Mbunge wa Jimbo la Kwela Dkt Christant Mzindakaya(kushoto) akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini Mh. Paul Kimiti wakielekea katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha thelathini cha mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge wote hao wameshatangaza kutowania tena nafasi hizo baada ya kutumikia kwa muda mrefu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Sophia Simba (kushoto) akibadlishana mawazo na Mbunge wa Kuteuliwa (CCM) Zakia Meghji(kulia) leo nje ya ukumbi wa Bunge la Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu cha kikao cha thelathini cha mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mbunge wa Jimbo la Kwela Dkt Christant Mzindakaya (kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Profesa Jumanne Maghembe(kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Lediana Mng’ong’o (kulia) akijadiliana jambo Mbunge wa Kuteuliwa (CCM)Mchungaji Getrude Rwakatare (kushoto) wakati wanaelekea kuhudhuria kikao cha thelathini cha mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Bungeni Dodoma leo
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF )Emmanuel Humba (kushoto) akijadiliana na Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkulo(katikati) na Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe(kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2010

    Hayo maji ya natakiwa vijijini!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2010

    I HAVE HEARD OF PAUL KIMITI AND MZINDAKAYA SINCE I WAS AT KINDERGATEN/VIDUDU UNTIL NOW! AMAZING! AND I AM 52 YEARS OLD NOW MIND YOU! THESE GUYS HAVE DONE A GREAT DEAL FOR THIS COUNTRY, ONCE I ADMIRED KIMITI WHEN I WAS A SECONDARY SCHOOL, HE WAS HITTING A GROUND RUNNING, HE USED TO BE NYERERE'S FOLK, NYERERE LOVED HIM SO DEARLY

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2010

    Anon wa Fri Jul 16, 12:46:00 AM:

    Tanzania ilianza zamani...!

    ReplyDelete
  4. Je kutoka kwa wabunge wa chadema bungeni inatujenga nini hapo baadae

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...