Sehemu ya wajumbe wa vyama wanachama wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho nchini wakipiga kura zao kwenye ukumbi wa BASATA leo kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa muda wa shirikisho hilo.Sekretarieti ya Uchaguzi huo ikiwa makini ili kuhakikisha kura hazichakachuliwi.Kutoka Kushoto ni Agnes Kimwaga, Alistide Kwizela na Mzee Mayanga wa BASATA. Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego (kushoto) akimpongeza mshindi wa Nafasi ya Makamu wa Rais na ambaye pia ni Mkufunzi wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo,Bw. Abraham Bawadili.Kulia ni Mkongwe wa Sanaa za Maonyesho,Mzee Nkwama Bhalanga ambaye ameshinda nafasi ya ujumbe.Viongozi waliochaguliwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo pia wasimamizi wa uchaguzi huo.Katikati waliokaa kwenye viti ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo,Dkt.Hebert Makoye.


Na Alistide Kwizela

Mkakati wa kuyawezesha na kuyapa nguvu mashirikisho ya wasanii nchini leo umeendelea tena ambapo shirikisho la Wasanii wa Sanaa za Maonyesho limefanya uchaguzi na kujipatia viongozi wake wa muda watakaoliongoza jahazi kwa mwaka mmoja.

Katika uchaguzi wa leo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa,BASATA na kusimamiwa na Mkuu wa Idara ya Sanaa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt.Hebert Makoye,Bi.Agnes Lukanga aliibuka kidedea katika kiti cha urais baada ya kuwashinda wapinzani wake ambao ni Alex Mwakabama (6) na Denis Mango (6).

Ushindani mwingine ulikuwa kwenye kiti cha Makamu wa Rais ambapo, Bw.Abraham Bawadhil ambaye ni Mkufunzi katika Taasisi ya Sanaa Bagamoyo TaSUBA aliibuka mshindi baada ya kumuangusha Alex Mwakabama aliyeambulia kura 6 pekee.

Aidha,nafasi ya Katibu Mtendaji ilinyakuliwa na Denis Mango aliyepata kura 15 dhidi ya tatu za Irene Sanga huku nafasi ya mweka hazina ikichukuliwa na Mary Mwangato aliyepata kura 9.Nafasi za ujumbe zilienda kwa Alex Mwakibinga, Nkwama Bhalanga na Mahadia Ally.

Baada ya uchaguzi kumalizika, jopo la usimamizi likiongozwa na Dkt.Makoye lilitoa nasaha kwa viongozi kwa kuwataka kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kulifanya shirikisho hilo kusimama na kuwa na nguvu pia kujenga umoja miongoni mwa wasanii wa sanaa za maonyesho kwa ajili ya utetezi wa haki na maslahi yao.

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego aliwaeleza viongozi kwamba, kazi kubwa ya shirikisho hilo ni kufufua nguvu ya sanaa za maonyesho ambazo katika siku za hivi karibuni imefifia kutokana na ujio wa teknolojia mpya.Alisema kwamba, leo hii hakuna sehemu mtu anaweza Kwenda kuangalia ngoma, maigizo, sarakasi nk. na hii ni kutokana na wadau kulala,hivyo shirikisho halina budi kuja na mikakati ya kukuza sanaa hiyo adhimu.

Naye Mlezi wa Mashirikisho ya Wasanii,Mzee Rashid Masimbi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya BASATA alisema kwamba, kazi iliyoko mbele ya shirikisho hilo ni kuja na mpango kazi kabambe, kuandaa kanuni za kuliongoza shirikisho, kutafuta ofisi, kuongoza wanachama wapya na kusaka fedha kwa ajili ya kuendesha rasmi shughuli za shirikisho.

Kesho ni zamu ya Shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu) ambapo litapata rasmi viongozi wake na kuanza safari ya kuandika historia mpya katika tasnia ya sanaa nchini.Wadau wote mnakaribishwa sana kushiriki.Matokeo yatamwagwa hapahapa kwenye libeneke la jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mnataka kutafuna tu pesa za wasanii !! kuna humuimu gani wakuwa na ma vyama kibao ya wasanii !! tumo moja hikusanye mapato na kuangalia haki za wana sanaa !1 sanaa ni sanaa music wapiga sarakazi zote sanaa tu!!
    ache kuzuga watu ! kwanza sizani nyie wazee mnajua chochote kuusu music !! sorry hila ndo kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...