memba wa benchi la ufundi la simba. toka shoto ni kocha msaidizi na mchezaji wa zamani selemani matola, meneja wa timu innocent njovu na kocha msaidizi na mchezaji wa zamani amri saidi, wakiwa wameulamba wakati wa sherehe za Simba Day juzi. kumbe inawezekana benchi la ufundi kuwa smati kama wenzetu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Wewe Matola na Amri acheni uzembe, mmeacha kucheza mpira juzi tu sasa mmeshaota vitambi? Embu jiwekani fit bwana, fanyeni mazoezi na kula diet kama wachezaji wenu. Hii itawasaidia kujenga afya zenu na kufurahia zaidi maisha yenu.

    Ni vizuri pia kuona wachezaji wa zamani wanachukua mkoba wa kuendeleleza vipaji vya wachezaji wa sasa. Hapo nawapa hongera.

    ReplyDelete
  2. shua, wanapendeza sana nafikiri waendelee hivohivo wawe mfano kwa wenzao na wengine tujifunze toka kwao.

    ReplyDelete
  3. Yah,inawezekana ila tatizo la huku Bongo ni joto sana,kwa hiyo kuvaa hivyo wakati wa mechi inatesa sana.Tusige kila kitu ligi ya Ulaya inaanza Agosti(Joto linapoanza kupungua na kuendelea hadi mei kabla ya joto(summer) kuanza).
    Wao Ulaya wanachofanya ni kuepuka joto.Kwa hiyo kwa wenzetu inawezekana.

    ReplyDelete
  4. Kuiga mavazi ya Nje si Ndio Kuwa Smart. Hata wangekuja na Vazi la Kimasai ni Smart tu.

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli watanzania wote ukiondoa mababu wa zamani, kama kuna kitu hatujui na hatujali ni mavazi, hasa wanaume. Hatuko sensitive na matukio, mahali tulipo, na muda vitu ambavyo vinachangia saana maamuzi ya mavazi ya kuvaa. Unakuta kwenye harusi mtu kavaa T-shirt! Kanisani mtu kavaa track suit.., mkutano wa high level mtu kavaa casual, wachezaji wengi nikionana nao mtaani muda si wa mazoezi bado unakuta wameng'ang'ania mabukta na mashati ya mpira. No wonder makocha wetu hawajifunzi kupiga pamba kama hivyo uwanjani. Au ni kwa sababu hawaitwi mameneja kama kwa wenzetu? Meneja utavaaje track suit au kaptula ofisini!!?? Wabongo tuache ushamba. Labda tungekuwa na vazi la kitaifa ingeeleweka.

    ReplyDelete
  6. Bongo joto kaali halafu hauna usafiri unaishia kwenye daladala sasa suti wapi na wapi.

    ReplyDelete
  7. annon Tue Aug 10, 01:11:00 PM
    ilo nalo neno kwakweli,maana mie sielewi kabisa wanaume mnanovaaga!

    mweee

    ReplyDelete
  8. Mimi wala sifagilii watu wanaosema wabongo hatujui kuvaa. Nimekaa huku zaidi ya miaka 16 na nimebahatika kutembelea nchi kadhaa na ninakwambia kama hujui kitu kaa kimya...Sio vyote ni kweli vinavyoonekana kwenye TV...Hata huku watu wanavaa vitu vya ajabu sana tu na kuna watu. Mimi naona as long whatever you put on is clean and you are comfortable go for it. Kama sherehe haijaweka dress code kwanini mtu uende umevaa vitu ambavyo hauko comfortable na wakati nyingine unaweza kuwa overdress. Kama sherehe imeagiza watu wavae business attire halafu mtu akaja casual hapo ndio nitashangaa. Umeshaenda harusi za summer huku??? Wageni wamevaa flip flaps na vi sun dress halafu hapo utasema hawajui kuvaa????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...