
Mnara wa bia ya Ndovu Special Mart wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio unavyoonekama mara baada ya kuzinduliwa leo.

Mnara wa Ndovu Special Mart ukizinduliwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),
Robin Goetzsche akifafanua jambo kuhusu bia ya Ndovu Special Mart huku akiwa ameshika chupa ya kinyaji hicho katika uzinduzi wa mnara wa bia hiyo leo wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio uliopo maeneo ya Namanga jijini Dar.

Meneja wa Bia ya Ndovu Special Mart,Oscer Shelukindo akielezea namna walivyoweza fanikiwa kupata tuzo ya ubora wa bia kutoka kitivo cha upimaji na ubora (Monde Selection) ambao bia ya Ndovu Special Mart iliupata huko nchini ujerumani ambapo kwa kulienzi hilo kampuni ya bia ya TBL iliweza kutengeneza mnara mkubwa katika maeneo ya Namanga jijini Dar unaoonyesha mfano wa chupa ya bia hiyo uliozindiliwa rasmi leo.

Mpishi mkuu wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),Mzee Gaudence Mkolwe nae aliongea machache kuhusu bia hiyo katika uzinduzi wa mnara wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio wa bia ya Ndovu Special Mart,uliozinduliwa leo jijini Dar.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),
Robin Goetzsche (kati) akigonganisha chupa na Meneja wa Bia ya Ndovu Special Mart,Oscer Shelukindo (kushoto) pamoja na Mpishi Mkuu wa kampuni hiyo,Mzee Gaudence Mkolwe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mnara wa bia hiyo ya Ndovu Special Mart uliopo Namanga jijini Dar.
Burudani ikiendelea kabla na baada ya uzinduzi huo.

Wadau wa TBL wakigonganisha chupa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mnara huo.

Viongozi wa Juu wa TBL wakifuatilia uzinduzi huo.

wadau mbali mbali waliofika katika sehemu iliyoandalia kwa ajili ya uzinduzi wa mnara wenye kuonyesha sehemu ya mafanikio wa bia ya Ndovu Special Mart,wakishuhudia uzinduzi huo leo katika maeneo ya Namanga jijini Dar.
Watu ohhh after 4 days ni picha ya Kikwete na CCM kuomba kuchaguliwa tena kiko wapi? Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza jamani.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteNinyi watu wa tz, hakunaga kasi ya kufanya, mbona mnapeana ma ujinga ya kukunya pombe tuuuuu, hii siyo kitu ya kusherekea, bwana hii ni ya kufanya kwa siri tu, sasa inyi hakyna maendereo lakini wanaabiki pombe tuu weeeee, hakuna maendereo
ReplyDeleteMujomba Paulo Kamau
Nakuru Kenya
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteWabongo hatuna ila haya mambo tu kila siku viwanda au aina mpya ya pombe ambapo haileti faida yeyote ya nchi, tutabaki kulewa mpaka lini watu wanaendelea na kutengeneza viwanda vya maana sisi na pombe kila kukicha.
ReplyDeletenchi ya walevi !! wenzenu wanapenda pombe na kazi !!nyie mnapenda starehe kuliko kazi !!
ReplyDeletewatanzania tumezidi kuabudu upumbavu jamaniee
ReplyDeleteJamani Michuzi,
ReplyDeleteTunajua una vijana wa kazi ndio wanakusaidia ku update blog ukiwa haupo Bongo. Sasa, waambie wawe makini kidogo.
Wameandika uzinduzi wa Ndovu special 'mart' mi nikajua kosa moja tu, kwenye habari yenyewe wata rekebisha, kumbe wapi!! Mart imeandikwa humo zaidi ya mara 5!! Nikaangalia kuona hilo duka au soko la Ndovu li wapi?
Kumbe malt
Watu wa dini wafanye nini?,kwani mmelazimishwa kunywa?wamewatangazia wanaojua kuburudika na kilaji,kama nyie hamtumii mkiweza fumbeni macho msione kabisa
ReplyDeleteahmada umeleewaaaaa..X 3
ReplyDeleteHaloow
ReplyDeleteHii ndo Bongo na hizi ndo bongo zetu, kama mtu hataki akakojoe akalale au aanzishe chake nae aje afanye uzinduzi ili "aprove" kama na yeye anaweza, maneno hayajengi, mmekalia uvivu wa kufanya kazi na mnachoweza kufanya ni kupiga SOGA tu... HAMNAZO NYIE.
kipapai.
Eti pombe hailetei nchi faida!!!!!! na tax je???????????? hivi unajuwa kodi ya kutokana na beer ndo inaendesha serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteOnyo kwa akina dada usiolewe na wanywa pombe kwani familia yako itasambaratika kabla hujazeeka, hakuna furaha zaidi ya kunusa pombe za watu usiku mzima. Rushwa na umalaya unasababishawa na hizi pombe. Dada jisome na jitahidi kuwalimisha wengine wanotarajia kuolewa na hawa walevi, Hao wenzetu weupe wanjuwa kunywa na wanjuwa maana yake ni kitu gani, sisi akina yahe tunafuta mkumbo, hata bia itashuhwa bei ili tuendelee kunywa. Poleni sana wanfamilia kwani najuwa pombe ni adui ya jamii yetu.
ReplyDelete