Mnara wa bia ya Ndovu Special Mart wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio unavyoonekama mara baada ya kuzinduliwa leo.
Mnara wa Ndovu Special Mart ukizinduliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),Robin Goetzsche akifafanua jambo kuhusu bia ya Ndovu Special Mart huku akiwa ameshika chupa ya kinyaji hicho katika uzinduzi wa mnara wa bia hiyo leo wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio uliopo maeneo ya Namanga jijini Dar.Meneja wa Bia ya Ndovu Special Mart,Oscer Shelukindo akielezea namna walivyoweza fanikiwa kupata tuzo ya ubora wa bia kutoka kitivo cha upimaji na ubora (Monde Selection) ambao bia ya Ndovu Special Mart iliupata huko nchini ujerumani ambapo kwa kulienzi hilo kampuni ya bia ya TBL iliweza kutengeneza mnara mkubwa katika maeneo ya Namanga jijini Dar unaoonyesha mfano wa chupa ya bia hiyo uliozindiliwa rasmi leo.
Mpishi mkuu wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),Mzee Gaudence Mkolwe nae aliongea machache kuhusu bia hiyo katika uzinduzi wa mnara wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio wa bia ya Ndovu Special Mart,uliozinduliwa leo jijini Dar.Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),Robin Goetzsche (kati) akigonganisha chupa na Meneja wa Bia ya Ndovu Special Mart,Oscer Shelukindo (kushoto) pamoja na Mpishi Mkuu wa kampuni hiyo,Mzee Gaudence Mkolwe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mnara wa bia hiyo ya Ndovu Special Mart uliopo Namanga jijini Dar.
Burudani ikiendelea kabla na baada ya uzinduzi huo.
Wadau wa TBL wakigonganisha chupa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mnara huo.
Viongozi wa Juu wa TBL wakifuatilia uzinduzi huo.
wadau mbali mbali waliofika katika sehemu iliyoandalia kwa ajili ya uzinduzi wa mnara wenye kuonyesha sehemu ya mafanikio wa bia ya Ndovu Special Mart,wakishuhudia uzinduzi huo leo katika maeneo ya Namanga jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2010

    Watu ohhh after 4 days ni picha ya Kikwete na CCM kuomba kuchaguliwa tena kiko wapi? Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza jamani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2010

    This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  3. Ninyi watu wa tz, hakunaga kasi ya kufanya, mbona mnapeana ma ujinga ya kukunya pombe tuuuuu, hii siyo kitu ya kusherekea, bwana hii ni ya kufanya kwa siri tu, sasa inyi hakyna maendereo lakini wanaabiki pombe tuu weeeee, hakuna maendereo

    Mujomba Paulo Kamau
    Nakuru Kenya

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2010

    This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2010

    This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2010

    Wabongo hatuna ila haya mambo tu kila siku viwanda au aina mpya ya pombe ambapo haileti faida yeyote ya nchi, tutabaki kulewa mpaka lini watu wanaendelea na kutengeneza viwanda vya maana sisi na pombe kila kukicha.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2010

    nchi ya walevi !! wenzenu wanapenda pombe na kazi !!nyie mnapenda starehe kuliko kazi !!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2010

    watanzania tumezidi kuabudu upumbavu jamaniee

    ReplyDelete
  10. Mdau, BloomsburyJuly 24, 2010

    Jamani Michuzi,

    Tunajua una vijana wa kazi ndio wanakusaidia ku update blog ukiwa haupo Bongo. Sasa, waambie wawe makini kidogo.

    Wameandika uzinduzi wa Ndovu special 'mart' mi nikajua kosa moja tu, kwenye habari yenyewe wata rekebisha, kumbe wapi!! Mart imeandikwa humo zaidi ya mara 5!! Nikaangalia kuona hilo duka au soko la Ndovu li wapi?

    Kumbe malt

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2010

    Watu wa dini wafanye nini?,kwani mmelazimishwa kunywa?wamewatangazia wanaojua kuburudika na kilaji,kama nyie hamtumii mkiweza fumbeni macho msione kabisa

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 24, 2010

    ahmada umeleewaaaaa..X 3

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 24, 2010

    Haloow
    Hii ndo Bongo na hizi ndo bongo zetu, kama mtu hataki akakojoe akalale au aanzishe chake nae aje afanye uzinduzi ili "aprove" kama na yeye anaweza, maneno hayajengi, mmekalia uvivu wa kufanya kazi na mnachoweza kufanya ni kupiga SOGA tu... HAMNAZO NYIE.

    kipapai.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 24, 2010

    Eti pombe hailetei nchi faida!!!!!! na tax je???????????? hivi unajuwa kodi ya kutokana na beer ndo inaendesha serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2010

    Onyo kwa akina dada usiolewe na wanywa pombe kwani familia yako itasambaratika kabla hujazeeka, hakuna furaha zaidi ya kunusa pombe za watu usiku mzima. Rushwa na umalaya unasababishawa na hizi pombe. Dada jisome na jitahidi kuwalimisha wengine wanotarajia kuolewa na hawa walevi, Hao wenzetu weupe wanjuwa kunywa na wanjuwa maana yake ni kitu gani, sisi akina yahe tunafuta mkumbo, hata bia itashuhwa bei ili tuendelee kunywa. Poleni sana wanfamilia kwani najuwa pombe ni adui ya jamii yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...