Mgeni rasmi ambaye ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar es salaam,Mh Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mh. Sophia Simba.
Mmoja wa washindi waliochaguliwa,Bi. Ritah Mlaki akishangilia mara baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa washindi watano katika Matukio mbalimbali yaliyofanyika jana jijini kwenye uchaguzi wa Wagombea kupitia UWT kwenye mkutano Mkuu Maalum Wa uchaguzi Mkoa wa Dar es salaam uliofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika viwanja vya Sabasaba.
Katika uchaguzi huo wajumbe wa UWT waliwachagua wawakilishi wa makundi mbalimbali kwa ajili ya VITI MAALUUM, Mwenyekiti wa UWT Mkaoni Dar es salaam Zarina Shamte Madabida alikuwa mshindi wa kwanza. na kufuatiwa na Ritah Mlaki, Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mlezi wa Chama mkoa wa DSM Abdulrahman Kinana, na kuhudhuriwa na MWenyekiti wa UWT Taifa Sophia Simba.
Mgombea wa Viti Maalum Janeth Masaburi akiomba kura kwa wanachama.
Wanachama wakigawiwa karatasi kwa ajili ya kupiga kura.

(picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2010

    Mheshimiwa naomba matokeo ya Sumbawanga!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2010

    Sasa nimeamini kuwa hii ni blog ya CCM. kila siku habari za CCM tu, kwa nini huweki za vyama vingine?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2010

    Shehe Michuzi, siye wote wanaume bwana. Nisaidie contacts za huyo dada anayegawa pepa za kura. Nsaidie shehe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2010

    mama masaburi kashindwa??? duh hii kali..hongera mama madabida kwa ushindi wa kishindo..hongera ritha mlaki kwa ushindi wa kishindo...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2010

    jamani huyu mama Sophia Simba, anafanana na Rep. Sheila Lee Jackson(D) Texas. I could be wrong

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 30, 2010

    Wanaopiga kjura hapo wameneemika kweli walal hoi wako wapi?

    ReplyDelete
  7. mlala hoiJuly 30, 2010

    Je Vyama vya upinzani navyo vinapewa nafasi ya wabunge wa kuteuliwa na wabunge maalumu? Je kama wanapewa idadi inakuwa katika uwiano gani? Bwana Michuzi naomba unitafutie jibu tafadhali. Nitashukuru sana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 30, 2010

    JK alisema wanawake waende majimboni wakagombee na si kusubiri wateuliwe, sasa Ritha Mlaki amecha kwenda Kawe ndo ameingia kwenye viti maalumu UWT au aliyelewa alifahamishe tafadhali.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 30, 2010

    Ati Ritha Mlaki kapita kwa kishindo kama mwakilishi wa NGOs??!! Tangu lini Ritha na NGOs! Acheni sinema za Fiction! Khaaaaa!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 30, 2010

    Kunani dodoma? Mbona watu wakipata wanashangilia sana?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 31, 2010

    Duh Mi nliskia atii madam Rita amestaafu yaani ameritirez... sasa hapa hata sielewi... hembu nisaidieni.... kustaafu si ni kuacha kabisa ama waweza tokea kwa pande ingine kwa shuhuli ile ile !!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...