ujumbe uliobwebwa na waandamanaji hao leo waliotembea toka mnazi mmoja hadi manzese katika maandamano ya kushinikiza kuanzishwa mahakama ya kadhi leo jijini dar
waandamanaji
ujumbe
waandamanaji wakiandamana









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 59 mpaka sasa

  1. M&M$%##F'uRJuly 09, 2010

    kwa kuangalia hii picha harakaharaka naona hawa jamaa sura zimechokaaa sanaa sijui njaa kali ama jua la bongo. inakaa wamejazwaa ujinga na watu fulani or wamepatiwa posho kidogo waandamane. orelse ni wafwata mkumbo wasiofikiria kabla ya uamuzi.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2010

    nakuungeni mkono waisilamu wenzangu 100%.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2010

    M&mp !
    ukisema njaa kali una maanisha nn?maskini,hawajala au?

    Ni haki ya kikatiba kuandama wajua?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2010

    ITAMBULIKE KIKATIBA? KWANI TANZANIA NI NCHI YA KIDINI? KAMA NINYI WAISLAM MNATAKA KUANZISHA KADHI COURT YENU MNARUHUSIWA KUANZISHA KWANI KUNA MTU ALIYEWAZUIA? MSITAKE KUTUFANYA WASIO WAISLAMU TUFUATE MKUMBO WENU...SIJUI KWA NINI MNA UELEWA MDOGO NAMNA HIYO MMESHAELEZWA KAMA MNATAKA KUANZISHA MAHAKAMA YENU MUANZISHE LAKINI SI KUSHINIKIZA SERIKALI IWAANZISHIE..TANZANIA HAINA DINI!

    ReplyDelete
  5. Wewe unayejiita mdau wa USA acha kutukana watu unasema wanaonekana wamechoka, au kwa sababu huko Unyamwezini sisi wengine tumekaa huko Marekani hakuna mpango wowote ule watu wengi kama wewe mnafanya kazi za kuosha mavi ya wazee kwenye manursing home na mnawaacha wazee wenu huku Bongo wakiwa hawana watu wa kuwaangalia.

    ReplyDelete
  6. Wagulugulu!July 09, 2010

    Wa akina mama wako wapi? Hili swala la mahakama ya kadhi linatakiwa kufanyiwa ufumbuzi wa kutosha, kuna swala la mwizi akikamatwa, talaka, mirathi, elimu, sauti kwa wakina mama na watoto wa kike.

    Pia serikali wanaangalia hii mahakama ya kadhi itashirikiana kivipi na vyombo vya dola kuhakikisha haki ya kila mwananchi haivunjwi kwa sababu tu dini inasema kitu fulani.

    Na kama ingekua mahakama ya kadhi ndo sababu ya waislam kushindwa kupata maendeleo basi wengine tungeelewa, lakini sio hivyo, sijui kuna sababu gani hasa au faida kubwa ilioje hii mahakama itawasaidia waislamu.
    Waislam hebu tuwe na subira kidogo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2010

    Hawa ndio wenzake na Mike Tyson

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2010

    mdau USA
    inaonekana uwezo wako wa kuona na kutoa maoni ni mdogo sana, kupigwa na jua au kua na njaa haizuii kudai kile unachokiona ni haki yako.It seems hujui uandikalo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 09, 2010

    Wanawake wako wapi?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 09, 2010

    Ngoja mkianza kukatwa mikono ndo mtalia kilio cha Mbwa! Mnafikiri Sharia itawakuta mawaziri, makatibu, matapeli wakubwa? Ni sisi tu walala hoi tunapoiba mhogo ili tuwape familia zetu chakula mezani... Asilimia 80 nina hakika hata hawajui kinachoendelea, twendeni shule na tuache mambo ambayo haytufikishi popote! kumbuka Serikali yetu HAINA DINI!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 09, 2010

    M&M$%##F'UR, hiyo ndio nguvu kazi ipo tayari kujitoa kafara na kujilipua kwa kisingizio cha jihad, muulize mdau wa Afighanistan atakupa data kamili.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2010

    SASA HUYO KADHI ATAMBULIKE BA KATIBA INA MAANA BASI KATIBA IFANYIWE MAREKEBISHO SIYO? NA HII INABIDI IFANYIWE MJADALA NA WANANCHI WOTE NA IENDE BUNGENI IKAPIGIWE KURA NA WABUNGE NDIYO IINGIZWE KWENYE KATIBA BASI HIYO SI MWAKA HUU, ILI HILI LIKAMILIKE BASI TUAAHIRISHE UCHAGUZI MWAKA HUU TUANZE MCHAKATO WA KATIBA KWANZA IKIKAMILIKA NDO TUFANYE UCHAGUZI MKUU, SASA KWANI HUYU KADHI AKIRUHUSIWA TU NA NYARAKA ZINGINE ZA SERIKALI HAITOSHI? LAZIMA AINGIZWE KWENYE KATIBA? HILI NI JAMBO LA DINI WANA DINI WENYEWE WAKUBALIANE NA WAANZISHE KADHI WAO NA WALE WANADINI WATAKAOONA KESI YAO IENDE KWA KADHI HIYO NI JUU YAO SI JUU YA SERIKALI, MBONA TAYARI DINI ZINGINE NA KAMA SIKOSEI ZINASIKILIZA KESI ZA WANADINI, KUNA MAPADRE WANASIKILIZA KESI KAMA ZA UNYUMBA PALE WATU WALIOOANA WAKIKOSEANA WAKO WANAOPELEKA KESI YAO KWA PADRE NA AKAWAONGOZA VIZURI TU NA KAMA SIKOSEI HATA WAKO MASHIEK WANASIKILIZA KESI ZA WAUMINI WAO. HILI NI JAMBO LA DINI LIAMULIWE NDANI YA DINI KAMA WAMATAKA KADI WAANZISHE TU. ILA JAMII HAITAKI HII KITU IGARAMIWA NA SERIKALI KWANI ITALETA VURUGU KWA MAANA KWAMBA KILA MTU ATAANZA NA MIMI DINI YANGU NATAKA KUANZISHA SYSTEM YANGU YA KUSIKILIZA MALALAMIKO NA KESI ZA WAUMINI WANGU NATAKA PESA YA KUANZISHA MAHAKAMA YANGU, IKITOKEA HIVI SERIKALI ITAKATAA? NA MAHAKAMA TULIZONAZO ZITAFANYA KAZI GANI TENA KWANI KILA KESI YA MUUMINI WA DINI FULANI ATAKWENDA KUIFUNGUWA KWENYE DINI YAKE. PIA NINA WASIWASI KAMA HIZI MAHAKAMA ZA KIDINI TAYARI ZINAUWEZO WA KUSIKILIZA KESI. KWA MFANO MUUMINI WA DINI FULANI AMEUA MTU HII KESI ITAENDA MAHAKAMA GANI? AU KUNA SPECIAL CASES TU ZITAKUWA ZINASIKILIZWA NA HIZI MAHAKAMA ZA KIDINI NA KAMA NDO HIVYO KUNA HAJA GANI YA KUINGIZA KATIKA KATIBA - MWISHO RUKSA KADHI RUKSA AANAEA KAZI YAKE LAKINI OFF THE GOVERNMENT TILL

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 09, 2010

    Jihad maana yake si vita ya kuuwana watu embu nendeni kusoma tena na mutafakhari maana ya jihadi, kama mnamaanisha jihad ya vita sasa mnataka kupigana na nani serikali? au? maana serikali ndo yenye uamuzi wa kadhi awepo au asiwepo kupitua bunge na wanchi wote wa Tanzania, na kama mnataka atiwe katika katiba basi ni lazima kuwa na REFERANDUM wananchi wote wahusishwe na wapige kura juu ya hilo na lipelekwe bungeni likapigiwe kura na wabunge baada ya kupigiwa na wananchi wote, lazima iwe hivyo kwa vile katika ni ya wananchi wote na kubadilishwa kwake ni lazima kuridhiwe na wananchi wote, and then the president should sign it.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 09, 2010

    sipingi hio mahakama kwa sababu sijui kama KATIBA INARUHUSU, wasiwasi wangu ni kuwa hao waandamanaji,ni % wanajua maana ya MAHAKAMA YA KADHI na kama katiba inaruhusu hio mahakama.Badala ya jazba za kusema hata kwa JIHAD wanataka hio mahakama wangejiuliza kwanini mpaka leo haipo?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 09, 2010

    Katiba ya nchi inapinga vitisho!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 09, 2010

    Mahakama ya Kadhi Mkuu hutetea haki fulani zilizoainishwa katika dini yetu ya Kiislamu.

    Ninachoshindwa kuelewa mimi ni hiki, kwani lazima iwe kwenye Katiba na mfumo wa sheria wa nchi ambayo si nchi ya Kiislamu?

    Iwapo nchi inaweza kutambua mila na desturi za makabila, kuna ugumu gani kuhusu hii? Kwa nini isiwe huku huku misikitini na kisha watu tukishindana ndiyo tunakwenda kwenye mahakama za serikali?

    Jamani Waislamu wenzangu, tuache kelele. Mahakama yetu ni yetu, acheni ikae kwenye mikono yetu na si ya serikali.

    Mungu Mkubwa Waislamu wenzangu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 09, 2010

    wewe mpiga box hapo juu acha ushamba wako hapo kuna watu wanapesa kukuzidi ktk haohao wanaoandamana, kama huna la kusema kwani ni lazima uweke comments??? unamaanisha nini kusema wamejazwa ujinga au wanafuata mkumbo?? mkumbo upi huo tueleze tuelewe, isije kuwa wewe ndiye unayefuata mkumbo??? je mtu kudaia haki yaki yake ya kidini ni kujazwa ujinga ama kufuata mkumbo?? inaonekana hata hujui unalolizungumza. kila kinachotokea bongo mna kandia utandani huko mnaishi maisha kama P Diddy wakati mnaishi maisha ya kubangaiza na yaliyo magumu bora hata huku.. anyway inaonyesha jinsi gani ulivyo mfinyu kimawazo hivyo kuna nafasi ya kukusamahe..
    BOX JEMA
    Wa hapahapa..

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 09, 2010

    Unfortunately katiba yetu haina mambo ua udini, japo inatambua na kuheshimu dini mbalimbali, na kutoa uhuru kwa wananchi wa Tanzania kuabudu dini wazipendazo. Mshanifahamu?

    Hivyo, mkae mkielewa kuwa kwa kufikiriwa tu kuwa kuna uwezekano wa kuwa na hizo mahakama za kadhi, mjue kuwa mmependelewa sana.

    Halafu jamani, hembu twende mbele, turudi nyuma, mnataka hizo mahakama za kadhi, ili iwaje? Then what?

    Hayo masharti yenyewe ya uislam mnayafata kiukamilifu? Hamnywi pombe nyie? Hamkwapui nyie? Hamzini nyie? Hivi mna upendo kweli nyie? Mnasamehe nyie? Hivi mnatafuta amani na watu wote nyie? Enh?

    Mnataka hayo mambo ya upanga kwa upanga, jino kwa jino, jicho kwa jicho, kupigana mawe mtu akizini, ili iwaje?

    Hivi jamani katika masuala ya dini, muhukumu wa kweli si ni Mwenyezi Mungu tu! Kazi ya Mungu haiingiliwi jama.

    Na hayo mambo ya Jihad mnayoyachochea hapo labda muombe mtengwe katika eneo lenu maalum ndio mfanye hizo jihad zenu. Msituvurugie amani.

    Utambulisho wa Tanzania ni amani.

    Amani iwe nanyi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 09, 2010

    TAKBIIIIR!

    Ila jamani, mbona mahakama za kazi zipo nyingi sana Tanzania?

    Au mlikuwa mnataka makahama kuu ya kazi?

    Kwanza nyie nyote hapo mna ajira kweli?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 09, 2010

    weka wewe sura yako tuione!!!wacha dharau !!unajiona umefika!!ATII!! USA ndio nini sasa '''

    ReplyDelete
  21. ...Nakubaliana kabisa na mdau wa kwanza hapo juu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 09, 2010

    Hivi kunatatizo gani kama mahakama ya kadhi ikitambulika na BAKWATA (si ya waislam bytheway) au ndo ikitambulika ndo iwahukumu hadi wahindu... am just asking??!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 09, 2010

    KADHI HATA KWA JIHAD? JIHAD MTAPIGANA NA NANI? KIKWETE, MKAMBA, BAKWATA WOTE WAISLAM WENZENU.

    MBONA KUNA MAMBO MUHIMU ZAIDI YA MAANA AMBAYO HAYAJETEKELEZWA NA SERIKALI NA MKO KIMYA. KADHI ATAWASAIDIA VIPI KUPAMBANA NA HALI NGUMU YA MAISHA SASA?

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 09, 2010

    kumekucha ati hata kwa jihad... !! hawa ndio walewale no ilimu mukichwa full makorokoro...
    mdau wa US uko right hii kitu si bure benderaz fata upepo, i luv north america full maendeleo no bla bla kama hapo pichani baada ya hiyo shughuli nzito ya kutembea juani huna shilingi mfukoni home hakieleweki no maji, no umeme mngeandamana ili mpata mahitaji nyeti haya mambo waachieni waliowatuma!!
    mdau canada

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 09, 2010

    Haya kadhi hata kwa Jihad,haya mimi yangu macho.Kujulikana kikatiba sio tatizo ila mnataka mahakama iendeshwe kwa fedha za walipa kodi ambao sio wote ni waislamu hiyo ni sahihi? na pia mjue serikali haina dini, kwa kugharamia hiyo mahakama inaonekana mnataka serikali iwe ya kiislamu.Ca marche pas comme ca,jamais,jamais.

    ReplyDelete
  26. Kuandamana ni sawa (mradi kwa amani), kutaka kadhi--sawa, But...LAZIMA?!...."HATA KWA JIHADI"? I don't think so...hapo ndipo wanakosea. Jazba...Jazba nduguzangu.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 10, 2010

    Mdau hapo juu nasapoti maoni yako kuna mtu kawahutubia ujinga wamecharuka bila kufikiri, ukiwauliza maana ya hiyo mahakama hata moja hawajui, kifupi wana ufinyu wa busara.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 10, 2010

    UKOSEFU WA SHUGHULI

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 10, 2010

    SUBHAANALLAH!!
    JAMAA WAISLAMU WENZETU HUKO TZ MNAPATWA NA NINI?
    MBONA MATENDO HAYAENDANI NA MAHUBIRI YA VIONGOZI WA DINI?
    MBONA HILO BANGO LENU LINAPINGANA NA MANENO YA KIONGOZI WETU, MTUME WA ALLAH, MUHAMMAD SAW?
    KUNA NINI HASA?
    AU MAADUI WANAKUTUMIENI KWA NIA YA KUIPAKA MATOPE DINI YETU ILI IONEKANE NI CHANZO CHA VURUGU NA ILIYOKOSA BUSARA?
    INAWEZEKANA KABISA PICHA HII INAWAKILISHA WATU WALIOFATA MKUMBO WASIOFIKIRI KABLA YA MAAMUZI.
    PIA INAWAKILISHA HALI YA HATARI, HALI YA UCHAFUZI WA AMANI AMBAO SI KWAMBA NI KINYUME CHA MAUMBILE TU, BALI PIA NI DHIDI YA MAELEKEZO YA KITABU CHA ALLAH YA KUTANGULIZA BUSARA, SUBRA, WEREVU, UPOLE, MAKUBALIANO NA UTULIVU.
    NAFAHAMU KUNA WATAKAONIPINGA NA KUDHANI KAMA KWAMBA NAPINGANA NA HARAKATI ZA WAISLAMU WA NYUMBANI ZA KUDAI MAHAKAMA YA KADHI, LAKINI KWA KWELI LENGO LANGU SI KUPINGA JUHUDI HIZO.
    LENGO LANGU NI KUKUMBUSHANA TU KWAMBA KWA MUISLAMU, KILA MAAMUZI NA MATENDO YAKE NI LAZIMA YAFUNGAMANE NA MAFUNZO YA ALLAH NA MTUME WAKE.
    KAULI ZA VITISHO SI MWENDO WA MTUME SAW.
    WALA SI KWELI, KWA MUJIBU WA IMANI YETU, KWAMBA TUNALOLITAKA SISI NDILO LITAKUWA, HAPANA.
    LINALOKUWA, KWA MUJIBU WA AYA YA QURAN, NI LILE TU ANALOLITAKA ALLAH MWENYEWE. TENA BASI ANATWAMBIA:
    HAKIKA MWENYEZI MUNGU HABADILISHI HALI ZA WATU MPKA KWANZA WATU WENYEWE WABADILIKE@
    JE, WAISLAMU WA TZ MKO TAYARI KIASI GANI KUIPOKEA MAHAKAMA YA KADHI?
    JE MMESHABADILISHA TABIA ZENU ILI KUWA TAYARI KUTII AMRI ZA ALLAH NA MTUME WAKE?
    NAULIZA HAYO KWA SABABU NASIKITIKA KUSEMA KUWA NIMESHUHUDIA KWA MACHO YANGU MWAKA JANA TU NILIPOKUWA HUKO KWAMBA JAMII YA KIISLAMU INA MAPENGO MENGI NA NYUFA NYINGI ZINAZOTAKIWA KUZIBWA ILI IWE JAMII YENYE MSIMAMO, UADILIFU NA UTAYARI WA KUIPOKEA MAHAKAMA YA KADHI.
    NA PALE ALLAH ATAPOONA KUWA SASA JAMII YA WAISLAMU TZ IMEKOMAA NA IKO TAYARI KUIPOKEA MAHAKAMA YA KADHI, KWA AHADI YAKE MWENYEWE, MAHAKAMA ITAKUWEPO. WAISLAMU HAWANA HAJA YA KUANZISHA JIHADI FEKI YA KUSHINIKIZA MAHAKAMA YA KADHI, BALI KWANZA WAANZISHE JIHADI YA KUPAMBANA NA NAFSI ZAO, NA HAPO NDIPO ALLAH ATAWALETEA MAHAKAMA YA KADHI.
    IKIWA LEO HAPA UK MAHAKAMA YA SHARIA IMERUHUSIWA, KWA NINI HAPO TZ MAHAKAMA YA KADHI ISIWEZEKANE?
    ITAWEZEKANA LAKINI KWA UWEZO WA ALLAH, SI KWA JIHADI ZISIZO NA UTARATIBU MAALUMU
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 10, 2010

    Mdau hapo juu you are right. Ndivyo vichwa na akili vya binadamu mweusi vilivyo. Brain washed. Wako tayari kuchinjana hata na dada na kaka zao kwa ajili ya mila na tamaduni za kigeni. Jihadi kati ya mtanzania na mtanzania ndio nini sasa hiyo; ufumbavu mtupu. Afadhali wachina, wakorea, na hata waarabu wanatetea na kuimarisha mila zao. Hii issue nasema haimfaidishi wala kumkomboa mwandamanaji hata mmoja hapo.May be watatu wanne tu wa waloandamana. It is just a Mob psychology here.
    Haya, Yangu Macho!!!!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 10, 2010

    SAFI SANA PIGANIENI HAKI!!WANAFKI NA MAADUI NA WAJINGA WASIOJUA HAKI ZAO ZA MSINGI WATACHUKIA NA KUPONDA KUTOKANA ADUI HATA SIKU MOJA SUALA ZURI HAKUSIFI!!UKIONA ANAKUSIFIA UJUE UNAWALAKINI!!MAANA IMESHAELEZWA MWENYEZI MUNGU HAWATOWAPENDENI MPAKA MTAKAPOFATA MILA ZAO!!SASA HAWATOPENDA ZURI LOLOTE LILE KWENU LENYE KULETA MAENDELEO!!SUALA LA WAISLAMU WAGALA NA WANAFKI KAENI PEMBENI HALIWAHUSU.MNAJUA UMUHIMU WAKE NA NDIYO MAANA LINAWAGUSA.
    PIA SIKU ZOTE WANAFKI HUMWABUDIA MWENYE NGUVU NA KUFYATA KAMA MBWA KOKO
    PIA WAJINGA SIKU ZOTE HAWAJUI HAKI ZAO ZA MSINGI NA PIA HAWAWEZI KUTOFAUTISHA ZURI NA BAYA.
    SAFI MUNGU ATAWAJALIA HERI MZIDI KUPIGANIA HAKI ZA WAISLAMU MUUACHE VIBARAKA NA MAADUI MIDOMO WAZI

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 10, 2010

    anonym wa kwanza ukisikia ugomvi wa kidini ndio huo hao wanapigania haki yao ya msingi mbaya zaid serikali ynu iliwaahidi na kuwageuka lkn inshallah MUNGU atatulipia duniani na akhera pia naona ameanza kwa zenji kwa kuleta mageuzi ya rais kutoka Pemba basi soon nanyi mtaipata tu joto ya jiwe

    ReplyDelete
  33. acha ushamba ww sasa ukiandika usa ndio nn?
    nyie ndio mlikuwa na dream ya kuzamia majuu kutokana na njaa zenu, bibi zako, babu zako na jamaa zako walioko afrika nao wamechoka vilevile kama ww.
    halafu sio unakurupuka tu kuongea wakati mambo huyajui limbukeni ww,sijui ulikuzwa uchi ndio maana akili ya kibinaadam huna!?

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 10, 2010

    hawa wanaodai kadhi, niruhusu niwafanyie survialance kwa miezi sita tu na kubaini makosa wanayo yafanya ktk maisha ya kila siku ambayo wangestahili adhabu kwa mujibu wa SHARIA kisha tuwaulize kama wapo tayari kuikabili hukumu ya sharia. sio wanakimbilia vitu pasipo kufahamu nani yuko behind the idea!!
    sasa kila dini wakidai hukumu zao zikidhi matakwa ya imani zao je nchi itakuwa a secular government au a religiously rulled govt???

    ReplyDelete
  35. WAGULUGULU!July 10, 2010

    Naomba tukumbuke haya mambo ya kufuata dini za wenzetu (uislamu na ukristu), zinaweza kutupeleka pabaya na baadae tukajutia.

    Ukristu na uislam tumerithishwa na wazungu na waarabu, yote heri amri kumi za mungu zinatuzuiwa kufanya maovu na kupendana kivile, lakini tusifuate mambo ambayo baadae tunaweza kujuta, wakati wa ramadhani, BAR zote Tanzania kunakua hakuna wateja! Na VITI moto huwa vinashuka bei, wakristu nao kama muonavyo wanavyoanzisha madhehebu mbalimabli mpaka ya pombe, tunakuwa kama tumechanganyikiwa na dini za watu (ndio, maana sio zetu!).

    Ukileta mahakama ya kadhi, ina maana waislamu wote watakua wanasikilizwa kesi zao huko, iwe mirathi, ndoa, vifo na usuluuishaji wa kesi ya aina yoyote, lakini mahakama ya kadhi inapendelea sana wanaume, na kusahau wanawake na watoto wa kike, sasa kama wewe ni baba kweli utakua unamtendea mtoto wako wa kike haki? Au utasema Mungu kapenda usipate urithi? Au asipate elimu na haki mbalimbali ambazo KWA SASA wanazipata bila matatizo yoyote.

    Ngoja niulize, kwani mahakama ya kadhi ikija itafanya maajabu gani makubwa zaidi ya mahakama zetu kwa sasa? Maana mkisema mahakama ya sasa kuna rushwa na wizi, lakini hata BAKWATA kila siku wanachapana viboko ama kwa kugombania uongozi au ubadhirifu wa mali!

    JAMANI, TUIGE DINI ZA WATU NA KUFANYA YALE MAZURI NA SIO KUIGA MPAKA SHERIA ZINGINE ZA DINI AMBAZO ZINAWEZA KUTULETEA MAAFA.

    HATUTARUHUSU NA HAITATOKEA. TUACHIENI NCHI YETU ILIO "SECULAR" IFANYA KAZI YAKE!

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 10, 2010

    Tembelea astrosheikhtz ktk youtube umuone Sheikh Yahya Hussein akisema masuala ya mirathi, ndoa, katiba na mali za wakfu za waislaam zote zimo toka enzi za Mwalimu Nyerere mwaka 1971 chini ya BAKWATA, hivyo wapendwa tutambue kuwa kuikataa BAKWATA tunakataa kazi iliyopewa BAKWATA kufanya kazi hizo za Kadhi, ambazo kikatiba hazitaleta mgogoro wa kuingiza serikali ktk masuala ya kidini iwe ya Waislamu, Wakristo, Wabahai, Wa Imani za Asili n.k
    Mdau
    Manzese.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 10, 2010

    NYIE WASLAMU MMNGEKUWA NA HUMOJA KAMA HUU WA MAENDELEO BASI TZ HINGEKUWA KAMA ULAYA VILE!! HILA NYIE MNA KUWA KAMA VIBERENGE MNA KWENDA KWENDA TU MBELE MBELE MNAKUWA KAMA ROBOT MKIAMBIWA RUKENI NAY NYIE MNARUKA HATA AMHUULIZI KWA NINI!!

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 10, 2010

    KATIBA YA TANZANIA, TANZANIA NA SERIKALI YAKE HAINA DINI, WANANCHI NDIO WENYE DINI.

    HAIWEZEKANI, HAITOWEZEKANA, NA HAITATOKEA HIZO MAHAKAMA KUTAMBULIWA KIKATIBA NDANI YA NCHI YA TANZANIA KWA MAANA ITAKUWA NI KINYUME YA KATIBA YA TAIFA LA TANZANIA.

    SWALI? HIVI HAYA MASWALI MBONA YANAKUJA KIPINDI HIKI? NA SIO KILE CHA BEN? AU NYUMA ZAIDI?

    ReplyDelete
  39. Hakuna siku Waislamu wa Tanganyika wamenifurahisha kama hii leo -kwa kudai haki zao.

    Vitisho vya vyombo vya dola havikusaidia kuzuiya nguvu za waislamu.

    Waislamu wameithibitishia CCM kuwa wanayaweza na wako tayari kwa lolote.

    Mahakama ya kazi ni haki yao waislamu. kama wakiristo wana wivu juu ya suala hili na wao waanzishe mahakama zao!

    Waislamu ,kwa umija wetu tulionao tunaweza kudai haki zetu!

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 10, 2010

    MIMI SIDHANI KAMA WANAKATAZWA KUANZISHA MAHAKAMA YA KADHI HII NI KITU YA DINI WAMALIZANE NDANI YA DINI KAMA NI KIZURI WAKIANZISHE, LAKINI SI SAHIHI KUHUSHISHA KATIBA NA SERIKALI, MBONA HATA SASA KUNA MAMBO YANAPELEKWA KIDINI MISIKITINI NA MAKANISANI SI WATU WAENDELEE HIVYO HIVYO TU MPAKA KATIKA IBADILISHWE JAMANI, NA DINI ZINGINE ZITADAI HIVYO HIVYO SI ITAKUWA VURUGU TU. JAMANI ANZISHENI TU SIDHANI KUNA MTU ATAWAKATAZENI! NI JAMBO ZURI KWENU HAMNA HAJA YA JIHAD

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 10, 2010

    Yale yale ya Somalia, watu wanaweza kuzuiwa kuangalia kombe la dunia kwa kuitafsri Koran wanavyotaka.Imani ni kitu hatari hasa unapojaribu kuishi tofauti na majirani wako. Mahakama wanayoiomba itakuwa inahamua kukata mikono na miguu ya watu? Tanzania ni nchi ya waumini wa dini tofauti kwa hiyo wanaomba lazima wazingatie hilo.

    ReplyDelete
  42. ''ya kaisali muachie kaisali''
    eti mtu ana comment humu kma ana elimu ya kujadili mahakama ya kadhi eti watoto hawatosoma wanawake watanyanyaswa hivi unajua kama wasomi wakubwa wengi ni waislamu>
    unajua aligundua hesabu?
    science?
    astronomy?
    economics?
    hivi unajua lolote kuhusu mkutano uliofanyika saudia na kuwakutanisha wanasayansi wakubwa kama keith moore,armstrong,marshall johnson,yushidi kusan na wengineo!
    hivi nyinyi mna elimu ya kumfikia yoyote kati ya hawa?

    haya mkatoliki eti na ww unataka mahakama yako kitabu gani chako kinasema uwe na mahakama yako?labda lije agano jipya tena.

    mahakama ya kadhi ni haki ya muislamu ambayo tanzania ilikuwepo na wakoloni waliikuta ila kwa chuki zake nyerere akaiondoa,na mpaka inaondolewa hakukuwa na machafuko ya amani kwa sababu ya uwepo wake.

    na sio kila muislamu atahukumiwa na hio mahakama eti kwa lazima bali ni kwa kukubali mwenyewe.

    na kuhusu kutumia kodi za wanachi tafadhali wadau rejeeni memorandum of understanding baina ya wakatoliki na nyerere halafu mnijibu ni kodi za nani zile.

    hakuna anayependa amani ivunjike kila mtu anapenda amani na uislamu ndio dini yenye amani na upendo.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 10, 2010

    Nimesoma mengi hapo juu hasa kutoka kwa ndugu zangu ambao nadhani si waislamu.
    Kuna kitu kimoja kinashangaza na sijui kama ni kwa bahati mbaya au ni uelewa mdogo wenu.
    1.Mahakama hii iliwahi kuwepo wakati wa mkoloni na wakati wa huyo BABA WETU WA TAIFA(punde atakuwa mtakatifu japo alikuwa kiongozi wetu sote katika nchi isiyo na dini!)
    2.Wenzetu mliosoma na wenye busara ndiyo mnaoongoza nchi hii zaidi ya miaka 50 sasa lakini hali mnaiona ya maendeleo.Sijui huo juzi wenu umeenda wapi.
    3.Kuna harakati za kuwanyanyuwa watu walionyuma katika jamii kwa sababu za kihistoria,kisiasa na hata kijamii au vyovyote iwavyo na hawa ni kama akina mama na maalbino.Hivi hawa yanapofanyika mbona hamsemi na kunungunika na je kwani nchi hii ni ya wanawake na maalbino tu? Je kwani kuna mfumo rasmi wa kuwabagua wao au inatokea tu.
    4.Suala hili lilianzishwa na Mrema na CCM wenzake na mpaka likawekwa kwenye ilani yao kwanini wasilaumiwe wao badala yake tulaumiwe sie Waislamu mbumbumbu tusiyo jua lolote maskini.
    Nadhani tuzungumze tunayo yajua na tusiwe na jazba kama Wajinga Waislamu kwani watu watatucheka wote.
    Ndiyo maana leo haishangazi kusikia mtu akisema Kikwete nchi ataifanya kama Mwinyi na anasifiwa Mkapa pamoja na EPA,Kuuzwa nyumba za Umma na mashirika yake nk.
    WAISLAMU WENZANGU POLENI.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 10, 2010

    watanzania wenzangu tujiepushe kwa gharama yoyote na political islam stereotypes.INCHI ITAWAKA MOTO

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 10, 2010

    MIMI NI MKRISTO,NAWAOMBA WAKRISTO WENZANGU MSIKURUPUKE KUCHANGIA JUU YA HII MADA,MUACHE SERIKALI IFANYE MAAMUZI YAKE MSILUMBANE NA WAISLAMU HUMU BLOGUNI! HAYA MARIDHINO NI BAINA YA SERIKALI NA WAISLAMU. WAKRISTO MSIPORIDHISHWA NA MAAMUZI MUIHOJI SERIKALI NA SI WAISILAMU.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 10, 2010

    duuh nasikitika kuwa mnaoandamana hata hamjui haswa mnataka kitu gani, je huu mfumo wa ssa umashindwa wapi kukidhi mahitaji,au dukuduku zenu? anyway wanaoandamna ndio wale waleee wankwapua humomuomo ktk maandamano, sharia ikiwepo mnakatwa mikono hiyo! hata mawazo kidogo loo! haya BAKWATA ikiitambua so what? Mumevizia eti JK kaingia madarakani atatoa upendeleo kwa uislam, duuuh la hasha, JK ni msomi na najuifahamu katiba ya nchi kwa kichwa hawezi kurupuka kama ninyi! wenye hela zao kina Bkhersa waala wametulia tuli, mnaungua jua hovyooooo!

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 10, 2010

    Tanzania kuna aina mbili ya Wakristo (1) Wakristo ambao wanaishi na Waislamu bila matatizo, hawa ni majority (2) Wakristo (minority) ambao wamekwishajenga chuli kubwa dhidi ya Waislamu na Uislamu; ni hili kundi la pili ndilo linalopinga mahakama ya kadhi ambayo haitagusa masuala ya jinai. Iweje wao wapinge chombo ambacho kitahusika na taratibu za ndoa???

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 10, 2010

    Just wanted to say that not all christians oppose the kadhi court, at least not those who know that it will not affect them. Edward M. Sinza. (safarini UK)

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 10, 2010

    mbona hawaandamani ili nchi iwe na maji safi,umeme na barabara? mjinga ni mjinga tu

    ReplyDelete
  50. AnonymousJuly 10, 2010

    Hkn haja ya kupigishana kelele na waislam,maana muamuzi wa mwisho ni serikali na km wao waislam wanataka kuanzisha mahakama ya kadhi wako huru kuanzisha kwa pesa yao na hawmuombi mtu mchango watachangishana,Serikali haina bajeti na mipango kazi yao,maana hizo mahakama za kawaida zinaishinda na mattizo kibao.Ndugu zanguni waislam chinjaneni maana hiyo kwenu ni suna.

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 10, 2010

    Am so much interested in zis isue,but am afraid wiz wats gona kam zen afta,sijajua rizonz za wa2kutaka hii mahakama,kazi zake zikoje na ufanisi wake ukitofautisha na mahakama za serikali ambazo zipo kwa sasa,na kama ikwepo,ni factors zipi zitaangaliwa ili kuamua eiza kesi isikilizwe wapi,mshtakiwa au mshitaki ndiye atakuwa na right ya kuchagua aina ya mahakama,kama m2wa upande mmoja atakuwa na uamuzi wa kuchagua mahakama,je hii haitakuwa na maana upande wa pili utakuwa kama unanyimwa haki,sabu nazani mbele ya sheria kuna haki za mshitaki na pia mshitakiwa,....etc,zen sipati picha ikiruhusiwa itakuwa inafanya kazi kwa namna gani...???
    Sio mbishani au mpinzani,ila nazani mchangiaji wa juu kabla yangu atakuwa anapotea,kwenye haya maoni huwezi jua mchangiaji ni wa dini gani no mata kasemaje,hata wewe ingawa umesema ni mkristo,unazani nani mwenye akili timamu ataamini,kwa pruf ipi,jst kuandika tu ndo2amini udini wako!!??
    Pia huwezi kuwa sure kuwa kila anayepinga ni mkristo,unazani waislam wote hili suala wanalikubali au......?????
    AM FOLOWING THOSE HU SAID,''DONT CRITISE SOMETHING ZAT U CANT PROVE OR U DONT DONT IT AT OL.''
    Niambie basi Mie niliyeandika hii coment ni wa dini gani,ukipatia zat minz nawakilisha MAJORITY HU HAV BRAINS,PEOPLE HU THINKS...!!!!

    ReplyDelete
  52. AnonymousJuly 10, 2010

    Habari za Leo wadau wote, Naomba na mimi nitoe machache kuhusu mjadala huu.

    Awali ya yote nampongeza mkuu wa police kanda ya Dar kutoa kibali cha maandamano, Maandamano ni haki ya msingi, hata hivyo, pia, Hushusha jazba ya wahusika na kuwatoa upepo huku maisha yakiendelea. mi naonelea watu wakiandamana wapewe kibali ila wachungwe wasifanye uhalifu kwa kuwa jazba zitaisha na haja ya maandamano haitafikia mahitaji ya msingi.

    Nirudi kwenye mada sasa, Chanzo cha mahakama ya kadhi Tanzania zilikuwa siasa za Mrema enzi zile akigombea jimbo la temeke,alihamasisha kuwa yeye akichaguliwa atahakikisha anashughulikia mahakama ya kadhi.
    Kuona hilo kuna chama kiliona kita loose wanachama wake hivyo kikaamua kuchomeka kipengele cha Mahakama ya kadhi kwenye ilani yake ili kiindelee kupeta,MUngu akisamehe maana wakati huo kilikuwa hakijaona Katiba ya nchi inasema nini kuhusu masuala ya dini.
    Baada ya kupima upepo mwaka huu kimechomoa kushughulikia hiyo mahakama, NAKIPONGEZA KWA HILO NA NAKIPONGEZA KIDUMU HADI MWISHO WA MAISHA yetu wote sisi watoa maoni.

    Kwa nini kimechomoa, nadhani Mahakama ya kadhi si swala la kiserikali ni la KIDINI zaidi, na nchi hii haiongozwi kidini wametambua hilo mapema.

    UGOmvi wa kidini ni mbaya na mbaya sana, hauwezi kuisha hata kidogo, Tanzania tumefanikiwa kushinda ugomvi wa kisiasa, Tushukuru hilo, maana nina hakika hata hao walioandamana jana hawajawahi kuona yanayowapata wakimbizi wakati wa machafuko, Embu ulizeni wenzenu wa kigoma na kagera wenye uzoefu na kuwaona wakimbizi watawaambia mateso wanayoyapata.

    NIGERIA, bila shaka mnaijua, kuna machafuko makali sana ya kidini, machafuko yakija hayaangalii aliyendamana na ambaye hakuandamana, ukiwa kwenye njia unakwenda, yaani unakufa. Kwa hiyo mijadala kama hii ya mahakama ya kadhi kuingizwa serikalini italeta migogoro kwa kuwa serikali haibagui wananchi wake, kwa kuwa kuna wengine hawatapendezwa na uamuzi wa upande fulani.

    Mimi naamini kwamba mahakama ya kadhi, inasistizwa iwepo kwa kuwa inatoa ajira kwa baadhi ya watu, mimi naonelea kama wanataka iwepo iwepo ila wahusika wasilipwe na serikali. Waamue mambo yao huko huko, ila wakija kwa jumuia, waheshimu wenzao kama ilivyo sasa, Tatizo ni pesa za kuwalipa kadhi au ni nini? kwa nini msichange sadaka kwa ajili ya kadhi kila ijumaa?

    Vilevile niliskia, jamaa mmoja aliyekuwa akisoma hotuba siku ile ya maandamano akisema wao wanataka mahakama ya kadhi ishughulikie Mirathi na mambo ya ndoa (Taraka), lakini hilo danganya toto, mahakama ya kadhi haishughulikii hayo tu, kwa wale mnaoelewa na mmesoma sheria za dini ya kiisilaamu zina cut across, hata mwizi atahukumiwa kwa sheria hizo kama kadhi yupo, Hivyo naamini wanatanguliza mirathi na mambo ya ndoa ili wachomekee mengine badae.

    Inabidi serikali iwe imara kwa mahakama ya kadhi, ikishakubali itakuwa ngumu kuchomoa matakwa mengine ya mahakama ya kadhi.

    lingine, ni kwamba kama mahakama ya kadhi itashughulikia mambo ya ndoa, itakuwa imeharibu kuna watu hupendezwa kuoa au kuolewa na mtu wa dini yeyote na mpaka ninapoandika huu mchango kuna watu wameolewa na kuoa watu wa dini tofauti lakini kila mtu anaabudu kwenye imani yake ya zamani kabla ya kuoa au kuolewa, mahakama ya kadhi ikija, kimbemebe kwa hao kwanza.

    baada ya kusema hayo, naomba viongozi wa dini ya kiisilamu tanzania wawafute uumini wote walioandamana kwa kuwa wamekwenda kinyume na matakwa ya viongozi wao ambao waliwaomba wasifanye maaandamano kwa kuwa swala liko kwenye mchakato. Ingekuwa DINI la dhehebu fulan, fasta walishatengwa na dhehebu hilo ili kuondoa mgongano. Embu waulize wale viongozi wa dini walioshindwa kuvumilia kuoa, wakaoa! walifukuziwa mbali kwa kuwa msimamo wa viongozi wakuu ni kutokuoa, iweje ukataze maandamano watu waandamane uwaache? Ndo maana hata vyuo vikuu wakiandamana vinara wote hufukuziwa mbali, na nyie vingozi wa kiisilamu chukueni hatua mara moja ya hao wabishi.

    Naomba kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kujiweka mbali na mambo ya dini, na msithubutu kamwe kufikilia mahakama ya kadhi kiserikali mtakuwa mmegeuza nchi kuwa ya kiisilamu.

    ReplyDelete
  53. AnonymousJuly 10, 2010

    B4sijaondoka,ningependa kujalizia kwa kufungia coment yangu hapo juu,nimejaribu kusoma coment olmost zote,baadhi yazo zina sm rules2b4folowed na adhabu kwa wavunjaji,nazani wewe kama binadamu una utashi wako,do wat U think is right4U and ur GOD,kama sheria yako inasema ukifumania kata chinja,zen chinja,ukimkamata kibaka kata mkono,jst do it,ukimkuta hata kama ni mwanao anazini piga MAWE,basi beba vitofa nawewe jiunge na wahukumuji,kwani hatari iko wapi bwana,mbona wa2miaka ya90'z walikuwa wanvisha vibaka matairi na kumaliza kesi wao wenyewe,zen wats frightens U2serve ur GOD,ukisubiri thawabu zako na MABIKIRA siku ukirudi kwa yule unayeamini kuwa ni muumba wako na uliishi kwa kufuata sheria zake na kuzisimamia ipasavyo,jst IMAGINE HOW GOOD ZAT WIL B4U ZER...,ila2sihau na wale wanaoamini kuwa akupigaye shavu la kushoto mgeuzie na la kulia,msamehe akutendaye ubaya,bkoz yupo atakayemuhukumu yeye na mtendwa pia,ya kwamba SERIAKALI ni moja mamlaka za MUNGU kusimamia na kuongoza wa2wake,..etc,vp nao wakianza kuisist uwepo wa system itakayooparet kufuatana na imani yao,si itakuwa balaa sasa ktk nchi????
    MWISHO,KWA MICHUZI,PENGINE UNGEIWEKA HII ISUE INTERMS OF MAADA ILI WA2WACHANGIE,NA SI IISHIE HEWANI NA HII HABARI YAKE,ZEN MAONI YOTE YAPOSTI KWA KIKWETE NA JOPO LAKE KULE MJENGONI B4UCHAGUZI!!!!

    ReplyDelete
  54. AnonymousJuly 10, 2010

    ...NAKUULIZA YA NGOSWEEEEE.......?

    ReplyDelete
  55. AnonymousJuly 10, 2010

    JAMANI MBONA UWANJA UMECHAFUKA....KWANI HAWA WATZ WENZANGU WAMEKOSEA NINI KUANDIKA JIHADI????NATAKA KUULIZA HILI NENO JIHADI LINA MAANA GANI.....MAAANA WATU WANAKURUPUKA NA KUANDIKA UTUMBO USIOELEWEKA NA HATA WAISLAMU WENGINE HATA HAWAJUI IMEKUSUDIWA KITU GANI.......KUNA JIHADI KUBWA ZAIDI YA NAFSI????????????SASA SIONI KAMA WAMKOSEA AU JAMANI MMEFAHAMU UGAIDI NA MISHALE NA BUNDUKI.????TUFAHAMU MANA KABLA YA KUDANDIA MANENO. PILI WADAU WANAOISHI UGHAIBUNI INAONEKANA HATA MKIKAA MIELE YAWEZEKANA HAMTOKUWA NA USTAAARABU..YAWEZEKANA MUKO BRAINWASHED KAMA WENGINE WANAOAMINI AFRICA UKIJA UKITOKA AIRORT BASI UTAKUMBANA NA WILD ANIMALS.....JIREKEBISHENI AFRICA INA WASOMI WENGI NA WENYE AKILI...UKIFAHAMU USEMI USEMAO MUNGU HAKUPI YOTE NDI UTAJUWA NAKUSUDIA NINI.ILA KUMBUKA HUNA HAJA YA KUPATA SOMO MPAKA KUWE NA DARI AU BATI JUU.

    ReplyDelete
  56. AnonymousJuly 10, 2010

    NAPENDA KUTOA HONGERA KWA WOTE WALIOCHANGIA MADA HII, PIA NAPENDA KUTOA FUNDISHO FUPI KWA WALE WALIOTUMIA LUGHA MBAYA. NINACHOTAKA KUSEMA MIJADALA KAMA HII INATAKA SANA KUTUMIA MANENO MZURI NAYAMAFUNDISHO KWA DINI ZOTE MBILI. MAANDAMANO YANAWEZA KUA NIMAZURI KWA JAMII AU SIMAZURI KWAJAMII, TUNACHOTAKIA NI KUJADILI KATIKA KULEA MAFANIKIO NA MAFUNDISHO FOR OUR COUNTRY.

    ReplyDelete
  57. AnonymousJuly 10, 2010

    MAHAKAMA YA KADHI NI RUKSA KAMA TU ITAKUWA NDANI YA DINI NA INAKUWA FUNDED NA SADAKA ZA WAUMINI SI SERIKALI, KWANI SERIKALI HAINA PESA KIASI KWAMBA IMESHINDWA KUPANDISHA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WAKE NA PIA KATIBA INASEMA SERIKALI HAINA DINI NA PIA SERIKALI TAYARI INA MAHAKAMA ZAKE, SIDHANI KAMA INAHITAKI MAHAKAMA ZA KADHI KAMA SERIKALI, NA IKITOKEA PIA KUNA UWEZEKANO WA DINI ZINGINE KUDAI FUND TOKA SERIKALINI NA ITAKUWA HAKI YAO KUFANYA HIVYO WAKINYIMWA ITAKUWA UBAGUZI. MIMI NINAVYOAMINI TAYARI DINI ZOTE ZINA MAHAKAMA ZAKE NA ZINASIKILIZA KESI MBALI MBALI, HATA DINI ZA KIKIRSTO ZINA MAHAKAMA NA ZINAWAPATANISHA WATU KILA SIKU.

    ReplyDelete
  58. AnonymousJuly 11, 2010

    ASSALAAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU.
    Amani juu yenu kwa rehema za mwenyeezi mungu na mbarikiwe.

    Nyie mnaoandamana kuipinga Bakwata kwa kutumia sababu za kidini mnakosea, na nyie mnaotukanana humu vile vile mnakosea.

    Tanzania yetu ni ya amani hatuna udini wala ukabila, tuache hizi nuksi zinazochochewa na wasiopenda amani.

    Ya Rabbi tustiri, na utuepushe mabaya.

    Amin.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...