Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa pool Tanzania (TAPA),Isack Togocho (kati) akizungumza leo wakati wa utambulisho wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Pool,Denis Lungu (kushoto) toka nchini Zambia.kulia ni Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa Pool Tanzania (TAPA),Amos Kafwinga.
Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Pool,Denis Lungu toka nchini Zambia akiongoe na wanahabari (hawapo pichani) waliofika katika hafla ya utambulisho wake leo katika kijiji cha Makumbusho,Kijitonyama.kulia ni Mwenyekiti wa chama cha Pool Tanzania,Isack Togocho na kushoto ni Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Zambia nchini,Sunday Chikoti.
picha ya pamoja,toka kulia ni Katibu mkuu wa mchezo wa Pool Tanzania,Amos Kafwinga,Meneja wa Kocha mpya wa timu ya Taifa,Bw. Stanlas Chisanga,Kocha wa timu ya Taifa,Denis Lungu,Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Zambia nchini,Bw. Sunday Chikoti na Mdau wa Pool,Bw. Innocent Melleck mara baada ya hala ya utambulisho wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Pool uliofanyika leo katika kijiji cha Makumbusho.

==========================

Chama cha mchezo wa Pool Tanzania (TANZANIA POOL ASSOCIATION- TAPA) kwa kushirikiana na mdhamini mkuu wa chezo huo wa pool nchini Bia ya Safari Lager, inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imemtambulisha rasmi kocha mpya wa timu ya taifa ya mchezo huo kutina nchini Zambia,Bw. Denis Lungu kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia tarehe 01.08.2010 mpaka 28.07.2012.

Lengo la kumleta kocha huyu ni kama inavyoeleza katika katiba kuwa chama kitasimamia na kuendeleza mchezo wa pool table Tanzania na kwa kuzingatia jukumu hilo zito, Chama cha Pool Tanzania kwa kushirikiana na mdhamini wao mkuu wa mchezo wa pool table nchi,Safari Lager waliamua kumleta kocha huyo ili kuhakikisha kwamba mchezo unachezwa katika kiwango cha juu hapa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu mkuu wa chama cha pool Tanzania,Bw. Amos Kafwinga alisema “Ni azma ya Chama cha Pool Tanzania kuhakikisha mchezo unachezwa kwa kufuata sheria na viwango vinavyoeleweka ili mchezo uwe na ladha na hata mtazamaji afurahie kuangalia ili kutekeleza vyema hazma ya mdhamini wetu Safari lager ya kuleta mapinduzi ya kweli na mafanikio makubwa katika mchezo wa Pool hapa nchini.

Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA),Bw. Isack Togocho amewasihi wachezaji wa timu ya Taifa na watakao teuliwa katika timu ya taifa wamtumie vyema kocha huyu ili kukuza viwango vyao na hatimaye waweze kupata nafasi ya kusajiliwa katika vilabu vya kulipwa nje ya nchi. Pia aliwaasa sana wale wote watakaopata bahati ya kufanyan kazi na kocha huyo katika kipindi atakachokuwa nafundisha watumie nafasi hiyo vizuri kwani ni nadra sana kurudi tena.

Mwisho, kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA),Bw. Isack Togocho alitoa shukrani zake za dhati kwa Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kwa mchango wake wa dhati kwa mchezo huo kwa kusema,”Tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa bia ya Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa mchango wao katika kuhakikisha mchezo huu wa Pool unakuwa na kupata hadhi ya juu hapa nchini na kumpongeza sana meneja wa Bia ya Safari Lager Ndugu Fimbo Butallah kwa kuwa bega kwa bega na mchezo wa pool Tanzania.

Kwa kweli TBL kupitia BIA yake ya SAFARI LAGER wamekuwa Ni mfano mzuri katika udhamini Kwa kutekeleza ahadi Na kutoa ushirikiano mkubwa katika mchezo huu, na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hata mchezo wa pool kocha anatoka nje ya nchi tena Zambia, ni lini na mchezo gani watanzania watakwenda kufundisha nje ya nchi? Hivi tunajivunia mafanikio yapi?

    ReplyDelete
  2. Jamani TANZANIA, ni kweli tunahitaji kocha wa POOL TABLE toka Zambia? kweli fikra za kikoloni zimetujaa vichwani mwetu, ehe Mungu tusaidie

    ReplyDelete
  3. Sasa hii imezidi kiasi, mnatutukana sana Watanzania nyie viongozi wa vyama vya michezo. Na wizara ipo na inaona sawa tu, tena nadhani ndio inayosaidia vyama vya michezo katika kututukana Watanzania.

    ReplyDelete
  4. Duuhhh, nnashindwa kuamini ninacho kisoma hapa, yaani hadi kocha wa pool Table anatoka Zambia??? kwakweli inatia uchungu sana. Nazani watanzania tumerogwa na mchawi wetu alisha kufa.
    Eee Mwenzi MUNGU tunakuomba uturehemu.

    ReplyDelete
  5. Jamani mpaka pool ?????

    Kweli aliyesema ..Watanzania aliyeturoga kisha kufa hajakosea!

    Tudanganywe na uchumi bomu ,uongozi ovyo,eti kilimo kwanza-wakati maembe yanaoza lushoto, eti tumia chandarua-wakati mazalia ya mbu wanayaacha, eti zungumza na umpenda kwa msaada wa marekani- mmh , wakati marekani ndoa ziongoza kwa vituko na kuuna!!, kwani sisi hatuwez kuozungumza na wapenzi wetu mpka msaada wa marekani ???

    upuuzi wote huo na sisi tunakubali tuuu!! mmh! kweli tumelogwa!!

    Na hii ya kocha wa pool ndo kibo zaidi! mmmmh yangu macho tu!!!

    ReplyDelete
  6. kabla sijawasoma nilikua na ili wazo:
    ili wimbi la wazimbabwe na wazambia kujaa Tz kulikoni???naona wameshika hatamu kwelikweli thz dayz

    ReplyDelete
  7. mimi jamani nimempenda juyo kocha , yuko handsome kweli ....au mnasemaje ?

    ReplyDelete
  8. Watanzania wenzetu walio katika nafasi za kufanya maamuzi (yenye athari kwa waananchi wengi) ndio wanaoimaliza Tanzania. Wengi wako katika nyadhifa ambazo laiti kama wangezitumia vizuri basi zingeleta mabadiliko makubwa sana, na faida kwa wananchi wengi wa kawaida wa Watanzania. Hata angeletwa kocha wa Pool kutoka Ulaya! mchezaji wa kitanzania akishajua kucheza pool ndio nini!!?? mtu mzima anayejiita 'mdhamini' anaamka asubuhi anapeleka wazo kwa wakuu wake kwamba kampuni idhamini mchezo wa pool!!??? kwa faida gani!?? Haingii akilini kabisa!!!Huu mchezo una faida gani kwa jamii yetu watanzania??!!! Hivi kuna siku kweli tutaamka tukiwa na majuto kwamba watanzania hatujui kucheza pool????!!!! Kiongozi wa chama anawahimiza wachezaji watumie fursa ya ujio wa kocha kutoka Zambia ili waujue vema mchezo wa pool. Wakishaujua ndio ILI IWEJE!!!??? Yote haya ni kwasababu akili za hawa watu zimejaa matope, haziwezi kufikiri vitu vya maana.
    Kama ni wadhamini kwanini msidhamini vitu vya maana??? Mfano; Dhamini watoto kumi bora (Mfano wasichana) wanaofanya vizuri katika mitihani kama ya darasa la saba, kidato cha nne, cha sita, n,k au dhamini mashindano kwa ajili ya kujenga na kuendeleza vipaji vya watoto kama riadha, kuogelea, muziki, kusoma mashairi, ngoma n,k. Unapofanya hivyo sio tu unamsaidia mtoto/mwananchi mmoja mmoja binafsi, bali unaleta mabadiliko kwa taifa lote la Tanzania kwa ujumla. Ina maana baadaye utakuwa na Taifa lililojaa wanamichezo wenye vipaji ambavyo wewe, mdhamini au kiongozi wa chama umeviedeleza. Kuna mengi sana ambayo Tanzania inahitaji kudhaminiwa na maeneo mengi sana ambapo fedha zinahitajika. Tumieni muda kufikiri vizuri ili mje mtoe maamuzi mazuri. KAMA MMESHINDWA KUFIKIRI VITU VYA MAANA OMBENI MSAADA WA MAWAZO - LAKINI SIO MCHEZO WA POOL.

    ReplyDelete
  9. DUH KAAZI KWELIKWELI..YAANI KUNA KOCHA NA MENEJA WA KOCHA ..TEH TEH

    ReplyDelete
  10. Huyo kweli handsome, apelekwe zenji yakheee!

    Ataweza kucheza pool la mombasa huyoo?

    ReplyDelete
  11. Jamani sasa hii ni too much huyo jamaa si kocha wala nini mi nshacheza nae sana pol pale Jolly yaani hamna kitu. Watanzania vipi jamani???????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...