Wadau wakiwa wamepozi ili kupata picha za ukumbusho kuhusiana na mfululizo wa filamu ya ‘Sex in the city 2’ iliyokuwa ikiooneshwa rasmi nchini kwa mara ya kwanza.
Baadhi ya waalikwa wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa sinema wa Century kabla ya filamu hiyo kuanza kuoneshwa rasmi.
Baadhi ya wadau walioalikwa kuhudhuria uzinduzi rasmi wa mfululizo wa filamu ya ‘Sex in the City 2’ iliyotengenezwa Marekani na Abu Dhabi, Dubai wakipita kwenye pinki kapeti kuingia kwenye ukumbi wa sinema wa Century uliopo Mlimani City kuhudhuria hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wanausalama ‘Bouncers’ hawakuchezea mbali eneo la tukio kuhakikisha usalama kwa wageni waalikwa unakuwepo wakati wote watakaokuwepo katika eneo hilo la ukumbi wa sinema wa Century.
Wadau wakiwa wamepozi kwa kupata picha za ukumbusho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2010

    Why by invitation only? Exclusivity zingine hazina mpango mbona New York walipozindua Sex and The City 2 ilikuwa wazi kwa kila mtu anayeweza kununua tiketi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2010

    Nnavyojua hawakuruhusiwa ku-act Abudhabi waliambiwa that film is too sexy for the city (Abudhabi) na scene zao nyingi walichukulia Morocco sijui Tunisia lakini si Abudhabi!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2010

    picha ya pili kulia black dress, ASHURA umekuwa mama la nguvu.kweli tumezeeka.
    CLASSMATE WA PRIMARY.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2010

    hizo suti za wa beba vyuma haziwaki motot kweli !!lol

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2010

    Not filmed in Abu Dhabi!The scene depicting Abu Dhabi is actually Morocco. The movie does not comply with the culture identity of the United Arab Emirates (capital Abu Dhabi) thus its also banned from theaters etc.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2010

    Bongo kama Mbele....!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2010

    kaka michu hawa The Agency ndo nani tena bongo ?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2010

    why invitees only...! wabongo tunajua sana kugawa watu. kila jambo ni invitees tu halafu invitees ni hao hao siku zote! no new faces! kwani ingekua open to everyone with money ingekuaje? acheni ubaguzi.

    ReplyDelete
  9. UkweliuongoshauriyakoJuly 12, 2010

    Hii film ya sex in the city, nashangaa inapigiwa matarumbeta hivyo, sababu kama umewai kutazama series zake, basi utajua haiendelezi wanawake zaidi ya kusifia ufuska wa wanawake. Inasifia mwanamke kuwa fuska kwa kutembea na wanaume kadhaa, wanawake waliooelewa ni rahisi kuanza kuiga tabia chafu cha hawa ma actresses wa hiyo film.
    Lakini kama kawaida yetu bongo, sie tunaiga vitu bila kujali kama vitatu athiri, sie tumo tu, hata kama hii film ni inahusika na ufuska na sio fundisho kwa wanawake kuwa maendeleo sie hatujali.
    Kweli bongo soko la uchafu na ufuska!

    ReplyDelete
  10. Hii film haina mafundisho yoyote ya maana kwa wasichana wetu walio single, zaidi ya kuwahimiza kutembea na wanaume wengi bila ya kujali wanando au la.
    Kuna film nyingi tu zina mafundisho ya kumkomboa mwanamke toka kwenye umaskini lakini sio hii. Inakuza umalaya na ufuska.
    Wenye wake wajihadhari sana na hii film maana itaotesha mbegu za kutembea nje bila kujali madhara yake.
    Kama kweli walengwa wameangalia hizi series za sex in the city, watakumbuka kuwa ma actresses wao ni shopping, sex, sex na kutembea nje ya ndoa basi.
    Kwanini bongo lazima tunapenda kuiga mambo kutoka nje bila kuwa waangalifu.
    Sasa mtabisha na kubisha, ila kila mwanaume ajihadhari na mke au partner wake baada ya kutazama hii film, kama mnabisha mtaona!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 12, 2010

    middle age crisis for ladies who are over 40 years of age.

    Aim is to explore something they missed in their 20s,30s, so goodluck to you all.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 12, 2010

    BAADHI YA WADAU WANAENDELEA KUONESHA MSIMAMO KWA KUUTETEA UTAMADUNI WA KITANZANIA WA KUUPIGIA MAYOWE UFUSKA.
    LAKINI KWA HAPA TULIPO TENA ITASAIDIA NINI?
    MBONA JAMII IMESHAZAMA KATIKA LAANA ZA SHETANI NA KUKUMBATIA UKAHABA, USAGAJI, USHOGA NA NGONO ZEMBE?
    HII FILAMU NI MOJA TU YA KICHOCHEO NA KIHIMIZO CHA UKAHABA NA JAMII YOTE YA USHETANI WA KUPINDUKIA AMBAO TANZANIA YA SASA IMEGUBIKWA NAVYO.
    TUNAYO NA MENGINE, AMBAYO KILA KUKICHA YANAPAMBA MOTO NA KUFUIMBIWA MACHO NA MPAKA VIONGOZI WA SIASA NA JAMII. TUNALO HILI BALAA LA MAMISS AMBALO NDILO ZAO KUU LA UKAHABA NA UASHERATI, SI TU NI MAPOROMOKO YA ITIKADI, BALI NI MTEGO HATARI WA KUNASIA BINTI ZETU.
    KUNA HII MIZIKI YA KIITWACHO KIZAZI KIPYA, UKISIKIA SKENDO ZA WANAMUZIKI WAKE NI HUO UFUSKA NA UKAHABA TU, HAKUNA MANUFAA YOYOTE YA MAANA KWA JAMII YA MTANZANIA!!
    JAMII INATEKETEA, NA INATEKETEA KWA KASI SANA.
    LAKINI NANI ANAJALI?
    ZI WAPI TAKWIMU ZA UKIMWI?
    HAZITOLEWI TENA SASA, SABABU ZITAREJESHA NYUMA JUHUDI ZA WAASHERATI NA MAKAHABA.
    HUKU ULAYA NA MAREKANI KUNA KILIO CHA WATOTO KUKOSA MAADILI, NA MOJA YA SABABU NI BROKEN FAMILIES, YAANI WATOTO WALIOKOSA WAZAZI WAWILI NYUMBANI. NJOONI MWONE MPATE KUSHANGAA, JINSI WORKING CLASS INAVOONGEZEKA NA JINSI MIMBA ZA UNDER 15 ZINAVYOTAWALA! NA MATOKEO YAKE NI KUKOSEKANA ADABU NA MAADILI, KINACHOWASAIDIA NI UTAJIRI NA NGUVU KAZI ILIYOPEVUKA, HIVYO HAWANA WASI WASI WA KUKOSA WA KUWAFANYIA KAZI.
    HATA BALAA LA UKIMWI KWAO SI BIG DEAL, WANA MADAWA YA KUTOSHA KUPUNGUZA KAZI YA VIJIDUDU, LISHE YAO NI BAB KUBWA NA MARADHI YA MAAMBUKIZI NI KIDOGO SANA.
    SASA SIE WAMATUMBI HUKO TUNAJITAHIDI KWA NGUVU ZOTE KUIGA MACHAFU YA HUKU, NI HATARI NA MAANGAMIZI MAKUBWA SANA.
    TUSUBIRI KUKIONA CHA MTEMA KUNI!!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 12, 2010

    Na hii walioitengeneza mara hii ndio imeitwa the death of sex and the city movies like if she didn't get it from the first one...bad bad bad movie....Ingawaje wanasema audience wake wengi ni wanawake lakini hata wanawake wameamka anavyoportrait mwanamke kwenye moviez zao sio halali kabisa...Na wanawake wameamka ndio maana haikumae money kabisa.....kama hujaiona you don't miss anything

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 13, 2010

    Hi Michuzi unavyotayarisha hizi news huwa unapotosha lugha kwa makusudi? Hii filamu inaitwa "sex in the City 2" or "Sex and the City 2". Before I thought you were referring to another movie. Heshimu lugha tafadhali. Hata kama utabania comment yangu ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 13, 2010

    Picha hizi zimepelekea niseme: Ulaya na USA watu wenye uwezo ni wembamba (si sana) na watu 'maskini' ndio wanene. Afrika matajiri ni wanene na maskini ni wembamba. Funzo? : Wenye uwezo Afrika hawana mwamko wa afya nzuri - ukiondoa wachache sana. Praise.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...