Vumbi kutimka leo Helsinki Kati ya watani wa jadi FC BONGO ya Helsinki na TAS ya mji wa Tampere Finland. Timu hizo mbili za watanzania waishio miji hiyo mikuu ya Finland hukutana kila summer mara mbili, home na away. Mechi ya kwanza mwaka huu ilichezwa katika mji wa Tampere mwezi wa jana na wenyeji TAS waliambulia ushindi wa magoli 2-0 kwa taaaaabu.Leo hii TAS wanadai ushindi kwao kama kawa kwani mtabiri wao PWEZA PAULO ametabiri kama hivyo inavyoonekana pichani. Picha ya pili ni ya mechi ilyopita inaonyesha mchezaji wa FC Bongo Bakari Wagadugu akidaivu lakini hakubahatika kuzawadiwa penati.
Habari na Picha kutoka kwa
Michuzi Blog Correspondant Finland.



Pweza Paul amestaafu kutoka katika fani ya "utabiri". Mwacheni a-enjoy retirement yake.
ReplyDeleteMPIRA GANI HUO WA KUCHEZA KWENYE SENYENGE! NI WA KUTOWA VITAMBI VYA CHIPS YA MCDONALD NA KFC SIYO?
ReplyDeleteMatekeo ya jana ni FC Bongo 3 TAS 2, kwa hio pweza amechemsha this time!
ReplyDelete