Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Dr.Barnabas Mtokambali akimkabidhi JK hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni kumi(10m/) kama mchango wa kanisa hilo kwa ajili ya kununulia mashuka ya wagonjwa kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano Mkuu wa Kanisa hilo uliofanyika chuo Kikuu Dodoma ambapo JK alikuwa mgeni rasmi,JK alikabidhi mchango huo kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhandisi Dr.James Nsekela.
akiwa ameshika bendera ya taifa pamoja na Maaskofu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God wakati wa sala maalumu ya kuiombea amani na ustawi Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa kanisa hilo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana.Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo.
akiwahutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God katika ukumbi wa Chimwaga chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God wakionyoosha mikono wakati wa sala maalumu ya kuiombea amani na ustawi Tanzania wakati wa mkutano mkuu wa kanisa hilo uliofanyika katika chuo kikuu cha Dodoma leo mchana.
(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2010

    Hivi Maandiko matakatifu yanatuelezaje interms of namna ya kutoa sadaka? Je yanatueleza tutoe sadaka huku tukipiga picha na kutumia mic --- ama kivingine?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2010

    WOW! This is great. Kumbe Tanzania ina madhehebu mengi ya kikristo ambayo yako organized lakini hayatambuliki na kupewa sauti na serikali. Serikali inaijua Roman Catholic, Anglican, Lutheran na Moravian zaidi. Kwenye vipindi rasmi vya dini katika vyombo vya habari vya serikali, katika hafla za kiserikali wanazohitajika viongozi wa dini, wanaopelekewa mialiko rasmi ni hao wa madhehebu niliyoyataja tu. Kwa ujumla ni kwamba kuna madhehebu mengi makubwa ya kikristo hayatambuliwi na hayapewi nafasi inayostahili na serikali kama hayo niliyoyataja. Sijui kwanini serikali imekuwa na ubaguzi. Kikwete ameonyesha njia. Congulatulations Bishop Mtokambali and TAG. Mungu aendelee kuwatumia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2010

    mdau wa pili,mimi napingana na kauli yako kuwa serikali ni baguzi,but ukweli ni kwamba madhehebu ulitaja kuwa yanapendelewa ndo madhehebu yenye huduma za jamii nyingi hapa nchini kama taasisi za elimu,afya, vituo vya wajane na yatima n.k, sasa basi kunapokuwa na hafla mbali2 za kijamii zinazoendeshwa na hizo taasisi za dini mara nyingi huomba uwepo wa serikali kwani ndiyo inayoongoza nchi hii,kwa hiyo basi uwepo wa serikali kny shughuli za hayo madhebu siyo kupendelewa but mchango wake wa kijamii kwa serikali, NDO MAANA HAPO PIA JK KAALIKWA SI UNAONA WATOA MSAADA WA MASHUKA, BASI KAZANENI KUCHANGAMKA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2010

    anony Thu Jul 15, 09:17:00 PM kwa hakika umenena.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2010

    Kwanini Msahada usitolewe kwa walengwa ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...