Mwenyekiti wa Kamati ya kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu 2010, Mh. Abdulrahman Kinana, akionesha baadhi ya stakabadhi za malipo yaliyofanywa na CCM kukodi ndege ya Serikali kwa ajili ya safari za Mama Salma Kikwete, mke wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete, alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya makao makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, leo.
credit source: http://www.wavuti.com/



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Hizo invoice zina walakini. Mbona zote zinasema 5 hours ? Inamaana yuko so specific kutumia muda uleule popote pale aendapo bila kujali urefu wa shughuli na urefu wa safari ?
    Hivi hizo ndizo risiti za serikali yetu ? Bora na sisi wananchi sasa tunaweza kujua ni kiasi gani serikali haiko makini.
    Hiyo risiti hata mtoto wa darasa la tano anatengeneza.
    Kinana njoo na kitu kingine, hapo bado hatudanganyiki.

    ReplyDelete
  2. hah ahahah kwa hela hiyo mbona wengi tutakodi hiyo ndege what a joke...

    ReplyDelete
  3. watanzania ammmkeni hii inaumiza sana roho ukiona watu wanataniwa kama watoto wadogo...yaani tshs 15,000 ndio bill ya nini hiyo

    ReplyDelete
  4. Mtakodishaje ndege ya serikali?

    Wapi ilionyesha kuwa hiyo ndege itakodishwa? Ni nani alitoa hiyo idhini? Ndege imenunuliwa kwa matumizi ya serikali leo inakodishw ani wapi panaonyesha hiyo ndege inaruhusiwa kukodishwa. Kulipa bills sio taabu ina maana kila mtu anaruhusiwa kuikosiha sasa au ni huyo mama tu??

    ReplyDelete
  5. Kinachoshangaza, inamaana hiyo Agency inawateja wengi kiasi hicho? Fikiria kwa wiki mbili tu risit number zinatofauti ya number 500, je hawa wote ni wateja?

    ReplyDelete
  6. Kuna maanon wawili hapo juu wanadhani hizo ni Tshs.

    Hapana. Ni USD 15,000. Haya kama mnaweza nendeni na nyie mkakodi.

    Ila kwa upande mwingine serikali ilisema marufuku kutumia dola Tanzania lakini cha kushangaza serikali yenyewe inakodisha ndege zake kwa kutumia dola.

    Kwani wangeandika bei ni Tshs. 22,500,000 kungekuwa na ubaya?

    ReplyDelete
  7. someni vizuri hiyo ni dola na sio shillingi ya Tanzania, si kama hawana akili hivyooooooo! kuwa wakajitie kitanzi wenyewe kwa kuonesha wamekodi ndege kwa Tsh 15,000. Kufeli nje nje!!!

    ReplyDelete
  8. ni dola 15,000 jamani sio tshs

    ReplyDelete
  9. Hayo ni baadhi tu ya mabo ya hovyo hovyo yanayotekelezeka na serikali yetu. Mwezi uliopita nilikuwa ng'urdoto na kuna mgeni alitaka kulala kwenye quaters anazofikiaga Rais kama mgeni wa kawaida. Akapewa bei lakini ni baada ya kufanyika kwa mawasiliano meengi yaliyojaa urasimu kibao. ni baada ya kama saa moja hivi aliambiwa haitowezekana yeye kupata malazi katika quarters hizo. namwisho wa siku ilivuja kwamba ni mh Kinana alikataa kwakuwa ingeshusha hadhi ya gheto la rais. Sasa swali pale ni Ikulu?

    ReplyDelete
  10. USD 15,000 ni shule ngapi zingalipata madawati jamani watanzania wenzangu?

    ReplyDelete
  11. HIYO NI HATI YA MADAI SIYO RISITI,RISITI YA SELIKALI NI NDOGO NA INA RANGI YA NJANO.TAFADHALI TUONYESHE RISITI,ILI UTUOKOE SISI WANACHAMA WAADILIFU WA CCM.

    ReplyDelete
  12. tuonyeshe risiti si hati ya madai.

    ReplyDelete
  13. Ni US Dolars jamani lo mbona mnapenda mizengwe wabongo baada ya hapo mtasema ooh Hela hiyo ingefanyiwa kitu kingine cha maana

    ReplyDelete
  14. hii nchii hi,hawa viongozi wetu hawaoni kabisa nini kitatokea mbele......

    ReplyDelete
  15. mi swali langu moja tuu hapa je CHADEMA nao wanaruhusiwa kukodi ndege hiyo au CCM na WAMA tuu wadau nisaidieni.

    ReplyDelete
  16. sio tshs 15,000/= ni dola za marekani ($) 15,000/= kwa masaa matano. kila saa moja ni dola 3000. kwa fedha ya tz ni shs milioni 22 na laki tano(22,500,000/=) kasome hesabu.

    ReplyDelete
  17. Jamani mi siasa sizipendi,,ila nataka nimrekebishe mdau wa tatu,,hiyo invoiuce ni ya dola 15,000/= na siyo elfu 15,000/=

    Tunaomba wato maoni waendelee kutupa data

    ReplyDelete
  18. jamani watanzania wenzangu inatia uchungu na huruma kuchezewa akili zetu kama watoto wadogo. hivi ni lini watapatikana viongozi wenye kuchukua dhamana ya mamilioni ya watanzania na wenye nia ya kweli. NAUMIA SANA NINAPOONA WATU KAMA AKINA KINANA AMBAO FAMILIA ZAO ZIMESHEHENI NEEMA WAKIONYESHA INVOCE ZISIZO NA KICHWA WALA MIGUU AFU MICHUZI NA YEYE KWA USHABIKI WAKE AMA NJAA YAKE KM WALIVYOWENGI KUBANDIKA BILA TATHMINI YOYOTE YA KINA!! NASEMA NIMECHOKA KWA KILA HALI NA MUNGU ATAWAHADHIBU KWA KUDANGANYA UMA WA WATZ HASA KTK UMRI MKUBWA KIASI HICHO

    ReplyDelete
  19. CCM tumewachoka kila mtu mwenye akili anajua kuwa hizo document si ajabu mmezifoji,tumechoka na maamuzi mabovu ya serkali na kukingiana kifua,Rwanda walikuwa chin yetu lakin angalia kasi yao ya ukuaji,Kenya wana mpango wa kujenga bandari mpya, sisi ni kuahidi kujenga barabara na mkichaguliwa ni kujenga bunge jipya au tumbo

    ReplyDelete
  20. HIVI UNAPOSEMA KINANA ASAWAZISHA MAMBO UNAKUWA UNATAKA KUMAANISHA NINI? TOA U-CCM WAKO HAPA

    ReplyDelete
  21. Ni USD 15,000 sio TSHS

    ReplyDelete
  22. jamanieeeeeeee!jaribuni kuwa walevu iyo ni u.s.d elfu kumi na tano sasa ingiza kwnye madafu.ushambiwa mwenye nacho atangezewa kuwa nacho nyinyi kaeni kupiga kelele tu.kama vipi na nyinyi gombeni ujumbe wa nyumba kumi uko mitaani

    ReplyDelete
  23. Salaam,

    Binafsi sipo upande wowote, lakini ninachoona kinasomeka hapo ni USd 15,000/- kama nimeona vizuri.Ama kwa upande wa kukodi ndege kuna rules na regulations za kukodi ndege, kuna ambazo zinasema utakodi ndege tupu na wewe mwenyewe kulipia marubani na wahudumu, na kuna unayokodi kwa wakati maalum kama sikosei na kuna ambayo utakodi ndege pamoja na wahudumuwake, sasa huenda festi ledi ametumia hiyo facility ya masaa ambayo labda ndio rahisi, na pia inakuwezesha kwenda mahali popote mradi tu huzidishi masaa matano,

    Sina hakika zaidi nilisoma shule aina ya kukodi ndege

    Kila la Kheri TAnzania,

    ReplyDelete
  24. wajameni someni vizuri kabla ya kukurupuka,hiyo risiti inaonyesha ni dola 15000/= pesa ya wadanganyika iliyotumika kumsafirisha huyo mama akakampeni CCM,na mkumbuke hiyo ni gharama ya usafiri tu,bado malazi,chakula, posho kwa yeye na wapambe wote waliomsindikiza.kwa mahesabu ya chapchap gharama zote si chini ya dola 50,000/=asanteni sana,mi nabadili na uraia kabisa maana hii kuumizana namna hii inauma sasa potelea karibu uitwe mtumwa.BOKSI OYEEEEEE!ntarudi siku CCM ikiachia ngazi

    ReplyDelete
  25. Hivi inakuwaje kwenye hii digital age bado invoices zinaandikwa kwa mikono badala ya kuwa computer generated? Tunatunza vipi kumbukumbuku ya documents nyeti, mfano mzuri ni hizi kama hizi receipts za gharama za uchaguzi mkuu za CCM? na pia tuta guarantee vipi "authenticity" yake? Wale wanaofanya kazi za accounts payable mnaelewa haya matatizo inapofikia wakati wa kulipa bill.
    -Phatlorenzo-

    ReplyDelete
  26. Jamani hizo si Tzs ni USD, ila kiukweli tunatakiwa kubadilika, haya sasa ni maisha gani, mi najua risiti za serikali hazipo hivyo, tena pia je inaruhusiwa kukodi ndege za serikali?
    TUAMKEEEEEEEEEEEEEEEE,
    Wanaoshabikia hicho chama wana maslahi yao, acheni kulala

    ReplyDelete
  27. JAMANI HIZO SIO SH 15,000 BALI NI USD 15,000 AMBAZO NI SAWA NA MILIONI 22.5(TSH 22,500,000)

    ReplyDelete
  28. USD sio Tzsh ila Still Mh hiyo Pesa si bora yangefanyiwa mambo mengine?

    ReplyDelete
  29. Yaani serikali nayo inapokea malipo kwa US Dollars? Gavana alisema malipo yote nchini yanapaswa kufanyika kwa TSh. Sasa kumbe hata vyombo vya serikali haviheshimu pesa halali ya Tanzania, tunaelekea wapi?

    ReplyDelete
  30. Hii nati inanitia wasiwasi. CCM are capable of anything. Nadhani iliandaliwa chapchap baada ya Slaa kurusha kombora lake.

    ReplyDelete
  31. hiyo fedha ni ya ccm. mlipotuma sms zenu mliyegemea nini? ccm wanapata ruzuku nyingi serikalin kutokana na wingi wa wabunge na asilimia ya kura alizopata mgombea wake mwaka 2005. ina vyanzo vingi vya mapato mfano ccm kirumba majengo wamepangisha nk.kwa makusanyo ya miaka mitano wanaweza kukodi mandege sio ndege. mbona chadema wanakodi helkopta hamuulizi vyanzo vya fedha wamepata wapi na hawana vitega uchumi vya chama? au billicanas ni ya chadema?
    Chama kina wanachama si chini ya milion 2 wana hela za kuwatosha. wapinzani wasipige kelele jipangeni kisawa sawa kuwang'oa ccm madarakani.

    ReplyDelete
  32. tumechoka na hii serikali ya wezi.
    Na wewe Michuzi kutuletea huyo Riziwani kila siku kwa nini? Hivi ni yeye pekee anayefanya kampeni? Mbona hutuletei vijana wenye uchungu na nchi kila siku-Mfano: mtanzania mwenye uchungu na nchi na maendeleo yake-John Mnyika.

    Wapinzani muungane sivyo wezi watakula watatoka na watoto wao wataingia kuendelea kula walichoacha wazazi wao.

    Watanzania tuamkeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...