Aisha Mashauzi (kuume) akitesa huku wadau wakimpa tafu
Katika kusherehekea Eid el FitrJumuiya ya watanzania ugiriki kwa kushirikiana na sponsors LELA NA KITOGO tulifanikiwa kuwafurahisha watanzania pamoja na baadhi ya ndugu zetu wa Kenya na marafiki wa Ethiopia katika mkesha wa Jumamosi 11/09/2010..
Mashauzi alifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno kuwafanya wahudhuria wasiweze kutulia na hasa kina mama.Mashauzi alielezea furaha yake kubwa jinsi watanzania wa ugiriki wanavyoshikamana na aliwaomba waendeleze moyo huo ."Najihisi kama nipo nyumbani kwa jinsi nilivyowakuta ndugu zangu mnavyoishi kwa maelewano kiasi hiki.Sikuwa najua kama mpo wengi na mna ushirikiano namna hii ' Alisema akiwa jukwaani kabla hajaanza kufanya vitu vyake na kushangiliwa na kupigiwa makofi na umati wa watu waliofurika katika ukumbi huo.

Kabla Mashauzi hajapanda jukwaani kikundi kipya cha watoto wetu KASSIM, MLOSI,FEYSAL,SELE na RUMINA (kilichozinduliwa hivi karibuni na Meneja ALI NYAU ) kilitumbuiza na kushangiliwa. Bofya hapa kwa picha za ziada

palikuwa hapatoshi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Yah, dunia sasa imerudi kwenye muhimili wake...hapatoshi!

    ReplyDelete
  2. Hivi huko ugiriki sasa kuna watu wengi namna hii?Naona kina dada ni wengi na wanapendeza mno . Enzi zetu hapa kulikuwa na meli tu na mabaharia wa kumwaga. Mungu awabariki na mzidi kuleta waimbaji na hata kama mnataka mimi nitawaleteeni Dogo Mfaume XMAS !!

    ReplyDelete
  3. can somebody say cleavage.

    ReplyDelete
  4. hao wanawake ndio ma baharia wenyewe siku hizi ugiriki.

    ReplyDelete
  5. wajemeni kumbe wanawake watanzania wakoge wengi hivyo ugiriki, Ndo maana sisi wengine hatupati wachumba huku Amerika.
    vijisichana virivyoko huku vinaringa kama nini,MMWEE!!!!

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaa aliesema CAN SOMEBODY SAY CLEAVAGE anakusudia nini hasa?

    ReplyDelete
  7. ongera sana ugiriki kwa kuwa na wachumba wazuri kama jinsi ninavowaona hapo pichani!!!! big up.... vipi lakini hapo umangani mmanga anatoa karatasi au??????

    ReplyDelete
  8. labda kwanza utafute maana ya cleavage halafu angalia tena picha zote.

    ReplyDelete
  9. wamanga karatasi HAWATOI.... ni usumbufu tu kuishi kule na hao wanawake ni wakubwa sana sio watoto naona kwenye miaka ya 35

    ReplyDelete
  10. Cleavage ! hivi sidiria hakuna au mamabo ya kutegana?..... wanawake kweli ni mthani!!!

    ReplyDelete
  11. ha ha ha! he he he! sidiria bei mbaya wanunulie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...