wadau wenye data msaada tutani tafadhali...
Asalaam alaykum Ankal
Mechi ilipigwa mjini Dar uwanja wa uhuru kama sikosei 1972.
Wanaoonekana Pichani ni Rais wa Zamani wa Sudan ambaye alikuwa mgeni wa heshima Gaffar El Nimeir akisalimiana na wachezaji wa taifa stars, Kutoka kushoto ni Mohamed Chuma , Omar Zimbwe ,Kitwana Manara,anayeonekana Kichwa ni Shaaban Baraza ,Kapteni Kibadeni.Kilichotokea siku hiyo timu zote zilikuja na jezi zinazo fanana na refarii wa Mechi hiyo Manyoto Ndimbo akawaamuru wenyeji wavue jezi zao Huku Mwalimu akishuhudia tukio hilo.
Prof. Mrisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2010

    mgeni rasmi ni rais wa zamani wa sudan bwana gaffar nimeiri,wa mwisho kushoto ni chuma,na anaefuatana na mgeni rasmi ni abdulrahman juma hicho ni kikosi cha kwala jangwani miaka hiyo au wana yanga wanga wa wakati huo katika soka.
    yanga oye usa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2010

    Du kaka..na netboli ilikuwa hivyo?
    Mdau Mbije,Andendekisye

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2010

    wooow...
    Yaani this was the REAL TAIFA stars. Nakumbuka waliichapa timu ya Brazil ya vijana twice when the Brazilian team made African tour,(this was NOT that match, I think this was against Egypt?) Sikumbuki pia ilikuwa ni mwaka gani. Lakini it was the only team that did so.

    Mechi ya jana ilikuwa mzaha mtupu. What a shame, kwa kweli vijana wetu just can't get it together. The Taifa stars now is probably one of the worst teams I've ever seen, and mark you Coach Maximo amefanya kazi kweeeli kuwafikisha kiwango walichonacho sasa.

    Nawaona hapo Boy Wickens, Omar Zimbwe, Kitwana Manara na Capt. someone Juma, sorry first name limenitoka. Mgeni wa heshima simkumbuki.
    Man those were the days!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2010

    Tukio hili lilitokea baada ya rangi za jezi za Tanzania na Sudan kufanana, ilibidi timu mwenyeji kuvua jezi. tukio hili sio lilomfanya Nyerere kuacha kwenda mpirani tena. Tukio lililomfanya Nyerere kuacha kwenda mpirani tena ni la mechi kati ya Tanzania na Ethiopia ambapo ngumi zilipigwa, Nyerere akasema "nimemekuja mpirani kuangalia mpira sio ngumi na kuanzia leo sitokuja tena mpirani".

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2010

    na aibu iliyomkuta jana JK wimbo wa taifa kugomagoma kuimba,naye ataacha kuja uwanjani?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2010

    kumbe jamani tumetoka mbali sana,umenikumbusha baada ya azimio la arusha, ambapo kila mtu upepo ulimfikia, hakuna aliyenusurika si mkulima.mfanyakazi,mfanyabiashara wala watoto naam baada ya dhiki imekuja faraja.tuko katika neema mungu abariki na azidishe ziwafikie hata majirani

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2010

    toka shoto Chuma, Omar Zimbwe,Capt. Abdulrahman Juma, Mgeni Rasmi , na King Kibaden

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2010

    Mwalimu Nyerere was never a sports fan. It was just a flimsy excuse.

    ReplyDelete
  9. Ankal,
    Pichani ni Mgeni Rasmi Aliekuwa Rais wa Sudan Jaafar Nimeiry na anatambulishwa na Kepteni wa Tanzania Abdulrahman Juma.
    Toka kushoto ni Chuma, Omar Zimbwe, Kitwana Manara na anaeonekana kichwa kwa nyuma ni Kibadeni.
    Kisa cha Wachezaji kuwa tumbo wazi ni Viongozi kutoihudumia Timu ikiwa Kambini hata Wachezaji wakalazimika kuja Uwanjani kwa Miguu [kambi yao ilikuwa jirani tu Jeshi la Wokovu] na hakupelekewa hata Jezi kambini.
    Mechi hiyo tuliifunga Timu ya Taifa ya Sudan bao 3-0.
    Storming
    Mdau wa www.uksokainbongo.blogspot.com & www.sokainbongo.com

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2010

    Kweli huu ulikuwa ni ujima. Watu matumbo wazi au labda niseme vifua wazi?

    Sasa Badala ya kuwatafutia Jezi mwalimu akasema harudi tena!!!! Wachezaji walikuwa wanatembea na mguu kwenda kucheza mechi!!!!!

    Mungu tuepushe na umaskini wa kiwango hicho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...