Vumbi kutimka leo Helsinki Kati ya watani wa jadi FC BONGO ya Helsinki na TAS ya mji wa Tampere Finland. Timu hizo mbili za watanzania waishio miji hiyo mikuu ya Finland hukutana kila summer mara mbili, home na away. Mechi ya kwanza mwaka huu ilichezwa katika mji wa Tampere mwezi wa jana na wenyeji TAS waliambulia ushindi wa magoli 2-0 kwa taaaaabu.
Leo hii TAS wanadai ushindi kwao kama kawa kwani mtabiri wao PWEZA PAULO ametabiri kama hivyo inavyoonekana pichani. Picha ya pili ni ya mechi ilyopita inaonyesha mchezaji wa FC Bongo Bakari Wagadugu akidaivu lakini hakubahatika kuzawadiwa penati.

Habari na Picha kutoka kwa
Michuzi Blog Correspondant Finland.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2010

    Pweza Paul amestaafu kutoka katika fani ya "utabiri". Mwacheni a-enjoy retirement yake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2010

    MPIRA GANI HUO WA KUCHEZA KWENYE SENYENGE! NI WA KUTOWA VITAMBI VYA CHIPS YA MCDONALD NA KFC SIYO?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2010

    Matekeo ya jana ni FC Bongo 3 TAS 2, kwa hio pweza amechemsha this time!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...