Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetoa sh. 4, 875,000 kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (TASWA FC) kwa ajili ya kushiriki katika bonanza la waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha.
Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TBL. Alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula na posho kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa siku zote watakazo kuwa Arusha.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Meneja Uhusiano wa TBL, Edith Mushi alisema kuwa msaada huo ni moja ya kazi za TBL katika kusaidia jamii na safari hii wameamua kufanya hivyo kwa waandishi wa habari.
Mushi alisema kuwa mbali ya msaada kwa jamii, lengo la TBL pia ni kudumisha ushirikiano wa karibu kwa waandishi wa habari ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya michezo na katika sekta nyingine hapa nchini.
Alisema kuwa wanaamini kuwa mchango huo utaleta mafanikio kwa timu hiyo na kuweza kutetea vyema taji lake. “TBL inatambua na kuthamini mchango wenu katika maendeleo ya sekta mbali mbali ikiwa pamoja na michezo, tunayo furaha kubwa kuona leo hii mmekuwa mfano wa kuonyesha kwa vitendo mchezo wa soka, tunawatakia kila la kheri katika mashindano hayo na katika kazi ya kuelimisha na kukosa jamii,” alisema Mushi.
Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary alishukuru TBL kwa msaada huo mkubwa ambao umeipa nafasi timu yake kutetea ubingwa wake ipasavyo. Majuto alisema kuwa TBL imeonyesha mfano wa kuigwa kwa jamii kwani imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia masuala mbali mbali ya jamii hapa nchini.
“Hii ni faraja kuwa kwa TASWA FC kwa kuwa na kampuni yenye kujali waandishi kama TBL, tunaahidi kufanya vyema katika mashindano hayo na kuibuka na ushindi,” alisema Majuto. Alisema kuwa Tanzania kuna makampuni mengi sana, lakini kutokana na kutojua umuhimu wa waandishi wa habari, wameshindwa kuchangia punde waombwapo misaada, na mara nyingi wakitoa majibu ya barua ya maombi kwa njia ya simu siku tatu kabla ya safari ya kuwa ``ombi lenu halikufanikiwa’’.
“Kwa kweli tumepata usumbufu mkubwa sana, kwani tulikuna vichwa ili kujua nini kifanyike ili kuikomboa timu na kufanikisha safari yetu,” alisema Majuto.
Mbona hiyo hundi inaonekana figure zinasema 4,800,000 Tshs lakini kwa maneno inasema FOUR MILLION AND EIGHTY THOUSAND ONLY ambayo tukiweka figure zake itaonekana kama hivi 4,080,000.
ReplyDeleteNadhani maneno sahihi ya hizo SHS4,800,000 yangekua hivi kwa kimombo "FOUR MILLIONS AND EIGHT HUNDRED THOUSANDS ONLY"
Nawakilisha
kweli watu kwa kuchunguza, nakuaminia mdau Thu Jul 29, 02:14:00 PM!!!
ReplyDeleteNadhani kosa kama hilo linaonyesha kiasi cha uzoefu kwa wahusika, mradi sio hundi halisi ni mfn tu, na msaada umetolewa ipasavo.
Pia wahusika wajitahidi kosa kama hilo lisitokee tena, kwani ujumbe unasomwa na wengi.
Keep it up Edith
Rubbish, how could u fagilia madudu?? we need professionalism in everything eti 'mradi' inaeleweka. Watanzania bado mko katika level ya kufanya vitu kwa kiasi cha 'just good' insteady of Exellent. Even the story haiko katika proper flow ya tenses....zero tupu
ReplyDeleteMimi mzee Kifimbo Cheza
Unaona hawa wa Tanzania ambavyo hawajui kuandika amount in words. Alafu wanasema waendeleze kiswahili. The amount should read: Four million eight hundred thousand(American way). Hicho kiswahili mnachokikumbatia hakiwapeleki popote. Mnadanganyana tu. Halafu kwa nini kila senior official wa TBL ni MCHAGGA? Acheni ukabila nyie WACHAGGA. Si kweli kuwa watu wengine hawana sifa za kufanya kazi isipokuwa WACHAGGA peke yao.
ReplyDeleteWACHAGGA SABABU TUMEPIGA SHULE ATHI! WEE CHEZA NGOMA TUU!
ReplyDeleteHii inaonyesha watu wamepigwa vyeo bila kwalifikesheni yeyote. Hiyo hundi ikishakosewa maneno basi ni batili iandikwe nyingine.. duuh!! Kiingereza cha Kimarekani tunasema Four Million Eight Hundred Thousand.. kizungu wanaongezea na ONLY!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteDaah na mimi nimeshachoka kupiga boxi sijui nije nipate cheo?
Mdau, Boston, US.
Hata makabila mengine yana wasomi vile vile. Tatizo ninyi wachagga mna ukabila mno. Ndio maana haitatokea siku hata moja mmoja wenu akawa rais wa Tanzania. Mtajazana Ikulu kuanzia mlinzi mpaka body guard. Tabia chafu sana. You guys don't know anything about diversity. Shame on you. Hayo si maendeleo, bali ni u selfish. That's why Nyerere ali make sure makabila yenye ukabila hayapewi nafasi kubwa.
ReplyDeleteWatanzania hakuna siku tukasifiana huwa wakwanza kuona makosa! Tumekubali cheki imekosewa sasa ishu ya wachaga na professionalism imeingiaje hapa? Kama mnaona walio katika ajira hawafai na nyie ombeni hizo nafasi si zinatangazwa?Na nina uhakika wote walioandika mambo ya uchaga ni wabeba mabox UK na US, mshachoka maisha yenu yasiyo na akiba,mnaanza ku-hate wabongo wenzenu walioamua kubaki nyumbani kutengeneza hela. You make a mistake, you correct it, next time it wont happen again! Ovyoooo!
ReplyDeleteEti Kimarekani "tunasema".... mnachekesha nyie mliokimbilia ulaya mnaacha familia zenu zinateseka, mnabakia kupraise mnaowabebea maboksi. Kama kweli mnasoma huko mliko basi rudini Tanzania, mchukue hizo nafasi mtuonyeshe hiyo professionalism! Bora huyo aliepata hiyo nafasi akakosea, kesho atajifunza ataandika vizuri, je wewe, wenye nchi yao wakikasirika ukarudi na sanduku la nguo tu na viatu utaeleza nini ukoo wako? kaa kimya kabisa,soma kwanza, rudi nyumbani and make those changes.
ReplyDeleteWewe wa 5:27 pm, hujui unachoongea. Kwanza U.S. haiko Ulaya. Inaonyesha jinsi gani ambavyo geography yako ni poor. Pili, sio kila aliye U.S. anabeba mabox. Tatu, kuna wa Tanzania wengi tu hapa U.S. ambao wamesoma kuanzia associate mpaka PhD., na wanafanya kazi nzuri tu. Nne, unazungumzia wenye nchi wakikasirika watu watarudi na sanduku la nguo. Kosa! WaTanzania wengi U.S. wamerekebisha mambo yao, either ni permanent residents au ni maraia. Mfano mimi mwenyewe hapa nina passport ya U.S. kwa miaka sasa. Nikija kutembelea ndugu zangu Dar, naenda kwenye embassy yenu kuomba visa. Passport yangu ya Tanzania ili expire miaka na SINA MPANGO WA KUI RENEW. Kwa sababu ninyi mmejaa rushwa na kutokuwa wastaarabu. Ndio maana mimi na wengine wengi hatutaki kurudi kwenye nchi iliyojaa rushwa na social injustice kibao. Hata kutoa mali zako bandarini eti uhonge mbali na tax halali unayolipa. Pia hata huyo uncle Sam wenu hajui ku calculate tax anyway. Badala ya kum tax mteja percentage ya value according to bill of lading, TRA wana calculate kivyao vyao. Kwa nini nije kuishi among corrupt people? Kama kwa elimu yangu naweza kulipwa U.S. $ 50,000+ kwa mwaka hapa U.S., kwa nini nije Tanzania ambako sitakuwa na uhakika kama nitalipwa mwisho wa mwezi, kwa kuwa mishahara inacheleweshwa. Na huo mshahara ni mdogo, kwa sababu ninawafahamu wa Tanzania wanaolipwa zaidi ya mara mbili ya hiyo ($100,000+) kwa mwaka. Convert hiyo hela into T Shillings uone ni kiasi gani. Sababu nyingine kwa nini nije kuishi Tanzania alafu watoto wangu wabaki wanaumwa malaria kila kukicha, au wawe wana nyanyaswa na wenye dala dala kwa sababu nauli yao ni ndogo alafu wachelewe kufika shuleni? Au wawe wanakuwa abused na walimu shuleni kwa kuchapwa viboko. Kama hamjui, kuchapa/kupiga mtoto ni CRIME. Hiyo ni phyisical abuse, matokeo yake mtoto anakuwa na heshima ya uoga, ambayo ni FAKE. Matokeo yake huyo mtoto akiwa mtu mzima kumbukumbu yake kuhusu mwalimu/mzazi ni NEGATIVE. Tembea uone/ujifunze. Kuna vitu vingi sana ambavyo huvielewi kwa sababu you have a closed mind. Ni mpaka pale utakapotoka huko na kuishi kwingine ndio utaona vitu fulani hapo Tanzania havina maana, na ni vingi sana.
ReplyDelete