Na Zawadi Msalla na Jovina Bujulu
-
MAELEZO DODOMA.

JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania lipo katika mchakato wa kubadilisha mfumo wa utoaji leseni za udereva kwa kuanza kutoa leseni za elektroniki.

Hayo yameelezwa leo Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Masha, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2010/2011.

Waziri Masha alisema lengo la mpango huo ni kuhakikisha kumbukumbu za madereva kote nchini zinawekwa kwa usahihi hivyo kupunguza ukiukwaji wa sheria barabarani na utoaji holela wa leseni bandia nchini.

Masha alisema mpango huo utatekelezwa katika awamu mbalimbali ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka2010 katika vituo tisa vya Arusha,Kilimanjaro,Tanga,Mbeya,Dodoma, Mwanza,Ilala Temeke na Kinondoni.

Masha alisema katika mabadiliko hayo leseni zitaongezeka kutoka aina nane zilizopo sasa na kufikia kumi na nne na zitakuwa na fursa ya kuweka kumbukumbu zote muhimu zinazotakiwa na kuongeza kuwa leseni hizo hazitakuwa rahisi kughushika.


Aidha Waziri alisema zoezi hilo litaenda sanjari na uhakiki wa leseni za udereva za daraja C ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wizara ya Miundombinu na Mamlaka ya Mapato litaanza zoezi la kuhakiki umiliki wa leseni za udereva daraja la C kwa lengo la kubaki na wamiliki wale tu wenye sababu za msingi za umiliki wa leseni hizo.

Alisema kwamba wapo wananchi wengi wanaomiliki leseni hizo kinyume na taratibu na sheria za barabarani kwani leseni hiyo ya udereva inaruhusu uendeshaji wa magari aina zote na pikipiki yakiwemo mabasi ya abiria.

Masha aliongeza watakao onekana hawana sababu za msingi za kumiliki aina hiyo ya leseni watapatiwa leseni ya udereva daraja B au D.

Waziri aliwaasa madereva kote nchini kuzingatia sheria za barabarani ili kupunguza idadi ya ajali za barabarani zinazoendelea kuzidi siku hadi siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2010

    GOOD IDEA IF ONLY THEY WILL GIVE PRACTICAL TEST TO DETERMINE THEY ARE CAPABLE OF BEING LET LOOSE ON THE ROAD.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2010

    IMHO hii ni nzuri. Tunapoteza vingi na wengi kutakana na madereva feki. Labda sasa watu watathamini Leseni zao na kuogopa kuzipoteza kwa ulevi na fujo.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2010

    WAGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHADMEA 2010

    DR. US BLOGGER
    JOHN MASHAKA
    JANUARY MAKAMBA
    MR. SUGU
    NAAKAYA SUMARI
    ZITTO KABWE
    JOHN MYINKA
    MANGE KIMAMBE
    LADY JAYDEE
    ISSA MICHUZI

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2010

    Hili ni jambo zuri sana. Hata hivyo tatizo si kughushi leseni bali ni kutoa leseni kwa wale wasiostahili (la sivyo sijui maana halisi ya kughushi). Hata hivyo suala la kutoghushika kwa hizo leseni lisitolewe kipaumbele ktk kutetea umuhimu wa kuwa na aina mpya ya leseni kwani hata wakati noti mpya zinatolewa tulipewa hadithi kama hizi na sasa kila mtu anajua kinachoendelea. Tunazisubiri kwa hamu.

    www.kapongola.wordpress.com

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2010

    Qualification za kupata hizo leseni mpya ni zipi? kutakua na test? Practical na theoretical na kupimwa macho au as long unayo ya zamani basi unapewa mpya hata kama ya zamani uliipata bila kufanya test yeyote...

    ReplyDelete
  6. Mpalang'ombeJune 27, 2010

    Mimi bado ninalia na KUWASHIRIKISHA TRAFFIC katika mchakato mzima wa utoaji leseni. Inatakiwa kuwa na kitengo ndani ya Wizara ya mambo ya ndani, ambacho kitakuwa linked na TRA kijulikane kama "Tanzania Driving and Vehicles Licence Authority (TDVLA)"
    Kazi yake iwe ni

    1. Kutoa electronic provisional licence(Learner) ambayo itakuwa ndiyo Identy ya kufanyia computer based theory test, mtu akipass anapewa practical test, mtu akipass vyote viwili anapewa leseni kamili ya daraja aliloomba.

    2. Kutoa usajili wa magari kwa kuoanisha na watakaokuwa wanaendesha magari hayo, yaani Driver na gari, kama litaendeshwa ni mtu zaidi ya mmoja wajulikane ni kina nani, ili polisi wanapoona gari wakiingiza namba kwenye king'amuzi wanajua dereva wake ni nani.

    3. Kazi ya Traffic police iwe ni kusimamia sheria barabarani na kurekodi makosa ambayo yakithibitishwa mtu anafungiwa leseni kwa maana hiyo gari lake halitakuwa barabarani, mpaka aweke bima ya mtu mwingine kuendesha.


    Polisi ndiyo waliotufikisha hapa tulipo kwa kuchukua laki moja moja na kutoa leseni kama njugu, walitakiwa sasa hivi wawe ni wasimamizi tu wa sheria za barabarani suala la nani anajua kuendesha na amejibu maswali vizuri ya theory iachiwe authority hiyo tu. Tukifanya hivyo tutajua wa kumkamaata ni nani pindi leseni za badia zipoonekana mitaani. Tatizo wanaoongoza hivi vyombo ni watu wa zamani sana hawana future vision zaidi ya kuhakikisha wanachokijua ni hichohicho basi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2010

    Ni mtoto wa kigogo gani aliyerudi nyumbani hivi karibuni kutoka ngambo ambae amekuja na idea hii ili kujipatia mtaji wa haraka haraka? tutaona ni nani atapewa tenda hii.

    Idea hii ilikuwepo miaka tele lakini haikutimizwa kwa sababu waliotowa wazo si watu wanaojulikana.

    ReplyDelete
  8. Haya ni mawazo mazuri, lakini kwa utamaduni wetu mambo mengi mazuri hayatekelezeki, people are not serious.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...