nani kasema ankal hatomboki tomboki. hapa ni kwenye mnuso wa kumeremeta mdau jackson wa nanihii. Ngoma iliyokuwa inapigwa ni sebene la "samaki ana vipande vingapiiiiii...., vitatuuuu, hebu taja - kichwa, tumbo na mukia......" halafu kingoma kinachang'anya. Acha!
ankal tino (kulia) naye hajambo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2010

    Kiswahili cha siku hizi yani hadi homa,jaribu kutamka hilo neno hatomboki tomboki mbele ya mkweo siunaishia sema matusi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2010

    HAhahahahaa safi sana hii Ankal kweli palikua hapatoshi burudani saafi.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2010

    Hongera Ankal kwa suti ya nguvu sio kila kukicha fulanazz, neno TOMBOKATOMBOKA naona unalianzisha liwe lugha ya mtaani halijakaa vizuri!!tafuta neno jingine wewe ni Mkuu wa wilaya ya Ukerewe sio fresh

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2010

    Nina hamu sana na kutomboka tomboka ila nanihii yupo nanihii sasa hivi...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2010

    ankaaaaaaaaaaaal hongera kwa kutomboka ,i like u when u dont wear that weird fulana u look mwaaaa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2010

    Duh! hii lugha yetu mwisho wa siku tataishia kutukanana. Tomboka?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2010

    sina hamu na ankali mwezenu!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 13, 2010

    Kutomboka maana yake ni nini?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 13, 2010

    Ladies mmependeza...My sis Try..is that not you!..You look STUNNING..FABULOUS as USUAL..Hahah!
    Ossamah

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 13, 2010

    Jamani maharusi wa siku hizi wame-data si mchezo.sasa ndo nini KUTOMBOKA KOTE bwana harusi.No wonder ndo hazidumu.
    Anyway,best of luck.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 13, 2010

    Jamani Ankal hicho kiswahili ni cha wapi!!! Uwiiiii

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 13, 2010

    Old is GOLD Michuzi. Kumbe na wewe wamo!!!!! Congrats

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 13, 2010

    Ninavyofahamu mimi kutomboka ni kilingala likiwa na maana ya kufoka au kumkaripie mtu ama kumkoromea kwa lugha ya siku hizi,kwa hiyo hapo bwana michuzi alikuwa anamkoromea huyo aliyekuwa anajifanya kucheza nae.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 13, 2010

    Hicho kiswahili au kilugha? kama ndio unaanza neno jipya achana nalo halina mantiki wala mvuto wewe ni mtu mzima.TOMBOKA!!!

    ReplyDelete
  15. kaka angalia sana sehemu fulani ulimi au kalamu isije ikateleza ukaweka herufi "e" badala ya "o".

    Itakuwa noma mtu wangu! Ohoo!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 13, 2010

    ankal anacheza kiduku anaweza huyoo

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 13, 2010

    Tigo tupu hapo...Namuona Tino...Devi...wengine nimeasahau...Long tyme...


    Mdau wa tigo ya zamani

    ReplyDelete
  18. Hadj le SouvereeJuly 13, 2010

    MUONGOZO:

    KUTOMBOKA JAMANI MKIKONGO NI KUONGEA KWA STYLE YA KUROPOKA WALA SI KUCHEZA RHUMBA AMA SEBENE,BUT U CAN SAY KWA KISWAHILI YA LUBUMBASHI,MANYEMA PRO AMA BUKAVU "YULE BWANA NI NINI?NJO VILE ANATOMBOKA MANENO MINGI SAWA VILE MUSODAA ANAFUNGULIA MASASI"

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 13, 2010

    Duh hilo neno co wala nini naogopa hata kulirudia

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 13, 2010

    Kutomboka ni neno linatumika Bukoba, yaani mkiwa wengi mwatomboka, mmoja yatomboka ni kutembea kwa madaa, msitake kubadiri maneno na maana zetu zingine, kwahiyo hii ni lugha ya kibantu, ambayo inaweza kutumika kama kiswahili kama maneno mengine ya kihaya yanavyotumika katika kiswahili mfano kibuga hili maana yake ni uwanja wa mbele ya nyumba.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 13, 2010

    mtoto anatombokt sana huyu yaani mtoto anaropoka sana

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 13, 2010

    Kwa wanaomshambulia ankal, kutomboka ni neno la kawaida si matusi kama mnavyodhania...mmarekani lugha ambayo anaanza kuongea after kuzaliwa ni English but hata akifika miaka 70, kuna maneno mengine mengi tu, hajui maana yake.
    mdau,
    USA

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 13, 2010

    hahahahahaahahahaahaaahahah! ncheka sana miye leo. Usite ncheke zaidi.. yatosha hasa

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 13, 2010

    wajameni kama kaka zetu wanakata mbuno kamamadada sijuwi inakuwaje wakati wetu tulivyokuwa vijana nunafurahiya kuona midondogo ya kina mama asii kweli bongo shule vijana samahanini yaelekeya ushoga unakunyemeleeni chungeni sana

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 13, 2010

    ni kikundi gani kilikuwa kinatombosha tombosha?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 14, 2010

    neno kutomboka sio geni kwa sisi wengine nahakika wengi wanaotoka au asili ya Manyema wanalifahamu hilo marehemu bibi yangu jina lake ukiniulza silitambui mpaka leo kwani zamani hukati majina unaita bibi tuu mama Jalala au bibi mama fulani na alikua akilitumia neno kutomboka ilikua ukileta jeuri anasema juu ya nini ukomukutomboka na kama mdau mwingine ana sema Bukoba nao wanaolo neno hilo hivyo sio geni

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 14, 2010

    Misupu aliona misosi tu hana lolote ,,,

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 14, 2010

    Michuzi eeh whats your email, nataka nikutumie mjadala!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 14, 2010

    naipenda hiyo picha ya kwanza. napenda michuzi unavyotishia.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 14, 2010

    Kwa wale mliouliza nini maana ya kutomboka. Kwa hapa Tanzania lina maana ya kudansi. Acheni hizo maana za lilikotoka. Hapa limepewa umaarufu na wasanii wa "Ze Comedy" ambao wamekuwa wakilitumia kwa maana ya "kucheza muziki wa dansi au wa bolingo" na ndivyo limeshazoeleka hivyo.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 14, 2010

    "Papa Michuzi, the International Bloglist, Na Kati ya Tegeta, Nambari One!", we acha tu Umetomboka ile mbaya,na hiyo elengi elengi ya Samaki! mimi naomba hiyo picha ya kwanza iingie kwenye kumi bora za mwaka, ambayo sisi wadau tutapigia kura

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...