparazzi wetu wako nje wanapiga story.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2010

    UTAKUTA HZ DATA HAKUNA MTANZANIA YOYOTE ALIEWEZA KUZIPATA, MAANA INAONYESHA HIZI ZIMETENGENEZWA/ZIMEFANYWA NA WATU WA NJE!.BONGO BWANA. GAME ICHEZWE KWETU ANALYSIS HATUWEZI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2010

    Attendece hairizishi kabisa Wangefanya majukwaa mwengine £5,500-£10,000 uwanja ungejaa mpaka basi Tanzania tungekuwa tumerudisha kama $3m-4m hivi Utalii gani mabango matangazo ya Tanzania ni Serengeti Bia na Bank ya hapahapa tumejitangazia Labda Serengeti Bia. Sijaona Tangazo la Website Labda utalii na vyakula? Tanzania tumejiangusha kweli kupoteza pesa Hizo zilizopatikana sijui zitaenda wapi? Juma Seif.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2010

    STATISTIC FEKI HIZO
    YONDANI KAPEWA KADI YA NJANO

    ReplyDelete
  7. Du tumepigwa mabao kotekote kuanzia uwanjani hadi kwa mapaparazi tukamera hatuonekani kwa mapaparazi wetu sijui kwa udodo au wamezificha?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2010

    mapaparazi wao wamekamilika,mikamera hito zoom hata upo maili mia kinakuvuta,wetu dah,tuko mbali sana,labda wangeazima ya mkuu wa wilaya ya nanihii.

    ReplyDelete
  9. Ingawaje tumepigwa ubaya,stats zinaonyesha kama vile tunaujua.Kufungwa tumefungwa lakini tuliweka mguu na timu bora duniani.Ndiyo machache yangu.LOL

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2010

    lol ! hadi mdau hawaii kweli dunia ndogo natamani kweli kufika honolulu. poa mdau boksi jema
    vancouver canada

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 08, 2010

    yani hao paparazi wetu michosho kweli angalia hata bodi langweji yao ya kichovuu utadhani hawapo mzigoni chekini wenzenu mikamera ya kuzoom udaku wa ukweli sio hivyo vikamera mdoli mmebeba maji ukiyavulia nguo huna budui kuyaoga.HISANI: wanabloug ya jamii woote popote duniani hadi huko honolulu tumeni japo dola moja moja kwenye akaunti ya ankal ili naye apate likitu la uhakika kama hao mapaparazi wauzunguni unavuta kitu level 8 kempisk wakti uko kwenye feri si mchezo! haya misupu achilia namba za akaunti tuanze kazi

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 08, 2010

    Takwimu zinaonyesha kipa wa Tanzania alikuwa likizo wakati Gomes anakuwa nyota wa mchezo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 08, 2010

    Kanuni za elimination ni kuwa ukitaka kufanya kusiwe na msongamano wa watu na kuwe na usalama wa kutosha unaweka kiingilio kikubwa basi. Sidhani kama shida ilikuwa kujaza uwanja ingetokea fujo hapo na idadi ya askari tulionao tungewabeba kwa mbeleko gani wabrazil. Sisi waswahili tumezoe kufanya analysis za kujazana watu mahali ndio mafanikio ya kitu. Kiusalama na ukizingatia muda mfupi uliopo kabla ya kombe la dunia kuanza kwa wabrazili hiyo ilikuwa ni mechi ya mazoezi the fewer watazamaji the better!

    Eti kiingilio elfu 5, wee ujaze uwanja ili iweje? Halafu waswahili bado wanaishi kiujamaa ni kijima kila kitu chao, eti tungerudisha kiasi kadhaa, mpaka sasa hamjui ni kiasi gani kimetumika, na kiasi gani kimepatikana kutokana na matangazo na viingilio na hamtakaa mjue kwa sababu hizo ni biashara za watu binafsi!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 08, 2010

    Kwa kweli Mujomba Kamau alisema kweli. Sasa Bodi Langweji ya hawa ma paparazi wetu imekaaje. Wanaonekana wamechoka sasa sijui wamechoka kimaisha au kitaaluma hapo sijaelewa!

    Kwani hata kuingia ndani ya uwanja walizuiliwa nini?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2010

    wabongo hatuna zawadi zaidi ya vinyago???

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 09, 2010

    ankal jaribu kufuatilia hili shem yangu alikwenda kata ticket ya 30000 kuona gemu kaambiwa zimekwisha zote lakina kulikuwa na vijana kibao waziuza mkononi kwa 70000 je kuna watu wenye pesa walinunua kwa wingi ili wapate faida kubwa? na kama ni kweli kwanini tff imuuzie mtu mmoja ticket kwa wingi inawezekana uwanja mzima ticket zilinununliwa ila kwa wachache wanaotaka utajili wa haraka wameharibu kilakitu tunaomba uwaulize tff kama kweli ticket zilikwisha asante mdau hoston texas

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 09, 2010

    Namuona mdau Ridhiwani Kikwete karibu na baba...mwana kama baba...kua mdau uje uongoze nchi vizuri kama baba yako.
    mdau DC

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 09, 2010

    Duuu! Hi kali.... yaani tumewalipa bilioni 3, matangazo yaliyo kuwa uwanjani ya kwao na zawadi tunawapa. Tutafika kweli!!!??... Kweli aliye nacho huongezewa.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 09, 2010

    Naomba kuuliza, kinyago alipewa Kaka tuu au na wengine walipewa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...