Chipukizi wa CCM akimkaribisha maua mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipowasili huko Ndungu,wilayani Same jana mchana na kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wakazi wa mji wa Same, Mkoani Kilimanjaro jana jioni.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Kikwete akiwahutubia wanachama wa CCM wakati wa mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa michezo mjini Mwanga,Mkoani Kilimanjaro
Baadhi ya wananchi wa Ndungu Same wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete waakti alipohutubia mkutano wa Kampeni.picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Yaani hayo maua mbona hayakufunguliwa kabisa? nyie watani vipi jamani?

    ReplyDelete
  2. michuzi kha unajua kurusha roho wenzio, sasa nikikutolea sehemu aliyotoka mkeo si roho itapaa,. boyfriend wangu ni mpare na mimi sijamuona siku nyingi nipo ukerewe nasoma basi nimefarijika, msinishambulie wadau ila imeniuma nampenda sana sitaki mzungu kabisa. nashukuru kaka yangu

    Manchester,UK

    ReplyDelete
  3. Dr Kikwete give me a break, he can not even debate

    ReplyDelete
  4. same kulivyo na ukame wamepata wapi maua? hivi ametekeleza ahadi yake ya 2005 kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya mkomazi,ndungu,gonja,same?

    ReplyDelete
  5. jamani naomba mnifahamishe mana nimechunguza sana misafara ya rais wetu katika kusaka kura kila anapoenda kuna wanajeshi sasa kampeni za vyama vya siasa na wanajeshi wapi na wapi au mi ndo sielewi naomba msaada wadau

    ReplyDelete
  6. mimi ninataka kufungua kesi dhidi ya mwenyekiti wa wama ambaye ni mke wa raisi kwa matumizi mabaya ya pesa za umma kumfanyia kampeni mume wake, ninaomba maoni ya wadau licha ya kwamba nina uhakika mahakama haita nipa haki.

    ReplyDelete
  7. Huyu Fred Maro si ni mpiga picha wa Ikulu, sasa huko kwenye kampeni za CCM anatafuta nini? Analipwa na nani kuzunguka huko na mgombea wa CCM? Au CCM wamemkodi kwajili ya kazi hiyo, na kama ni hivyo ina maana amechukua likizo. Nisaidieni wadau

    ReplyDelete
  8. Siku hizi wazee wa kijitonyama nao wanavaa sare za chama? suti zikowapiiii

    ReplyDelete
  9. Shikamoo kaka,
    japo najua huwa unaitangaza hii kuwa ya jamii, na kukana blogu hii kuwa inapendelea chama fulani au la ila ankal kipindi hiki cha uchaguzi kinatusaidia kujua kuona ambayo hayasubiri mpaka uulize..... kazi njema

    ReplyDelete
  10. MWISHO WENU UMEKARIBIA WEZI WAKUBWA, JAMANI TUJITOKEZE KWA WINGI OCT 31 ILI KUWAWAJIBISHA MAFISADI KWA NJIA YA SANDUKU LA KURA NA TUSHIRIKIANE KUZILINDA KURA ZETU

    ReplyDelete
  11. JAMANI NAOMBA KUULIZA HUYO MWANAJESHI ANAFANYA NINI HAPO KWENYE SHUGHULI ZA CHAMA CHA SIASA?

    ReplyDelete
  12. nyie chadema usiojua siasa na kudandia vit nyamazeni,eti mwanajeshi,ina maana hamumjui hata bodyguard wa rais,huyo ni bodyguard wa rais,sema akiwa mikoani ndo anavaa hivyo,akiwa sehemu maalum anavaa ile suti ya jeshi.na bodyguard wa rais ni lazima awena cheo ndani ya jeshi.inaonesha ulivyokuwa na akili ya la saba kama mgombe mwenza wenu.

    ReplyDelete
  13. mhh mumetutia aiu wapare maua gani hayo

    ReplyDelete
  14. Si unaona Ras makunja uzalendo unavyokushinda! wenzio wote hapo wamevaa sare za sisiemu!wewe upo mbele na pamba za gwaride gwaride na kikifia chako cha kutishia wengine amani! kamanda jaribu kubadili tabia zako

    ReplyDelete
  15. sasa ras makunja hiyo ni tabia gani?mbona wewe umevaa nguo tofauti na wenzio?

    ReplyDelete
  16. Jamani makamba naomba unisaidie, ras makunja ndio nani nashindwa kuelewa.

    ReplyDelete
  17. mdau seba umenena hasa ikiwa debate ya kiinglish ni ishu anakuwaga mnyonge kweli!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...