Ankal na Wadau samahani,
Jana kijiweni kwetu hapa Magomeni kwa Macheni nusuru tutoane ngeu baada ya kuzuka ubishi mkali kwamba huu mtindo mpya wa uchazaji muziku ujulikanao kama 'kiduku' kaanzisha Mzee Yusuf na bendi yake ya taarabu ya Jahazi. Leo jioni tunakutana tena kijiweni na kila mmoja wetu kaambiwa afanye rishachi na kurudi na jibu. Mie mpaka saa hizi kapa, nikaona isiwe taabu. Globu ya Jamii itanisaidia. Kwa hiyo wadau naomba msaada tutani.
MARLOW KWENYE WIMBO WA PIPIIIII NDO MWANZILISHI
ReplyDeleteShenzi type, ndo maana mimi bongo sirudi acha boxi liniuwe.Badala ya kutafuta kazi yakufanya and get busy unaongelea mambo ya vijiwe.
ReplyDeleteMdau washington, dc
what i know is aliyeanzisha KIDUKU ni MORLOW na wimbo wake wa "PIPI"
ReplyDeleteNeema wa Sinza
yaani nyie watu wazima mnakaa kubisha upuuzi huo na mbaya zaidi unapoteza muda zaidi kuja kwa michuzi kudhihirisha upuuzi wenu. dont u have something better to do? idiot.
ReplyDeleteMuanzilishi wa hiyo staili SI mzee yusuph kwani ukiangalia ile video ya BLICK & LACE kwenye ule wimbo wa "my love is wicked" wale stage show walicheza hiyo staili sasa ni kwamba mzee yusuph kaiga wala si staili yake
ReplyDeleteAcheni ushamba nyie. Kiduku kimeanzia mitaa ya Temeke kwenye shughuli za vibeseni, vigodoro, na kutoa mwali.
ReplyDeleteWakati huo mademu wa Temeke wakija hapo Hotel Travertine na kujiachia kwa staili ya kiduku kwenye show za rusha roho watu wengine walikuwa wanashangaa tu kwamba hii ndio staili gani.
Jamani kuna mada zingine hazina kichwa wala miguu. Ukimjua mwanzilishi kutakuwa na tija gain? Wabongo kazi kubishana kwenye maada zisizo na manufaa yoyote hadi mnashidwa kuhoji viongozi tuliyowachagua wametufanyia nini etc. No wonder nilikuta kwenye bar moja pale masaki karibu na kilima watanzania wakibishana nani mtu tajiri zaidi Tanzania for like 2 hours. Kaeni na watu wa-nchi zingine uone mijadala yao hata wakiwa wanapiga kilaji..Shame..
ReplyDeleteBradha!
ReplyDeleteKweli Bongo tambarare. Yaani watu wazima mnakaa kubishanaia nani kaanzisha Kiduku, badala ya kukaa na kubishana mambo ya maendeleo kama nani kavumbua simu za mkononi au gari nk.! Khaah!
Kweli ndo mana hatuendlei na tukaitwa dunia ya tatu.
Mweeh!
nenda kafanye kazi! Kujua kituku sijui kinini kaanzisha nani haitakusaidia, na badala ya kufanyia research mambo ya muhimu unapoteza muda wako kufikiria kiduku. Itafaa hapo kijiweni mtafute mbinu bora za kuikomboa jamii, kama ninyi wenyewe mmeshajikomboa kutoka kwenye lindi la umasikini.
ReplyDeletekiduku hakijaanzishwa na mzee yusufu (the self acclaimed king of taarab).
ReplyDeletekiduku kimeanzishwa na watoto wadogo wa kinondoni walipocheza shoo kwenye uzinduzi wa kikosi mawe.
Kiduku ni nini kwani? nashindwa kuchangia.
ReplyDeletekiduku ni cha zamani sana hata bi kiroboto alikuwa anacheza kwenye kipindi cha mizengwe
ReplyDeleteDaah bro Michu yaani nashangaa huyu mdau kuambiwa anapoteza muda hapa eti kisa kuuliza asili ya kiduku. Anaambiwa ajadili mambo ya maendeleo!!. Mi sina tatizo nao lakini pia sioni ndugu kuwa kijiweni kuwa ni kutokufanya kazi za maendeleo. Kijiwe ni sehemu ya kujichanganyana na kupata sitori. Kosa lake hapa nini. Hapa hajaeleza ni kijana wa kijiwe A-Z. Tumpe jibu na kama hakuna tuulizane hayo ya nani katengeneza simu au magari tuone kama yatatusaidia bila kufanya tathimini ya tatizo letu ni lipi. Tatizo si kijiwe, kufanya kazi wala kujua aliyetengeneza simu; tatizo ni sisi wenyewe(hatujitambui), namna tunavyotafsiri na kutatua matatizo yetu. Period.
ReplyDeleteHiyo Kiduku Ni Jina Lenu La Kibongo Lakini Jinsi Inavyochezwa ni TECHNO MALEWA COMPLETE ambayo muanzilishi ni NOEL NGIAMA MAKANDA WERRASON.
ReplyDeletePrince Sab - Werrasonique.
Nyie wote mnaokandia hii topic ndio mnamatatizo, mimi sio tatizo la swali la hapo juu, kila kitu kina mwanzilishiwake au chanzo,kiduku ni staili inayo furahisha umunapo mtu anacheza, hata mimi ningependa jua nani alivumbua, nadhani hata mike jack alikuwa anacheza kiduku kiana....
ReplyDeletehivi nyie madikteta mnafanya nini kwenye hii blogu? mnataka kupangia mpaka watu wawaze nini, wajadili nini na wafanye utafiti wa nini? aliyewakataza nyie kufanya kazi 24/7, kufanya utafifiti wa simu/magari, nk ni nani?
ReplyDeletemtoa mada, nimefurahia swali lako nami nafuatilia mno mjadala huu.
hivi watu wengine mnakuwa hamna la kufanya?mkisha kunywa supu ya utumbo mnaenda vijiweni na kujadiliana utumbo?na mawazo yenu utumbo
ReplyDeletewadau, wote sie ni watu wazima, tafadhali hizi mada zisizokuwa na mbele wala nyuma zisitishwe mara moja... huu ukumbi ni wa kujulishana matukio ya muhim na ya maana sio ili mradi kulijaza libeneke tu kwa uchafu kama huu.. kwa mwendo hii hatutoendelea kamwe.. huo ubishi wenu wa mitaani untaka kuueleta mbele ya ma-elfu ya watu wanaopitia libeneke hili ili kuonesha jinsi gani akili zako hazichaji au inakuwaje??? tubadilike wadau...
ReplyDeletewe anonymous wapili baada ya mohamed, akili zako na huyo aliyeuliza wote sawa... ndo nyinyi muliyokosa kazi zakufanya muhimu na kufatilia upuuzi... ndomana wa tz tutaishia kua wapumbavu kila kukicha kwa hali hii tuliyokua nayo... tumia ubongo wako kwa mambo ya maana na sio kujua nani aliyeanzisha kidiku sijui nn, mara nani tajiri... mutaishia kutaja watu tu huku munakula vyakula kwa bahati mbaya!... shenz type!
ReplyDeletehahahaa kwa kweli comment zenu zimenifurahsha sn lakini ngoja niseme nilichokisikia na mm au kujua ni kwamba kiduku kimeanzishwa na marlow na wimbo wake wa Pipiiii
ReplyDeleteMarimar L
Mimi ningefurahishwa na kijueholic kama angekua anafanya research yake kuandika kitabu cha kumbukumbu za sijui hii kiduku ni dance style au ni nini, anyway kama imekubalika kwenye society ni vizuri kupreserve kumbukumbu. Watu wanakwenda shule kusoma historia ya hip pop, rap reggae etc etc..sisi hatuna uwezo wa kufundisha utamaduni wetu mashuleni basi tungeweza kupreserve hizi dance styles zetu hata kizazi kijao kione...ukijadili kwenye vijueni ...kesho itaishia huko huko vijiweni na itakua wastage of time....
ReplyDeletehebu kwanza tueleweshe hiyo kiduku ni nini na inachezwaje na siye tulio mbali na upeo wa macho tuelewe ...who knows it's something very interesting that even grown ups can sit in a bar and decide to get into a hot discussion about it and then decide to take his time and sit down and write your email to Mr Michuzi regarding the same issue asking all Michuzi community to tell him about it...it must be something worth to know..I am in ..I wanna know tooo...what is that and who was the founder of Kuduku music, dance style whatever...I just want to know.... I gonna write a book about it and put in Makumbusho....heheheheheh. so nxt time people from vijueni will just get all information they want from there....
Tatizo nini jamani? mtu ameanzisha topic kama unaona ni kupoteza muda kwanini unasoma???? Wakati wote sio wakuwa serious!!! Kazi zetu wengine zinahitaji kufikiria kwa muda mrefu. kwahiyo vimada kama hivi vinatuliwaza!! Kuna mtu anaweza kuweka hiyo style ya kiduku kwenye youtube plz???
ReplyDeletewabongo wengi mnaosota huko nje mna tabia ya kuonyesha frasturation zenu mnapoona ishu kama hizi.
ReplyDeletehatuna haja ya kujadili simu, gari sijui nini kwa sababu tunajua nani katengeneza ni factory products na zina majina ya watengenezaji na nchi zilikotoka OK? tafuteni nauli maana najua zinapiga chenga... rudini nyumbani kama wengine walivyofanya tayari halafu mtumie hayo maarifa yenu mliyovuna huko ughaibuni kama kweli yapo au mmezidisha majungu tu.
hii ni blogu ya jamii na hili swala ni la kijamii.
tungejadili MICK JAGGER msingechonga sababu ni slave master wenu SHENZY KABISA tena tumechoka kuona watu kama nyinyi mnakandya kila kitu cha nyumbani kwenu shame on you mnahitaji kujikomboa na slavery mentality.
kwasababu mnafanaya kazi 18 hrs a day ndio maana mnapandwa hasira mkisikia watu wapo vijiweni na bado wanaishi; ishu ni kwamba sio lazima mtu akiwa kijiweni hafanyi kazi. inawezekana jamaa wapo workshop za milango, madirisha nk.
mngekuwa na busara mngeuliza kiduku ndio nini kama mdau mmojawapo alivyouliza. trying to get closer to your home au sio?!
yaani kama hii blog ingekuwa ni ya kihuni... mngeoga mitusi yaani mmeniudhi mwisho wa maelezo. nani alikulazimisheni kukimbilia huko?
wengine mnaona aibu kurudi kwa jinsi mlivyopauka.
endeleeni tu kubeba hayo maboxi who cares?
MWISHO: MADA NI NZURI SANA NA NAUNGA MKONO NA MGUU PIA. MDAU ALIYESEMA NI YA WERRASON YUKO RIGHT.
Mdau Kinondoni
JAMANIEE MSITUBONDE SIO WOTE TULIO MAJUU TUNA AKILI SAWA,KUNA TULIOKUJA NA WALIOLETWA HAO NDIO IGNORAMUS MTAUMIZA VICHWA BURE,ACHIMENENGULE TUNAJUA KOMBA IMESHINDWA KICDUKU KAMA IMKUBALIKA NA JAMII SIO VIBAYA TUKAMJUA MUASISI WAKE MINILIMUULILIZA DOGO ALLY KIBA HAPA UK NIKAONA HANA UHAKIKA NANI KAANZISHA,UK ATA KWENYE PATI ZA WABONGO WENZETU WALIORUDI WAKICHEZA KWA PAMOJA KIDUKU INAFURAHISHA.MSHIKAJI SWALI LAKO POA ACHANA NA HAO WALIKUJA KWA KWA EXHIBITION.
ReplyDeleteMijadala hii ya kipi kilianza kati ya kuku na yai huwa haina mwisho,na inapendwa sana na watu wasio na shughuli maalum.Okay,ukishafahamu kuwa mwanzilishi wa kiduku ni ABC,hao jamaa zako kijiweni wataafikiana nawe?Na hata wangetaka kuafikiana nawe,bado ubishi ungeendelea maana ubishi huo ni sehemu ya kupoteza muda.
ReplyDeleteAnyway,mkishachoka kubishana kuhusu kiduku mhamie kwenye chanzo cha umasikini wa Tanzania,na namna ya kupata ufumbuzi.Jibu katika mjadala huu linaweza kuwa na manufaa makubwa si kwenu tu bali hata kwa vizazi vijavyo,tofauti na hiyo ishu ya kiduku inayowatoa mapovu kwa kubishana.
Watu wazima hovyoo!
MDAU WA KINONDONI UNA HASIRA KAMA NINI HII NI BLOG YA JAMII NA UTANI UPO, WATU WANAVYOKANDIA VITU DON'T TAKE IT SERIOUS MAN, UNAVYONEKANA KATIKA MAELEZO YAKO UMEWAHI KUWAWEPO HUKU UGHAIBUNI NA BOX UNALIJUWA KISHENZI, UMELISOTEA KINOMA, NAHISI UMEKUWA HUKO NA MAKARATASI YALIOTA MBAWA, SASA UKO NYUMBANI UNAKULA KUKU KWA KWA MRIJA, PEOPLE HERE ARE JUST JOKING DON'T THEM SERIOUS MAN!
ReplyDeleteHuu mchezo ulianza maeneo ya Kinondoni Msisiri. Huu si mtindo mpya wa uchezaji muziki isipokuwa kilichofanyika ni kuongeza manjonjo kidogo kwenye mtindo wa "break dance". Kilichofanyika kwa vijana waliobuni mtindo huu wa kiduku ni kucheza break dance rusha roho zilizokuwa zikipigwa kwenye masherehe ya mtaani, hasa kwenye camps. Mtindo huu ulisambaa taratibu katika maeneo ya kinondoni shamba, msasani na baadae magomeni na maeneo mengine. Kadri ulivyokuwa ukisambaa ndivyo ulivyoingizwa katika kucheza aina nyingine za muziki mf. bongo fleva, dansi, n.k.
ReplyDeleteWote mliomponda mwanzisha mada ni pimbi tu mnasema anapoteza muda hana kazi ya kufanya wakati mmesoma na kuchangia kama hawana mambo ya msingi na wanapoteza muda mbona umesoma na kuchangia huo muda umekugharimu nini, Kiduku cha mtanzania hata mimi sijui wenye majibu msaidieni, siku hizi bongo vijiweni ndio magari yanauzwa, hivi hamjui kuna watu wa vijiweni ndio walipiga fedha za EPA,
ReplyDeleteKUJUA NINI MAANA YA KIDUKU ANGALIA VIDEO YA BLICK & LACE KWENYE WIMBO WA MY LOVE IS WICKED KUNA STAGE SHOW MMOJA AMEVAA NGUO RANGI YA NJANO
ReplyDeleteKama mada iliyoanzishwa unaona haina maana just be silent. Usiandike kinyesi hapa. baadhi ya comments ni kichefu chefu.hivi kama wewe u serious sana na kazi, why even waste your time reading and commenting on what u call "non sense". let people be.
ReplyDeletetukianza kudiskasi chanzo cha umaskini tutamkwaza mwenye blogg hii maana itabidi na wakubwa wa nchi walaumiwe kwa kuwa hypnotised na nchi za magharibi na huko amerika so it's better not to use this blogg politically.
ReplyDeletenakumbuka kulikuwa na blogg moja bomba sana ya jambo forum. hii ilikuwa noma sana yaani kuntu. lakini ilifungiwa sababu hii.
anyways wote mlochangia... tahks a lot nadhanin hata ankal amefurahi huu mjadala umekuwa na sparcs!!!
samahani kama kuna watu nimewakwaza
mdau kinondoni.
mwanzilishi ni msanii anaitwa Mataluma aliimba wimbo wa Mama Mbaya.. kipind hicho hata Marlow hakuwa ameimba huo wimbo wa Pipii.. tazama video hapa http://m.youtube.com/watch?v=nVsGk85ZDPg
ReplyDelete