Marehemu Felix Matela
enzi za uhai wake

MSIBA WA MWANAFUNZI WA KITANZANIA ALGERIA

Uongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa kitanzania wanaosoma nchini Algeria (ATSA), wanasikitika kutoa taarifa ya kifo cha mwanafunzi mwenzao ndugu Felix Matela, kilichotokea siku ya tarehe 05/08/2010 Jijini Algiers nchini Algeria .

Ndugu Felix alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Houari Boumediene (USTHB) Kilichopo jijini Algiers , Algeria . Alikuwa akiishi katika Hostel za chuo zinazotambulika kwa jina la CUB 3.

Uongozi unatoa shukrani za dhati kwa wizara ya elimu na ufundi na ubalozi wa Tanzania-Paris, Ufaransa kwa ushirikiano wao mkubwa katika kuhakikisha usafirishaji wa mwili wa marehemu kurudishwa nyumbani unakamilika pia uongozi unatoa shukrani kwa serikali ya Algeria kwa kujitolea kusafirisha mwili wa marehemu mpaka Tanzania.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa hivi karibuni mara tu taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu zitakapo kamilika .


Tunawasihi familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehem.

Uongozi – ATSA.
00213551713920,
00213553271791
tz_students@yahoo.fr

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. rest in peace ma best friend,,,!we wl be missing u man kule kwenye mijengo yetu,,,

    ReplyDelete
  2. jamani poleni sana, du! Mungu alinze roho ya marehemu mahali pema peponi.
    Jamani mbona hamjatuambia alikuwa anasumbuliwa na nini hasa.

    ReplyDelete
  3. Poleni wafiwa...and may God rest his sould in piece

    Ilikuaje???ni nini kilichompata mwenzetu....???

    ReplyDelete
  4. Man!!Rest in Peace!!,Du,Man I remember I met ya two dayz bfr what u did? Man Why didn't u tell me!! U were goin' to do that Stuff!,''QUE DIUE TE BENISSE!!n' Rest ya in PEACE!,I'll alwayz remember ya!!

    ReplyDelete
  5. Eh RIP matela jamani lini analetwa huku ili tuweze kuhudhuria mazishi yake?

    ReplyDelete
  6. may his beloved soul rest in peace; Amen

    ReplyDelete
  7. Michuzi,

    hebu tuambie nini kilichomuua huyu jamaa. i wont to know..... Nini kimemuua. i was been in Algeria past nine years ago. Naomba ututaarifu the course of his death... mtu huwezi kufa with no reasons

    ReplyDelete
  8. Wananchi, inabido samtaimz tukubali matokeo tu. Haitageuza ukweli iwapo tutaanika sababu za kifo katika mabulogu, hata kama uliwahi kuwa Algeria miaka iliyopita!

    Muhimu ni kumuombea marehemu apunguziwe adhabu za umauti, basi.

    Mdau, El Djazair - El Djazairia

    ReplyDelete
  9. MUNGU amlaze maala pema peponi, tulikuwa pamoja O'level KOLILA HIGH SCHOOL

    ReplyDelete
  10. inna lillah wa inna ilaih rajiuun!

    ndugu yangu Felix nitakumiss daima, tulisaidiana mengi sana tukiwa pamoja pale Blida tukisoma kifaransa... inauma sana kuona umetutoka kwa njia hiyo!

    jamani wadau wote tuliopo Algeria tusichoke kumuombea dua mwenzetu, na tusipende sana kumjudge.. tukumbuke kuwa sote ni wa mungu na kwake sote tutarejea!

    mdau,
    Algiers, ALGERIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...