East Africa Television (EATV) itazindua kipindi kipya cha luninga kiitwacho Wanawake Live siku ya Jumanne ya tarehe 14/ 09/ 2010 saa tatu kamili usiku.
Kipindi hiki kinalenga kuwajengea wanawake uwezo wa kutambua haki zao za msingi kiatika kupata huduma bora za afya ya uzazi, uzazi salama, pamoja na haki mbalimbali za kisheria anazostahili mwanamke wa Afrika Mashariki katika kujiletea maendeleo yake.
Ni jukwaa la aina yake litakalowakutanisha wanawake wa rika, elimu na kada mbalimbali katika jamii, wakibadilishana mawazo ya jinsi ya kuchangamkia fursa za kijinsia na maendeleo katika nyanja mbali mbali za kimaisha.
Wanawake Live ni kipindi kitakachowapa wanawake ufahamu wa masuala mbalimbali ya sheria na haki za binadamu, kwaelemisha wazazi watarajiwa (wasichana) umuhimu wa kuepuka mimba zisizotarajiwa pamoja na kujiepusha na ngono zembe.
Kipindi kitakuwa na muundo wa mjadala ambapo Mwongozaji atakuwa akimhoji mgeni mmoja atakaealikwa katika kila moja ya vipindi vya Wanawake Live.
Mahojinao yao yatakuwa ni ya kujenga zaidi yakihusisha maisha binafsi ya mgeni mwalikwa kiuchumi, kijamii na hususani uzoefu alionao mgeni huyo pamoja na changamoto mbalimbali alizozipitia.
Mbali na mahojiano kuhusu maisha binafsi, kutakuwa pia na mjadala kuhusiana na mada maalumu mara moja kwa mwezi ambapo mtaalamu wa fani husika ataalikwa kuzungumzia fani ya mada husika. Mada zote zitahusiana na masuala ya kijinsia yanayolenga kuelimisha na kuipa jamii taarifa muhimu zinazohusiana na changamoto zinazomkabili mwanamke wa Afrika Mashariki.
Wiki iliyopita EATV ilianzisha kipindi kipya cha uchaguzi kiitwacho 'Uchaguzi Express', kinachorushwa kila Jumatatu na Alhamisi saa 3 usiku.
Na sasa EATV inawaletea watazamaji wa Afrika Mashariki Wanawake Live, kila Jumanne saa tatu kamili usiku.
Alex Galinoma
Promotions & Campaign Coordinator

Lakini wanawake wengi wanaoteseka na hayo mambo ya uzazi etc wako vijijini hata umeme hawana ndo watakuwa na TV?
ReplyDeleteWazo zuri lakini naona kama walengwa hasa hawatafikiwa.
KILA LA KHERI